Tujikumbushe Tabia za wapishi Sekondari za Bweni

Tujikumbushe Tabia za wapishi Sekondari za Bweni

Life2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,387
Reaction score
4,880
Gombana na mtu yeyote shule za sekondari za bweni ila sio mpishi hasa kwa sisi wadau ambao muhula mzima unahudhuria kitchen utaona shule ngumu mchinjo kwa kwenda mbele.

Basi tujikumbushe kidogo tabia/sifa za wapishi wetu hasa shule za bweni.

Nakumbuka o-level hakukuwa na shida sana kwani tulikua tunalia kwenye madishi shida ilikua sisi kwa sisi hasa siku za wali,Nyama na matunda ukichelewa siku izo DH andika maumivu,pia wapishi walikua powa hata ukiwaomba TOP LAYER wanakupa.

Shughuli ilikua A-level hapa ndo nkajua kanuni ya STRUGLE FOR EXISTENCE AND SURVIVAL FOR THE FITTEST inafanya kazi.Mpishi alikua noma sana akiwa na uwezo mkubwa wa kukariri watu ilituwia vigumu sana kupiga paper two/kurudia msosi mara ya pili hata ukabadilishe nguo atakujua tu wengine wakawa wanavaa mpaka sweta zenye kofia lakini bado aliwashika tu.

Alikua bingwa wa kupiga Mchinjo hasa siku za wali daa unaeza kutoka jikoni unalia unapewa wali hata dakika 5 haziishi ushamaliza kula ila wengne wanatoka bakuli zimejaa.

Siku ya kugawa nyama hakosei idadi japo haesabu zikizidi anatoa jifanye mbishi sasa ukimbie nazo utapigwa mchinjo mpaka utaomba msamaha mwenyewe.

Staili yake ya kugawa ugali ilikua kiboko anakurushia ugali kabla hata hujafika kwenye sufuria ukichelewa kukinga sahani na ugali kudondoka imekula kwako iyo labda huruma akupe mwingine ila ujazo unapungua.

Kumkuta anacheka ilikua nikwa nadra sana bize 24/7.

Nimekumbuka ayo kwa kifupi,karibu nawe utukumbushe tabia/sifa za wapishi wenu.
 
Mimi nakumbuka ule wizi wao tu.

Wanaiba maharagwe,mafuta ya kula na mchele wakishirikiana kwa zamu.

Baada ya hapo ni kwenda kuwauzia wauza maduka kwa bei ya kutupa.
 
Nikiwa form II aliniomba mkopo wa shs 20/=. Usihangae narudia shilingi ishirini. Bahati nzuri nilikuwa nayo nikampa. Hakunirudishia wala sikumuomba ila siku za zamu yake alikuwa ananiwekea chakula hata kama sipo.
 
Hao wapishi noma saana kwanza wachafu na wakiwa wanapika jasho linaangukia ndani....

Anyway Siku moja nakumbuka uboyzini huko katika kusave mboga.

Foleni ilikuwa ndefu mnoo, watu Wa mbele wakawa washapata msosi wanaendelea kula,

Mpishi ile anakoroga maharage kwenye sufuria ili yajichanganye na mchuzi kupandisha mwiko ukaibuka na tambara la deki....

Duh watu tulitaman kutapika, mpishi alichezea vitasa vingi...
Mnoo.....
Kuna Siku za mboga za majani hawa jamaa walikuwa hawazikati kati walikuwa wazembe... Unakula chainizi lile jani lake zima. Tulikua tunayaita magazeti.
 
Hao wapishi noma saana kwanza wachafu na wakiwa wanapika jasho linaangukia ndani....

Anyway Siku moja nakumbuka uboyzini huko katika kusave mboga.

Foleni ilikuwa ndefu mnoo, watu Wa mbele wakawa washapata msosi wanaendelea kula,

Mpishi ile anakoroga maharage kwenye sufuria ili yajichanganye na mchuzi kupandisha mwiko ukaibuka na tambara la deki....

Duh watu tulitaman kutapika, mpishi alichezea vitasa vingi...
Mnoo.....
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] uliendelea kula hiyo menyu? Mambo ya boarding school hayo
 
Hahahahaha tulikua na Mpishi mmoja alikua mnoko balaaa alikua anaitwa Mzee Frank ila mwenzie alikua safi sana hadi tukawa tunamuita Gatho,alikua ananyoa kama Gatho kwa mnaomkumbuka mwanamuziki wa Congo aliyevuma sana miaka ya 1994-95; ukifika tu ukimwambia Mzee unafanana sana na Gatho lazima akujazie bakuli.

Siku moja sifa zikazidi, watu wakamwambia unafanana na Yondo Sister, huyu nae alikua mwanamuziki wa Congo enzi zile hakukua na akina Bongo flava. Siku moja akaja kuonyeshwa Yondo Sista mwenyewe alivyo kwenye Cover ya Kanda!! Kilinuka
 
mtoa mada kama A LEVEL umesoma lyamungo.??

hizo tabia alikua nazo mpishi mmoja anaitwa MANASE aka ZIZUU.
Aiseee huyu jamaa hapana aisee. Sema nn mtoa mada hajasoma lyamungo mana amesema ishu ya kukimbia na nyama, kwa zizuu tungeshazika siku nyingi. Yule jamaa ni ka israel tuu,, alishanipigia mtu dishi la kichwa nikajua kaua. Zizu hakua mtu wa mchezo mchezo kwa kweli
 
Mmenikumbusha Malata enzi hizo,mnenikumbusha kitchen force, Nzowa, alikuwa baunsa,yan unaweza ukakosa menu kwenye table yenu, wakati huo,,,,,,
 
Ok nimesikia tu kwa wadau mbalimbali waliokulia boarding, binafsi sijakulia mazingira ya boarding, THUG LIFE STREET LIFE......
 
Nikiwa form II aliniomba mkopo wa shs 20/=. Usihangae narudia shilingi ishirini. Bahati nzuri nilikuwa nayo nikampa. Hakunirudishia wala sikumuomba ila siku za zamu yake alikuwa ananiwekea chakula hata kama sipo.
Nahisi uliondoka shule na kitambi aise.
 
Back
Top Bottom