Tujikumbushe vita vya pili vya dunia, vitu 15 vya kustaajabisha

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Hii ni vita ya aina yake iliyojaa mauwaji, uwongo, fitna, mbinu, ubabe na matukio mengi ambayo kila kukicha yanazidi kujulikana na kustaajabisha dunia.
Pitia hizi kadhaa,

1.Mpiganaji wa KIJAPAN aliyekuwa anaongoza kikosi chao maeneo ya ufilipino aligoma kujisalimisha hata baada ya VIta kuisha (kupigwa mabomu ya ATOMIC), alikuja kusijalimisha na kukubali kushindwa miaka 30 baadae mwaka 1974 baada ya kushawishiwa na wenzake.
Japanese soldier who refused to surrender for decades dies at 91 - CNN.com
140117080502-01-hiroo-onoda-restricted-horizontal-large-gallery.jpg


2.Dicteta na mtawala wa kirusi Generali Stalin inasemekana aliuwa watu wengi kuliko hata hitler. Hitler aliuwa watu 12 Millioni wakiwemo wayahudi mill 6 wakati yeye aliuwa hadi 25 million kwa kuwanyima chakula na njaa.
Hitler vs. Stalin: Who Killed More? » WFJCSHD: World Federation of Jewish Child Survivors of the Holocaust and Descendants
holo-300x244.jpg


3:Japan na Urusi hadi leo hawajasaini mkataba wa kuhitimisha vita vya pili vya dunia kutokana na kugombea kisiwa kiitwacho KURIL.
Japan–Russia relations - Wikipedia, the free encyclopedia
1366352472.jpg


4:MAlkia ELizabeti II alifanya kazi kama fundi wa magari na Dreva katika vita hivi.
8 Things You May Not Know About Queen Elizabeth II - History in the Headlines
Queens%20Diamond%20Jubilee


5:Msikiti wa Jiji la paris ulisaidia kuokoa maisha ya WAYAHUDI kutokuuwawa na Hitler baada ya kuwapa vitambulisho vyao ili waonekane ni waislamu.
The Great Mosque of Paris that saved Jews during the Holocaust - Week's End
PA-12289105.jpg


6:Soda ya fanta ilivumbuliwa ujerumani , baada ya ugumu wa kupeleka unga wa kutengenezea Coka Cola kutokana na WW2. WaNAZI wakaamua kutengeneza hii fanta tunayokunywa leo.
Fanta - Wikipedia, the free encyclopedia
283px-FantaLogo.svg.png

7:Hitler alikuwa na Mpango wa kutengeneza jumba la makumbusho ambalo angewaweka wayahudi kadhaa humo kama kumbukumbu ya uwepo wa watu wao baada ya kuwa amewaangamiza wengine wote.
Hitler planned to collect thousands of Jewish artifacts to build a"Museum of An Extinct Race"after the war.
Most Shocking Revelations About Adolf Hitler
2127676_1433094596651.jpg


8:Mpango wa Hitler kwa Moscow ilikuwa ni kuifumuafumua yote na kuuwa wakazi wote kisha kutengeneza ZIWA hapo(man made lake).
Reichskommissariat Moskowien - Wikipedia, the free encyclopedia
ad_168134347.jpg


8:(WWI: INGIZO MAALUMU )Katika hali ya kushangaza SIKU YA KRISMASS 1914, wanajeshi wa ujerumani Mstari wa mbele na uingereza walisitisha kupigana, wakakutana kwenye mitaro na mahandaki yao wakacheza mpira, vuta sigara, soma vitabu, story, wengine drafti wengine wakakumbatiana bila viongozi wao kujua, kesho yake wakaendelea kupambana kama kawaida.
Christmas truce - Wikipedia, the free encyclopedia
Meeting the enemy: Tales of extraordinary camaraderie between British and German soldiers
truce-football.jpg

WWI-422689.jpg


9: Ukweli kwamba karroti zinasaidia kuona Usiku au macho sio sahihi. Huu ulikuwa ni ujanja na mbinu za kiinteligjensia za waingereza kuwadanganja wajerumani waamini kuwa marubani wao wanaona sana usiku kwa sababu wanakula sana karroti kumbe kiukweli walikuwa wanatumia RADA.
lots-o-carrots-670.jpg


10:Vita vilipoanza Wanyama na nyoka wote waliokuwa wanafugwa katika ZOO au sehemu ya maonyesho jijini london waliuliwa kwa hofu hiyo sehemu kupigwa bomu na wanyama hao wakali wakiwemo nyoka wenye sumu kusambaa jiji zima.
ZSL London Zoo during World War Two
_78606097_lion-regents-park.jpg


11:Miji ya Hiroshima na Nagasaki kwa sasa Haina madhara ya mionzi ya bomu la atomic la wakati wa vita vya dunia. Madhara makubwa yaliwapata wale waliopitiwa na mionzi hiyo na wamam ikiwemo wamama waliokuwa na mimba. Sababu kubwa ni kwamba hilo BOMU halikugusa chini, lilipikia angani kabla ya kutua ardhini. Bila Mabomu hayo kuna uwezekano mkubwa hadi leo vita visingeisha maana wajapan waligoma kusalimu amri.
Hiroshima and Nagasaki: The Long Term Health Effects

nuclear.jpg


12:MECHI YA KIFO
Hii ni mechi ya ajabu kabisa katika historia ya FOOTBALL iliyochezwa wkti wa hivi vita vya dunia.Ilichezwa team ya Kutoka UKRAIN KEIVE CITY na timu ya wanajeshi wa KInazi kutoka ujerumani. Refa alikuwa mwanajeshi akipendelea WANAZI 9/8/1942. PAmoja na kipa wa kisovie/ukrain kuchezewa faulo za kila aina ikiwepo kupiwa mateke ya vichwa huku akiwa ameshadaka mpira wanazi bado walifungwa 5 kwa 2. madhara ya ushindi kipa aliuwawa, wachezaji wengine waliteswa na kufa na wengine wakatukimkishwa
The Death Match - Wikipedia, the free encyclopedia
article-2127854-128981FF000005DC-436_634x344.jpg


13:Wachina waliouwawa na wajapani katika vita hivi ni wengi kuiko waisrael waliouwawa katika HOLOCOST.
Japanese war crimes - Wikipedia, the free encyclopedia
63-Japan-Apologies-for-World-War-II-02.jpg


14:Waziri mkuu wa uingereza WInston churchill aliyeongoza vita hivyo na kumshinda Adolf Hitler 1945. Aliporudi kugombea mwaka huo kwenye uchaguzi alishindwa.
BBC - History - World Wars: Why Churchill Lost in 1945
50th-Anniversary-Death-of-Winston-Churchill-Facts-About-Sir-Winston-Churchill-554789.jpg


15:Adolf Hitler alipomtaalifu rais wa Chekislovakia kuwa ndani ya muda mfupi wataivamia nchi hiyo. rais Ha'cha alipata HEART ATTACK, ilibidi alazimishwe kuwa macho ili asaini mkataba wa kujisalimisha kwanza.
The History Place - Triumph of Hitler: Nazis Take Czechoslovakia
AKG120351.jpg

karibuni wadau
 

Attachments

  • upload_2016-2-14_1-4-12.jpeg
    upload_2016-2-14_1-4-12.jpeg
    10 KB · Views: 116
mkuu hiyo #6, soda ziligunduliwa ufaransa during french revolution, ndo wakagundua kuanzia caustic soda, kapitie vizuri.
 
mkuu hiyo #6, soda ziligunduliwa ufaransa during french revolution, ndo wakagundua kuanzia caustic soda, kapitie vizuri.
PITIA SOURCE MKUU, HATA NENO FANTA LIMETOKANA NA NENO LA KIJERUMANI FANTASIE.
YAWEZEKANA NI KWELI KWA MAANA YA ORIGIN LAKINI SPECIFICALLY SODA AINA YA FANTA ,
MWEZI WA PILI 2015 ILIKUWA NI SHEREHE YA MIAKA 75 YA KUVUMBULIWA KWA FANTA UJERUMANI
 
Safi sana, lakini kubwa zaidi ni hii ya wapiganaji wa pande 2 hasimu kusitisha vita kwa muda wakapiga kilaji na kudance halafu kesho yake kichapo kikaendelea kama kawaida.
 
Usiamini kila kitu humo, Ishu za kwamba Hitler alitaka kuigeuza Moscow kuwa ziwa ni mambo ya propaganda tu, na ishu kwamba Stalini aliua watu wengi zaidi ya Hitler nao ni uzushi tu. Recodi za vifo vya WWII ni vya kukisia tu hakuna hesabu kamili mpaka leo na hii ni kutokana na vita kupiganwa maeneo mengi ya Dunia, Wewe unazani kwa Africa nani alrecodi Vifo?
 
Usiamini kila kitu humo, Ishu za kwamba Hitler alitaka kuigeuza Moscow kuwa ziwa ni mambo ya propaganda tu, na ishu kwamba Stalini aliua watu wengi zaidi ya Hitler nao ni uzushi tu. Recodi za vifo vya WWII ni vya kukisia tu hakuna hesabu kamili mpaka leo na hii ni kutokana na vita kupiganwa maeneo mengi ya Dunia, Wewe unazani kwa Africa nani alrecodi Vifo?
ndio maana nimeanza na vita hivyo vilijaa uongo, ubabe, propaganda na kila aina ya mambo.
Kwa sababu hata sababu za WWI na WWII bado hazijawahi kueleweka vizuri from conspiracy view
 
Back
Top Bottom