DidYouKnow
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 1,229
- 1,952
Rwanda inajilinda dhidi ya Corona kwa kujaza jiji la Kigali na masinki yanayohamishika ya kuoshea mikono katika vituo vya mabasi, migahawa, mabenki na maduka.
Mpaka sasa Rwanda haina tukio la Corona, isipokuwa nchi ya jirani ya DRC
Katika kituo kikuu cha mabasi jijini Kigali, wasafiri lazima waoshe mikono kabla hawajapanda mabasi. Vifaa hivi havijanunuliwa na serikali bali na kampuni mbalimbali kama za uchukuzi.
Mabenki, Maduka, Migahawa na pia Vilabu vya pombe vyote vimewekwa masinki ya kuoshea mikono na wateja wana ari ya kuosha mikono.
Kunawa mikono hakutokuwa shida kwa Tanzania, maana nilishawahi kuona ndugu wa wagonjwa waliopo hospitali ya kanda Mbeya wakiwa kwenye mstari mrefu wakisubiri kunawa mikono bombani, baada ya kutoka kutembelea wagonjwa wodini.
Hapa ni serikali kutoa muongozo wa kampuni za magari, mabenki, maduka, maeneo ya ibada kuweka masinki ya kuoshea mikono.