NETANYAHU awashitumu Waislamu kwa kumshawishi Adolf Hitler awauwe Wayahudi

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Katika video inayosambaa mtandaoni inamuonesha waziri mkuu wa Israel, Netanyahu akiwashutumu waislamu kwa kumshawishi Adolf Hitler kuwauwa na kutaka kutokomeza taifa hilo. Adolf Hitler aliacha historia isiyosahaulika kwa waisraeli kutokana na mauaji aliyoyafanya dhidi wayahudi, ambayo yalipewa jina la "THE HOLOCAUST". Katika video hiyo Waziri mkuu wa Israel, Netanyahu alisikika akisema;

Hitler hakutaka kuwaangamiza wayahudi kwa kipindi kile, bali alitaka kuwafukuza wayahudi, na Haj Amin al-husseini alienda kwa Hitler na kusema, "Ukiwafukuza watakuja hapa" (akimmanisha kurudi Palestina). "Kwa hiyo nifanye nini kwao" Hitler aliuliza. Haj Amin al-husseini akasema "Wachome moto".

Kwa kauli ya Netanyahu anamaanisha Adolf Hitler hakutaka kuwaua wayahudi, lakini waislamu walimshawishi afanye hivyo.

Tizama mahojiano hapo chini.

View: https://www.instagram.com/reel/CydEbv2q-rv/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==
 
Na ndio mzizi wa Antisemitism ulipoanzia hapo, ndiyo maana Nazi iliwabidi kwanza waanze na kuwarushia lawama wayahudi kusababisha Ujerumani kushindwa vita ya kwanza ya dunia.
 
Katika video inayosambaa mtandaoni inamuonesha waziri mkuu wa Israel, Netanyahu akiwashutumu waislamu kwa kumshawishi Adolf Hitler kuwauwa...
Ukweli ninkuwa WAYAHUDI walifanya khiyana katika vita vya kwanza vya dunia hasa wale waliokuwa upande wa UJERUMANI ili upande wa MWINGEREZA ushinde na WAO wapewe zawadi ya TAIFA LAO kwenye eneo la PALESTINE

Hitler alilifahamu hili na ALIAMUA KUWAANGAMIZA kwa sababu ya USALITI wao kwa Wajerumani....
 
Netanyahu is trying to play his cards tu ila sio kweli, tatizo la netanyahu anawachukia waislamu kwasababu ndio threat kwake na kwa taifa lake at the moment, anapambana sana na nchi kama iran ambayo anaamini kuna siku ikipata chochote cha kuifuta israel itafanya hivyo.

Anaona upinzani anaopata globally kutoka kwa waislamu kila anapojaribu kuitanua israel au kufanya uonezi kwa Palestine.

Huyu netanyahu ukisoma kitabu cha obama alimuelezea vizuri kwamba ni mtu muongo muongo na mwenye uwezo mkubwa wa kushawishi, there is a very thin line between evil and intelligence the guy is evil
 
Sidhani kama Kuna ukweli wowote,,coz main reasons ya Adolf hitriler kuwaua waisrael ilikuwa ni usaliti wa wa waisrael katika vita ya kwaza ya Dunia...
Elewa mantiki ya hoja yake

Sawa tunakubaliana na maoni yako, ila sasa baada ya hayo yote kutokea na kupelekea Adolf Hitler kuwakamata, Netanyahu anasema Adolf Hitler alitaka kuwarudisha (Expel) warudi walipotoka, ndipo Haj Amin al-husseini akaona watarudi na kukaa kwenye ardhi ya palestina akaamua kuwachomesha kuwa wauwawe hili wasirudi.

Sasa wewe baada ya kuongelea baada ya kukamatwa, unaanza kuturudisha nyuma ya Historia... Sawa tunakubali hawakutoa support kwa Ujerumani kitu kilichomkasirisha Adolf, lakini hapa Netanyahu anazungumzia kwa nini walivyokamatwa wakauwawa badala ya kurudishwa kwao
 
Ukweli ninkuwa WAYAHUDI walifanya khiyana katika vita vya kwanza vya dunia hasa wale waliokuwa upande wa UJERUMANI ili upande wa MWINGEREZA ushinde na WAO wapewe zawadi ya TAIFA LAO kwenye eneo la PALESTINE

Hitler alilifahamu hili na ALIAMUA KUWAANGAMIZA kwa sababu ya USALITI wao kwa Wajerumani....
Ukimsikiliza Netanyahu anasema Adolf Hitler alikuwa hana plan za kuwaangamiza alitaka kuwarudisha walipotoka... Ila Haj Amin al-husseini akaogopa watarudi Palestina akaenda kumshawishi wauwawe hili wasirudi Palestina... Hiyo ya vita ya kwanza hakuna anayekupinga, lakini sisi hapa tunaongelea kwanzia waisraeli walivyokamatwa na plan za Adolf Hitler kutaka kuwarudisha ila akashawishika kuwawuwa ambapo lawama anawapelekea waislamu
 
