Tujikumbushe 'streotypes' za zamani

SnowBall

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,054
2,840
Jamani nakumbuka nilipokuwa mdogo kulikuwa na imani za ajabu ajabu 'streotypes' katika makabila mbalimbali sina uhakika kama bado zinaendelea..
Mfano tulikuwa tunaambiwa..ukikalia yale mafiga kwa kule vijijini kwamba utakuwa mfupi!
..uking'oa jino ukilitupa batini basi hayataota meno mengine..
Mnaweza kuendelea na nyie kwenye maeneo yenu!!
 
Ukikutana na Albino jitemee mate mwilini !!

Kama mkiwa watoto mnakunywa chai, mwenzenu mmoja akiitwa, akiacha andazi lake eti analipigia dungudungu! Basi hakuna atakaegusa andazi hilo, eti ukilidokoa tu mom wako anadedi .
 
Kweli ilikuwa noumer..
 
Ukichelewa shuleni asubuhi chukua kijiti chomeka kwenye nywele(zamani nywele ndefu ndo fasheni), huchapwi na mwalimu yeyote ng'oo!
 
Ukinyooshea kaburi kidole kinabaki hivohivo,
Ukikata kucha usiku utakua masikini,
Ukiokota hela njia panda utapata masambatuta,
Ukila ukiwanumelala mama yako atakufa,
Ukikojoa barabarani lazima utemee mate mikojo
 
Ukikutana na Albino jitemee mate mwilini !!

Kama mkiwa watoto mnakunywa chai, mwenzenu mmoja akiitwa, akiacha andazi lake eti analipigia dungudungu! Basi hakuna atakaegusa andazi hilo, eti ukilidokoa tu mom wako anadedi .

Hapo kwenye DUNGUDUNGU umeniacha hoi zilikua ndo zangu.
 
Hii hadi leo dunia ya Www.com bado inatumika!
> Nenda usiku kwa muuza duka, then mwambie nataka Chumvi na pesa unayo mkononi hakuuzii, labda uje na kusema "nipe dawa ya mboga"
 
Nikiwa darasa la kwanza, eti nilikua nikijua kwamba siku ya kufanya mtihani, basi atakaemaliza wa kwanza kumaliza mtihani na kutoka nje ndiyo wa kwanza ktk mtihani husika.
 
Ukipiga mluzi usiku unawaita waliodedi...
Hakuna kufagia mabaki ya msosi, eti waliodedi huwa wanakuja usiku kugonga hayo masalia...
Kuku akichinjwa Dingi peke yake alikua anapewa paja, firigisi na maini...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom