1974hrs
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 741
- 536
TUJIFUNZE UPENDO WA KWELI KWA MAGUFULI NA SHEIN
Jana Raisi Magufuli na Raisi wa Zanzibar Dr Shein walimtembelea makamu wa kwanza wa raisi na katibu mkuu wa CUF Maalimu Seif Sharif Hamadi. Tukitazama katika hali ya kisiasa kwa sasa Zanzibar na mitazamo negative ya watu wengi kwamba Zanzibar hakuna amani kwamba seif na shein hawaelewani , CCM na CUF hawaelewani, hali hiyo imekuwa sio kweli baada ya Jana Shein na Seif kwa nyuso za furaha kabisa wamekutana pale Shein alipoenda kumjulia hali Seif ambaye alikuwa anaumwa.
Sisi kama raia lazima tujifunze kitu kwa hawa viingozi wetu, Zanzibar ni Moja na hakuna uadui wowote wa kisiasa wala ukabila, wala udini , wazanzibar ni wamoja na Tanzania ni Moja. Kwa hili la Jana kukutana viongozi hawa inaonesha dhahiri kuwa uchaguzi wa tar 20 March utakuwa wa amani kabisa kama alivyoandika Jana Jusa kiongozi was CUF kwamba hali ya Seif inaendelea vizuri na watashiriki uchaguzi.
Nawapongeza sana Viongozi wote wa CCM na CUF kwa moyo wa upendo na umoja mlionao, na tunawataki wazanzibar wote uchaguzi mwema na waamani, Pia tunaungana na Mh Raisi Magufuli kumuombea Maalimu Seif. Afya njema Mungu amponye kabisa ili pia aweze kushiriki uchaguzi wabkidemocrasia kupata raisi mpya waZanzibar.
TUJIFUNZE KWA HILI NA TUSIWEKE CHUKI ZA KISIASA KWENYE UHALISIA WA MAISHA TUTAKIANE HERI TUSIGOMBANE KISA UCHAGUZI.
#SISI_SOTE_NI_NDUGU