Tujifunze softwares za music/audio production

Kram Billz

Member
Dec 1, 2012
75
125
Kumekuwa na ushindani mkubwa kwa miaka ya sasa hivi katika utengenezaji wa softwares ambazo hutumika katika music production. Ilikuwa kazi sana katika miaka kadhaa ya nyuma kwa mtu aliyetaka kuwa music producer kutokana na alitakiwa kujifunza na kumiliki vifaa vingi ambavyo gharama yake ni kubwa kidogo so wengi wao waliishia kutamani tu pasipo kujifunza.

Lakini kutokana na mabadiliko ya teknolojia siku hadi siku watu wanagundua njia rahisi ambayo inaweza kumsaidia mtu kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja japokuwa anaweza kutokuwa na baadhi ya vifaa.

Softwares nyingi sana siku hizi ambazo watu huzitumia katika audio production kulingana na matakwa na uwezo wa mtu binafsi. Leo nitazungumzia baadhi ya softwares faida na hasara zake ambazo wewe kama ungependa kujifunza audio production waweza kuchagua ikufaayo.

Tunaanza na Fruity Loops (FL Studio). Faida zake ni kupatikana kwa urahisi na hukupa life time updates, rahisi kutumia, unaweza kutumia bila ya midi instruments, waweza load instruments nyingi uwezavyo,haihitaji system specifications kubwa mfano ram hata 512mb inatosha. Zipo faida nyingi ila hizo ni baadhi.

Tuje kwenye hasara haina auto saving project ambapo itakupa tabu wakati ikitokea imekorofisha kwa muda ile project yako huwezi kuikuta, inahitaji umakini wa hali ya juu wakati wa mixing na mastering wa nyimbo yako, haina time stretching nzuri kama softwares nyingine nk.

Software nyingine ni Cubase. Faida zake ni inakuwezesha kurecord multi tracks kwa muda mmoja, ina time stretching nzur ambayo inakupa option ya kuchagua jinsi utakavyo, inafanya mixing and mastering kwa ubora zaid nk. Hasara zake ni original setup yake mfano cubase 5.1 ni kubwa sana 6 GB, inahitaji system specifications kubwa, ni ngumu kutumia kwa mtumiaji wa mara kwanza, inahitaj midi instruments, pia sound card kwa ajili ya high quality sound nk.

Software nyingine ni Reason, Ableton live. Faida zake na hasara ni zile zile kama za cubase hazina tofauti sana.

Logic Pro X hii ni special kwa ajili ya Mac OS haipo kwenye Windows na hii ni moja ya hasara zake. Faida zake ni ina load instruments haraka zaidi kutokana na uwezo mkubwa wa computer aina ya Mac, mixing na mastering zinakuwa na ubora mzuri kutokana na built in plugins zake zenye ubora.

Hizo ni baadhi ya softwares za audio production ambazo unaweza kuchagua ikufaayo na kuanza kujifunza leo.

Nakaribisha michango yenu

Kwa wale ambao wanahitaji T Racks kwa ajili ya kufanyia mixing and mastering katika kazi zao nimeupload kwa ajili yenu so unaweza kudownload kupitia link hiyo hapo chini. Kama kuna matatizo yoyote katika installation process usisite kuuliza

NB::Hii ni cracked version so ni original sio demo.


IK.Multimedia.T-RackS.CS.v4.1.UNLOCKED-R2R

 

Murano

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
2,062
2,000
Thanks kwa info, eti VST plugin ipi nzuri kwa kufanya final mastering yenye kutoa quality nzuri kama sina sound card?
 

okaoni

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
1,394
2,000
Mada nzuri sana naomba iendelezwe na wadau mbalimbali , ili tupate updates za plugins mpya, sound card gani ni nzuri kwa uimbaji wa kitanzania, condenser gani affordable zinatoa sound nzuri,

Ni powermixer gani ya bei rahisi ina uwezo wa kutoa quality sound, tofauti na cubase/nuendo ni software gani zinazotumiwa na studio zinazofanya vizuri hapa bongo, je unaweza kuitumia FL studio kwenye cubase.

Ninamaanisha tofauti na zile plugins ambazo zinaingiliana kotekote je naweza kutumia vinanda vya FL kuvirekodi kwenye cubase?
 

Kram Billz

Member
Dec 1, 2012
75
125
Thanks kwa info, eti VST plugin ipi nzuri kwa kufanya final mastering yenye kutoa quality nzuri kama sina sound card?

