Tujikumbushe mambo Enzi za Mwalimu

duh kweli kaka..hii kitu naikumbuka plus vizibo vya soda unavitoboa halafu unavifunga kwa kamba katikati ukivitupia shingoni weye ndie mtabe school zima
 
wazazi wenyewe ndo mnawafanyia watoto shopping, unamwambia arodheshe mahitaji yake yote then mwisho wa siku unaenda mwenyewe dukani na kumletea mahitaji yake...........so hayo mengine atayajuaje...............na vitabu wewe mzazi unamtafutia tena wazazi wengine wana misemo kama mimi nimesoma kwa shida sitaki na mtoto wangu apate shida so ni mfumo tu uliopo sasa.
 
Sie tuliosoma shule za kata tulikuwa tunaweka kwenye kopo.
 
Tabia hizi mmekuwanazo mpaka kwenye kuibarasilimali zetu, nyambafuuuuu. Wizi ndio mmeona sifa kumbe ni ujinga

Dah, naona unauzalendo wa ukweli, hiyo ilikuwa michezo ya utoto ila mbona tuliacha tangu form 1 teh, teh dah.
 
ukiipata utakuta ni kimeo hutaamini kama umenunua,utadhani umepewa bure
 
cute we mtoto mayai umejulia wapi hii mambo wakati umesoma International,sisi watoto wa Ngongongare primary ndo tunajua bei ilikua ni 350
 
ukiwa na hili unaonekana wakishua.

Hizi mbona ni za baada ya mwalimu? Zilikuwepo zile ambazo huo mkebe ulikuwa na picha ya daraja na zilikuwa zinatoka china. Na tulikuwa tunaziita "set" na vifaa vyake ndani vilikuwa imara sana na baadhi ya majina yake ni kama- bikari,kipimapembe, pembe tatu, lura nk. Hizo ndo zilikuwa compass za ukweli haya ya sasa ni matakataka tu. Compass gani kila muhula lazima mtoto aiweke kwenye orodha ya vitu vya kurudi navyo shule?
 
Hapana. Mikebe yote hiyo ni ya enzi za Mwinyi yaani 1987 hadi 1996.
ile ya enzi za mwalimu ilikuwa na inabaki kuwa adimu
 
Asante. Hii ndiyo tuliyotumia enzi zetu. Umenikumbusha mbali sana sana.

Na kwa wale waliofanya mahesabu Form 5 and 6 sijui kama mnakumbuka ile calculator iliyokuwa inaitwa "slide rule". Bila hiyo mtihani ulikuwa umefeli.

Mkuu KVM umeikumbuka na hii


​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…