Netanyahu is trying to play his cards tu ila sio kweli, tatizo la netanyahu anawachukia waislamu kwasababu ndio threat kwake na kwa taifa lake at the moment, anapambana sana na nchi kama iran ambayo anaamini kuna siku ikipata chochote cha kuifuta israel itafanya hivyo.
Anaona upinzani anaopata globally kutoka kwa waislamu kila anapojaribu kuitanua israel au kufanya uonezi kwa palestine
Huyu netanyahu ukisoma kitabu cha obama alimuelezea vizuri kwamba ni mtu muongo muongo na mwenye uwezo mkubwa wa kushawishi, there is a very thin line between evil and intelligence the guy is evil
Ukisoma vizuri historia ya uongozi wa Israel... Netanyahu anafata tu maagizo ya serikali, kwa sababu yeye sio waziri mkuu wa kwanza kupigana vita na waarabu.

Kupigania ardhi ni Israel ni mpango wa serikali nzima na si ya kiongozi, hata leo akitoka Netanyahu anayefuatia nae atafanya hayo hayo...

Na huu ndio uongozi wa nchi zilizoendelea, hata Marekani maraisi wanaendeleza mipango ya rais aliyepita hususani kwenye kupambana na maaadui na kupata ushawishi kimataifa....

Ukisema Netanyahu ni muongo muongo ni bora useme viongozi wote wa Israel na mawaziri wakuu waliopota nao ni waongo kwa sababu Netanyahu anachokifanya leo kimekuwa kikifanywa na mawaziri wakuu waliopota pia.
 
Ndiyo kusema kichapo kutoka kwa Hamas kimemfanya aweweseke, au!! Halafu ile vita ya ardhini ya kuivamia Gaza na kuwaua wanamgambo wote wa Hamas, itaanza lini?
Fatilia habari... Vita ya ardhini imeshaanza, na hivi sasa wanafumua maandaki ambayo yalijengwa na Hamas... Na wameshatoa Onyo kuwa raia wote waondoke, ukikutwa unazurula na haujaondoka wanajua wewe ni miongoni mwa Hamas wanakumiminia risasi... Kuna video kadhaa zinaonesha Jeshi la Israel kwa mguu limekutana na wanaume kadhaa ambao kama walikuwa wanaonekana wanadhurura badae wakamiminiwa risasi
 
Katika video inayosambaa mtandaoni inamuonesha waziri mkuu wa Israel, Netanyahu akiwashutumu waislamu kwa kumshawishi Adolf Hitler kuwauwa na kutaka kutokomeza taifa hilo...
Wapi kasema Waislam?
 
German pamoja na kupigwa vita mara mbiki na kugawanywa but ndio taifa lenye uchumi mkubwa ulaya na teknolojia ya ajabu. Wajerimani ni wstu waliobarokiwa akili sana. Hivyo hawawezi shawishiwa na mwarabu, bali walitumia akili yao.
Napenda sana spirit ya ujermani.
Islael wangekuwa na uwezo wangelipiza kisasi kwa mjerumani sio kuhwngsika na mtotoo mdogo Palestina.
 
Wewe uliyeleta hapa hizi pumba na huyo yeriko wote kwanza ni washamba kwa kuupelemba huu ujinga hata mtoto wangu wa miaka 10 anaushtukia....
Huyu yericko kwanza aliishia la 4b hawezi kujua ni maana ya deep learning yenye matokeo ya deep fake...
Na hii sio deep fake, huu ni utumbo wa ze komedi, mtu anapandikiza sauti ya mjinga mmoja anayejaribu bila mafanikio kiuga sauti ya huyu kenge...
Hata ndimi haziendani na maneno..
Kweli watanzania wengi wana madudu kichwani.....
 
German pamoja na kupigwa vita mara mbiki na kugawanywa but ndio taifa lenye uchumi mkubwa ulaya na teknolojia ya ajabu. Wajerimani ni wstu waliobarokiwa akili sana. Hivyo hawawezi shawishiwa na mwarabu, bali walitumia akili yao.
Napenda sana spirit ya ujermani.
Islael wangekuwa na uwezo wangelipiza kisasi kwa mjerumani sio kuhwngsika na mtotoo mdogo Palestina.
Yana Israel Wakalipize kisasi Kwa ujerman kisa Adolf hitriler na ukichaa wake.yani mfano Tanzania twende tukaiangamize Uganda kisa idd Amin alituulia ndugu zetu, hizo akili matope.
Au hujui wajerumani wenyewe walilaani vitendo vya aldof likiwemo Hilo la kuwaua waisrael.
 
We hupendi kulipiza kisasi. Sasa kuna watu duniani hulipiza kisasi hata ipite miaka 200 kisasi kinaenda kwa vitukuu. Wangekuwa na uwezo wangelipiza kisasi tu.
 
We hupendi kulipiza kisasi. Sasa kuna watu duniani hulipiza kisasi hata ipite miaka 200 kisasi kinaenda kwa vitukuu. Wangekuwa na uwezo wangelipiza kisasi tu.
Kulipiza kisasi Kwa watu wasio kuwa na hatia ni upumbavu wa hali ya juu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom