Tujihesabie maumivu au tuendelee kunywa mtori nyama tutazikuta chini?

Black Opal

JF-Expert Member
Jan 22, 2023
201
263
Kama tumesikia visiwa vinauzwa wageni, mbuga nazo zinabebwa, madini huko nako ni kichomi kingine, bandari imekuja kuongeza msumari wa moto kwenye kidonda halafu wanakuja kukanisha sio miaka 100 ni miezi 12!

Uwekezaji tu uliofanywa ni zaidi ya miezi hiyo, hapo hujaagalia utekelezaji, faida na mambo mengine. Yaani ni changa la macho kweupeeee!

Sawa hatuna uwezo wa kuviendesha wenyewe, ndio tuendelee kufanya bogus deals na kushindwa kuingia mikataba ambayo itatufaidisha? Tumerudi enzi zile za kupewa mawe huku wao wakichukua dhahabu!

Team Ndugai wanaangalia huko na kusema hiiiiiiiii!

katuni.jpg
 
Back
Top Bottom