Kuna vst nyingi ambazo zinatofautiana katika features zake ila zina kazi moja. Vst's ambazo nimeona watu wengi hupenda kuzitumia ktk kufanya final mastering ni Izotope Ozone n T racks na hii T racks unaweza kuitumia kama stand alone vst so unaweza kuanza mastering na Izotope then ukamalizia na T racks
 

Kram Billz

Member
Dec 1, 2012
75
125
okaoni, Hapa kwa mimi kama nilivyokuelewa ni unamaanisha je kuna uwezekano wa kutumia FL ndani ya cubase at the same time? Jibu ni ndio kwa kufanya maelezo yafuatayo:

FL Studio ina option ambayo inaitwa fruity rewire hii option inaweza kukuwezesha kuitumia FL kwenye software nyingine ya audio production. So unaweza ukatengeneza melody kwenye fl and ikatokea kwa cubase at the same time
 
Last edited by a moderator:

okaoni

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
1,394
2,000
Hapa kwa mimi kama nilivyokuelewa ni unamaanisha je kuna uwezekano wa kutumia FL ndani ya cubase at the same time? Jibu ni ndio kwa kufanya maelezo yafuatayo:

FL Studio ina option ambayo inaitwa fruity rewire hii option inaweza kukuwezesha kuitumia FL kwenye software nyingine ya audio production. So unaweza ukatengeneza melody kwenye fl and ikatokea kwa cubase at the same time.
Safi mtaalamu, nitajaribu nimejiuliza sana na nimejaribu nikashindwa kwani kuna wakati ninatamani niongezee percussion voices za FL kwenye souti za kinanda ili kupata ladha tofaoti sasa ilikuwa inanichengua sana. Asante kwa kuanzisha mada hii muhimu
 

Kram Billz

Member
Dec 1, 2012
75
125
Safi mtaalamu, nitajaribu nimejiuliza sana na nimejaribu nikashindwa kwani kuna wakati ninatamani niongezee percussion voices za FL kwenye souti za kinanda ili kupata ladha tofaoti sasa ilikuwa inanichengua sana. Asante kwa kuanzisha mada hii muhimu

Poa poa mkuu tutazidi kujulishana mambo mengi kuhusiana na audio production na kama una swali lingine feel free to ask
 

Murano

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
2,062
2,000
Kuna vst nyingi ambazo zinatofautiana katika features zake ila zina kazi moja. Vst's ambazo nimeona watu wengi hupenda kuzitumia ktk kufanya final mastering ni Izotope Ozone n T racks na hii T racks unaweza kuitumia kama standalone vst so unaweza kuanza mastering na Izotope then ukamalizia na T racks
Ahsante mkuu ngoja nizisearch Google
 

Kifimboplayer

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
1,493
2,000
Poa poa mkuu tutazidi kujulishana mambo mengi kuhusiana na audio production na kama una swali lingine feel free to ask

Nilishawahi soma kwenye mtandao mmoja kwamba kwa kutumia simu hizi za kisasa unaweza ukaingiza sauti (vocal) ukaitoa na kuifanyia mastering kwenye comp na ikawa bora kwenye nyimbo?
 

big-diamond

JF-Expert Member
May 23, 2009
402
500
Nilishawahi soma kwenye mtandao mmoja kwamba kwa kutumia simu hizi za kisasa unaweza ukaingiza sauti (vocal) ukaitoa na kuifanyia mastering kwenye comp na ikawa bora kwenye nyimbo?

I hope hiyo itakuwa kwenye Option za FL Mobile studio, ambayo walianza ku release ya android then iOS, japo sijawahi kutumia mobile version. Hope itakuwa na hizo features
 

Kram Billz

Member
Dec 1, 2012
75
125
Nilishawahi soma kwenye mtandao mmoja kwamba kwa kutumia simu hizi za kisasa unaweza ukaingiza sauti (vocal) ukaitoa na kuifanyia mastering kwenye comp na ikawa bora kwenye nyimbo?

Yeah inawezekana ila hii nimeona ipoa sana kwenye IOS. Kuna software inaitwa iRig hii software ili kufanya kazi vizuri inahitaji iRig mic ambayo unaweza kuconnect na simu yako au ipad na kutumia ktk vocal recording...

NB: Licha ya hizi apps za kurecord kwa smart phone quality inakuwa tofauti na ile ya studio kutokana na uwezo na upungufu wa vifaa kama sound card na kuzuia noises ambako kwa studio kuna booth inayokinga unwanted noises ili kukupa ubora katika vocals zako
 

okaoni

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
1,394
2,000
Ahsante mkuu ngoja nizisearch Google
Mkuu kwenye Google inaweza ikawa ngumu kwa sababu zinauzwa mimi nilizipata kwenye pyrate sites. Jaribu Torrentz.com au The Pyrate Bay.org . Utapata version yoyote unayoitaka ila uwe umeinstall Bitlord , Bittorrent au U Torrent
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom