Tujihadhari na mahouse girl | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujihadhari na mahouse girl

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lekanjobe Kubinika, Jul 23, 2010.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hii ni story ya kweli kabisa. Hebu fuatilia kwa faida yako. Ukiona mwenzio ananyolewa kitie maji kichwa chako.

  Mdogo wangu mmoja pale Dodoma anaishi na mkewe, house girl na watoto wawili. mtoto mmoja ana mwaka mmoja sasa. Walipata house girl mnyalukolo kwa ajili ya kulea mtoto zaidi, kwa kuwa mama anasoma, baba anashinda kibaruani, mtoto mkubwa pia anasoma. Kwa hiyo ilibidi wapate house girl wa kukaa na mtoto wakati familia haipo nyumbani kila siku za kazi.

  Mtoto na familia kwa ujumla walikuwa wanauguaugua hapa na pale kama kawaida ya binadamu, lakini baada ya kupata house girl mambo yalibadilika na kuwa hovyo zaidi. Mambo yalianza kiaina pale wiki moja iliyopita mtoto changa alipoanza kuharisha na kutapika mfululizo, wazazi wakachanganyikiwa. Kufika nyumbani jioni walikuta mtoto anajinyonganyonga tumbo na anatapika kila anachowekewa mdomoni. Kuharisha kuliendelea na ndipo wakataka ushauri.

  Wakashauriwa wamtengenezee maji ya dawa mtoto na wampe dawa wakiangalia hali. Kweli mtoto akachangamka kidogo, lakini usiku wa manane hali ikabadilika tena. Asubuhi wakadamka kwenda hospitali ambako manesi walijitahidi kutafuta mshipa wampe drip wasiupate. Daktari akashauri utafutwe mshipa wa kichwani lakini wapi. Maji ya dawa yaliendela kuwekwa kinywani kwa mtoto na aliendelea kutapika kila kitu. Mara baba mtoto akachanganyikiwa na kuanza kulia. Manesi wakamtimua akabakia mama na mtoto. Kufika mchana mama naye akaugua palepale hospitalini naye akaanzishiwa tiba. baba kule kazini naye akaugua hajiwezi. Kule shuleni anakosoma mtoto mkubwa nako aliugua mwanafunzi wa familia hiyo. Kurudi nyumbani, failia nzima ilijikuta inaugua isipokua housegirl tu.

  Kumbe mama yake mke ambaye anaishi DSM na muumini wa Kakobe, katika sala zake aliona kitu kisicho cha kawaida. Alipiga simu kwa mwanae Dodoma akaambiwa hali iliyopo. Akaamua kusafiri kwenda Dodoma na kuikuta hiyo hali. Akaingia magotini na kuongea na Mungu wake kupata ushauri. Usiku huo katika chumba alicholala na housegirl kukawa na maajabu, mapanya yakakutwa yamekufa na yapo mlangoni. mama akahamishiwa chumba kingine. Siku iliyofuata huyo mama (bibi) akakaa na house girl na akaanza kumhoji akimwangalia uso kwa uso.

  "Wewe mtoto, kwa nini unawatesa watoto wangu hivyo?" Binti yule house girl akahamanika, akapatwa na kigugumizi na kujitetea, akisema sio yeye anayewatesa peke yake, bibi yake na wenzake wanakuja kutoka "Ilinga" usiku na wanamlazimisha waingie kuwachezea hawa. Yeye hataki lakini bibi anamtishia. Kwa hiyo house girl akaomba mamaa huyu asiwaambie wenye mji kwamba amesema maneno hayo wasije wakamfukuza kazi maana maisha magumu kwao akirudi.

  Polepole mama huyu akawapa ushauri wanae wachukue hatua za busara kuishiana na house girl huyo. Baada ya majadiliano ya mama huyu na house girl mambo ya afya ya familia yakabadilika na kuelekea unafuu. Usiku walilala vema na mtoto akaruhusiwa kurudi nyumbani kutoka hospitali.

  Walichofanya juu ya housegirl ni kumtafutia lugha kumrudisha kwao bila yeye kutambua kuwa hiyo ndio adios amigo. Hivi tunavyosoma hapa leo hii yule house girl yupo "Ilinga" akidhania kapata likizo na mwenye matarajio ya kurudi kibaoni mara likizo ikiisha ambapo mabosi wake wameahidi kwenda kumchukua wakirudi safari yao ambayo familia nzima inaenda.

  Kikulacho ki nguoni mwako. Majuzi tu tumesikia habari ya mtu kutoka morogoro kuifanya miili ya mabosi wake viwanja vya mazoezi, sasa kutoka "Ilinga" sijui kesho ni kutoka wapi. Unapotafuta house girl hakikisha umeijua background yake. Nenda mwenyewe kijijini au watumie wale unaowajua walioko kijijini unaowaamini. Hao mahousegirl wanaoletwa kama nyanya kwenye Fuso matatizo yao ndio hayo. Kuna wengine anafika leo na wiki moja tu baadaye ni mke mwenza au anagomabia waume za watu majirani na wake zao, au anakuja na lambo lakini mwei mmoja tu baadaye anayo masanduku matatu makubwa yaliyojaa kila aina ya manunuzi. Ukimminya sana unaenda kazini huku nyuma na hasira za swela anavinyonga vitoto vyako au anawanyima chakula na kuwapelekea maboyfriend nje, watoto wakiambulia mchuzi kama wana bahati.

  Mweeeee! Habari ndio hiyo.
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  hiyo ni kweli tena sana tu.....! kuna mmoja ambaye yeye akienda haja huyfunga kwenye ka-(lunchbox) parcel na choo chake kuja kuchukuliwa usiku......! wakataka kuua mtoto kosakosa wakaua mbwa wa jirani........WENGI WA WASAIDIZI WA NDANI NI WALOZI(WACHAWI)
   
 3. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu Lekanjobe,Asante mimi ninakupa kisa chaukweli sijasimuliwa mimi nilikuwaatafuta hgl Bahati nzuri Kuna mgonjwa alikuwa kalazw muhimbili Nikazungumza na babake mgonjwa nikmueleza tatizo langu akasema kwao yupo Songea Tunduru!mnipe nauli nitume sh50000,ikampa kweli hgal nimempoke j4 pale ubungo saa2 usiku.!!
  Kilichotokea akawa anaumwa kichwa!!Baadae wife akamuuliza mbona unaumwa tangu ufike unaonaje twende hosptal ukatibiwe unaweza kuwa na malaria mtoto asikatae!!!Wife akamuuliza kwanini??Akasema nina mashetani huwa nayalisha wali na nyama!!!kila mwezi wakumi!waifu akamwuliza kwanini uliuja ukijua unamatatizo hayo akasema tuliyaomba yakakubali ndonikaja huku!!!!!Nilivyo rudi home ndoyo history nimeikuta jana Alihamisi!!Nikamwambia wife basi usimwambie kama tunakurudisha!!Na asipewe kazi!,Sasa yule aliyeniletea jana mgonjwa wake amefariki jioni alikuwa anasubiri kupelekwa INDIA bahati mba kafa jana hivyo wanasafirisha kwenda Tunduru Nasijamwambia matatizo ya mtoto aliyeniletea utokana na msiba wa mwanae!!!wapo katika maandalizi ya kusafirisha msiba kwakuwa alikuwa mtumishi wa serikali wizara ya elimu ndo nasubiri taratibu zikamilike nimhabarishe hayo ndo ninayo ni kuhadisiwa nimimi mwenyewe leo nisiku yatatu!!!But thank you kwa kututahadharisha kwani niwengi wetu tunshida za mahausegirl.:A S-danger:
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  poleni mnaopenda vya bei poa.
   
 5. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kweli hali inatisha sana siku hizi, kuna ndugu yangu mmoja alikuwa na house girl siku moja aliamua kuchoma moto nyumba ikateketea yote....Inabidi ukimpata house girl kwanza kabisa unampeleka kwenye maombi kama kuna mapepo au majini yoyote yatoke.
   
 6. k

  kawaida New Member

  #6
  Jul 23, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani wakati umefika watu kufunguka macho nakuanza kutumia akili katika suala zima la kuajiri housegirl(beki tatu)kuwa waangalifu sana lasivyo yanaweza kukututa makubwa zaidi ya huyu baba na familia yake........
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Vya bure gharama plus uswahili aargghh basi bongo yazidi tu kuwa tambarare....................
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  .....???????....!
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nimeona mwingine kule anasema ka-HG kanamfundisha matusi mtoto wake..Sasa hii ni nafasi ya kijasiriamali hii (kwa wale wene macho hawaambiwi tazama) In fwakt nipo mbioni kufungua kampuni ya kutoa huduma za uyaya na utunzaji wa nyumba. Hii itasaidia hizi kazi MUHIMU ambazo watu wanatake for granted kufanywa kitaaluma zaidi na kimikataba BILA USWAHILI.
   
 10. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mh sisi tulikuwa na kabinti kutoka Morogoro jamni achani tuu hatuna hamu nao tena
   
 11. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :ballchain:Mhh Mungu atusaidie
   
 12. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  jibu lako lanikwaza! kwani hao ousegirls ni bei poa?
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Jul 23, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli inabidi tubadilike kuhusiana na hawa Mahausigeli!
   
 14. k

  kisukari JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,766
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  Mimi nashukuru house girl wa mama ni mtu mzuri sana na yupo nae mwaka wa 10 huu,ni mtu muaminifu,hana tamaa.mama anweza akasafiri na akamuachia nyumba bila ya wasiwasi. kwa sasa amepata mchumba mwezi wa 10 harusi yake. mama hatopata tena house girl mzuri kama huyo.
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mimi hawa ma TX nilishaancha nao siku nyingiiiii...
  Lea mwanao mwenyewe, pata ndugu wa karibu akusaidia kama mama yako etc au jipe likizo isiyo na malipo ulee mwanao hata afikie miaka mitatu umpeleke play group!
  Kwanza hawa ma hausigeli huwa wanadumaza akili za watoto - wengi wao ni wajinga ( baadhi siyo wote) unategemea nini kumwacha mjinga kukulelea mwanao? Kumbuka miaka 5 ya mwanzo ndio formative years za mtoto....
  Ni mawazo yangu tu... dont shoot me!
   
 16. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  hapo ningekuwa mie nicngemuhabarisha lolote, bali ningemlipia nauli aongozane na msafara wa mcba alieniletea ningemjulisha baada ya kumaliza matatizo ya mcba....yani haya mambo yanatisha, wacha tu wanangu wabakie boarding....
   
 17. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Yani mkuu, hujui tu hii project ninavyoiwazia!..Hakika italipa sana, najipanga mwenzio!!
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Jul 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Amin..utakuwa competitor wangu.
   
 19. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  That's terrible..!
   
 20. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hivi ukiwa na daycare,si unaajiri watu kama hawa hawa??hamna mahali pako safe!...labda mwajiri uwe na uchawi-detector...LOL:bowl:
   
Loading...