Tujikumbushe hesabu hii ya Rais Magufuli siku ya uzinduzi wa Terminal 3

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
"Nchi yetu ni tajiri, Watanzania tunaweza, Jengo hili limegharimu Mabilioni ya fedha zaidi ya bilioni 700, fedha hizi zimetolewa na Watanzania kwa asilimia 100, ambapo asilimia 15 fedha taslimu na 85% tumekopa , na mkopo huu utarejeshwa kupitia kodi zetu" - JPM

EA4AyP_W4AA9gCH.jpg
 
We

Weka clip ili nicomment
 
Shida ipo wapi mkuu Salary Slip ? Au hizo 85% na 15%? Mbona kasema vyema tu, hata ukikopa bado ni pesa za Watanzania na zitalipwa kwa kodi zatu.
Hebu niambie wewe ukienda Bank ukakopa pesa zikaingia kwenye account yako utasema pesa ni za Bank au ni za kwako?
 
Kwahiyo hakuna tofauti ya kukopo na kutumia fedha zako kufanya jambo fulani?!
 
Nadhani shida ni kusema hela zimetolewa na watanzania Kwa asilimia 100 alafu hapo hapo unasema tumekopa asilimia 85!
Shida ipo wapi mkuu Salary Slip ? Au hizo 85% na 15%? Mbona kasema vyema tu, hata ukikopa bado ni pesa za Watanzania na zitalipwa kwa kodi zatu.
Hebu niambie wewe ukienda Bank ukakopa pesa zikaingia kwenye account yako utasema pesa ni za Bank au ni za kwako?
 
Kwahiyo hakuna tofauti ya kukopo na kutumia fedha zako kufanya jambo fulani?!
Labda ametofautisha mkopo na fedha za msaada. Msaada hurudishi, mkopo unalipa kwahio umejenga kwa hela zako mwenyewe. Aliekukopesha ameharakisha zoezi la wewe kujenga kwa hela zako.
 
Shida ipo wapi mkuu Salary Slip ? Au hizo 85% na 15%? Mbona kasema vyema tu, hata ukikopa bado ni pesa za Watanzania na zitalipwa kwa kodi zatu.
Hebu niambie wewe ukienda Bank ukakopa pesa zikaingia kwenye account yako utasema pesa ni za Bank au ni za kwako?
Kimsingi pesa uliyokopa siyo yako faida utakayopata ndio yako, na mara nyingi pesa ya mkopo huambatana na masharti, au maelekezo jinsi ya kuitumia hauna uhuru nayo, na katikati ya mradi (bank) inakuja kukagua iwapo pesa yao unaitumia visivyo, ukitumia vibaya bank ina uhuru wa kuja kukutaifisha.

Mfano, umekopa 10,000= ya biashara unapata faida ya elfu moja, jumla utakuwa na 11,000=, huwezi kusema elf kumi na moja zote ni pesa yako, mwenyewe akichukua elf 10 yake utabaki na elf moja ndiyo yako.
 
Maneno hayo angesema baada ya kulipwa pesa yoote,tumesikia huko wenzetu wamekopa kijinga wachina wakataifisha mali zao. Huwezi jisifu kabla sema ukweli wananchi wenzangu tumekopa tunapaswa kupambana tumalize deni!!!
Tunafahamu matajiri waliowahi kopa na kujenga na kununua migari baadae walikufa kwa presha na familia zao kujikuta hoi baada ya kusifiwa na kujisifu sana hapo awali.
Ogopa MTU asiyejua uchumi na biashara vyema anapokopa ovyo na kupenda kujisifu kwakila afanyacho.
Sifa za kukopa na kujenga jenga kilamahali zisijetufanya tukakwama vibaya hapo baadae. Bunge lishirikishwe vyema rais ajae asijeachiwa mzigo usiobebeka
 
Back
Top Bottom