Tujikumbushe kwa takwimu: Taifa la vilaza wa mwendokasi

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
386
(TAKWIMU ZA UFAULU KIDATO CHA NNE (2015) ZINATOA TASWIRA GANI?)

Isangula KG

Hebu twendwe pamoja hapa.

Kulingana na taarifa kwenye Gazeti la Mwananchi zikimnukuu George Simbachawene;

1. Jumla ya Wanafunzi 393,734 (Wasichana 200,919; Wavulana 192,815 ) walifanya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne mwaka jana.

2. Kati ya hao ni wanafunzi 90,380 (wasinchana 36,005; wavulana 54,375) sawa na asilimia 22.95 ya wanafunzi wote ndio waliopata Division I-III (wasiovilaza) na wakastahili kuingia kwenye mchakato wa kujiunga na kidato cha Tano na vyuo vya ufundi.

KWA LUGHA RAHISI
• Kuna VILAZA 303,372 sawa na asilimia 77.05 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne. Hii unaipata baana ya kutoa waliofaulu (Division I-III) kwenye idadi kuu.
• Kati ya VILAZA wote, wasichana ni 164,914 na wakiume ni 138,440
Hawa wote wanaingia mtaani na kwa kuwa mfumo wetu wa elimu na Taifa hauna utaratibu mzuri wa kuwa-absord hawa vilaza wote, twaweza kutarajia kuwaona wasichana wengi wakijiingiza katika shughuli zisizo rasmi kama mabaamedi na machangudoa. Huku wavulana wengi wakijiingiza kwenye biashara ya Bodaboda, wizi n.k.Yaani zile shughuli ambazo kwa kiasi kikubwa zinahitaji NGUVU NYINGI na AKILI KIDOGO sana.

TUENDELEE TENA

3. Kati ya WASIOVILAZA 90,380 wenye sifa za kuchaguliwa kuingia kidato cha Tano na vyuo vya ufundi ni wanafunzi 64, 961 (Wasichana- 28,911, Wavulana-36,050) pekee sawa na asilimia 71.98 wanaliochaguliwa kuingia kidato cha tano kutokana na mfumo wa ‘combination’ na waliochaguliwa kujiunga na ufundi ni 759 (Wasichana 220 na wavulana 539).

SASA BASI

Ukiweka pamoja (64961+759) ni 65,720 ambayo ni sawa na asilimia 72.72 ya wasiovilaza ndiyo wamepata nafasi ya kujiunga na kdato cha tano na vyuo vya ufundi.
Hivyo wasio vilaza karibia 24,660 (24528 kwa takwimu ktk gazeti la Mwananchi) sawa na asilimia 27.28 wamekosa nafasi na naweza kusema wanajiunga kundi la wale vilaza.

HIVYO BASI
4. Ukijumlisha hawa wasio vilaza 24,660 na wale vilaza 303,372 unapata 328,032 sawa a asilimia 83.31 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne wanaingia mtaani
Kwa lugha rahisi, ukiachana na makosa madogo madogo kwenye hizo namba unapozijumlisha, Wasichana 171,788 na wavulana 156,226 wanaingia mtaani.

Kama nilivyosema, mfumo wetu wa elimu haujawaandaa hawa Vilaza (Division IV na Zaidi) na Wasiovilaza (waliokosa nafasi) kupata fursa ya kujipatia kipato kwa shughuli rasmi.

Pia shule na vyuo vya binafsi vikijitahidi sana labda vitapunguza asilimia 3 hadi 10

Kwa MWENDOKASI wa kuona asilimia 83.3 ya wahitimu wote (kidato channe) wanaingia mtaani UKIJUMLISHA na VILAZA wa DARASA la SABA ambao ni wengi Zaidi ya hawa na wale wa form six, TUNAANDAA TAIFA LA WATU AMBAO ASILIMIA KUBWA YA WANANCHI HAWATAKUWA NA SHUGHULI RASMI ZA KUWAWEZESHA KUJITEGEMEA na Kukua kiuchumi kwa Mwendokasi stahili.

Hili ni Taifa la watu wasiokuwa na kazi za uhakika, watu walalamishi na wasio na uwezo wa kuwahoji watawala.....TAIFA LA VILAZA WA MWENDOKASI

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Source: Mwananchi online
 
Ukichambua takwimu hukawii kuulizia cheti cha kuzaliwa cha Bibi yako aliyekufa mwaka 1888 wakati wa Mkutano Mkuu wa Berlin ukifanyika kuigawa Afrika
 
Back
Top Bottom