Watu 101 wakiwemo wafungwa 72 waambukizwa Corona Rwanda

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Kwa mara nyingine tena Rwanda imetangaza rekodi kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya Corona, baada ya watu 101 wakiwemo wafungwa 72 wa gereza la Ngoma Mashariki mwa Rwanda, kuthibitishwa kuambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19 ndani ya saa 24 zilizopita, hii ndiyo rekodi kubwa zaidi kuwahi kutangazwa nchini humo, tangu mgonjwa wa kwanza abainike katika ardhi ya taifa hilo, taehe 14 Machi mwaka huu.

Miongoni mwa wagonjwa hao wapya, 72 ni wafungwa wa gereza la Ngoma lililopo wilayani Ngoma mashariki mwa Rwanda na inasemekana waliambukizwa baada ya kutengamana na watu walio karibu na mpaka wa Rusumo unaotenganisha Rwanda na Tanzania.

Kwa maana hiyo rekodi ya wagonjwa wa Corona nchini humo imepanda mara dufu na kufika wagonjwa 1001, huku waliopona wakiongezeka na kufika watu 443 ambao wako hospitali ni 556 vifo bado ni viwili.

Ikumbukwe huku idadi ya wagonjwa wa Corona ikizidi kuongezeka, baadhi ya mitaa iliyokutwa na maambukizi makubwa jijini Kigali katika siku za hivi karibuni, imewekwa karantini ili kuzuia kuenea Zaidi kwa virusi hivyo katika maeneo mengine ya mji mkuu wa Rwanda Kigali.

Ugonjwa huo ulipoanza kusambaa kwa kasi nchini humo, serikali ilipiga marufuku watu kutembelea wafungwa ili usienee magerezani na wengi wanahoji, imekuwaje wafungwa wakaambukizwa virusi hivyo na hali hawatembelewi? Yamkini hili likawa ni swali tata ambalo wengi wetu hatuwezi kulipatia majibu.
 
Let them bear their own responsibilities waache kusingizia kwamba maambukiiz alitokea Tanzania. Kwani kuna mtu alitoka Tz kwenda gereza la Rwanda. Ifike mahala wakubali kukabiliana na tatizo wao wenyewe bila kujaribu kumnyoshea kidole mtu. Sidhani hata diplomatically hii kitu inakibalika
 
Kwa mara nyingine tena Rwanda imetangaza rekodi kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya Corona, baada ya watu 101 wakiwemo wafungwa 72 wa gereza la Ngoma Mashariki mwa Rwanda, kuthibitishwa kuambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19 ndani ya saa 24 zilizopita, hii ndiyo rekodi kubwa zaidi kuwahi kutangazwa nchini humo, tangu mgonjwa wa kwanza abainike katika ardhi ya taifa hilo, taehe 14 Machi mwaka huu.

Miongoni mwa wagonjwa hao wapya, 72 ni wafungwa wa gereza la Ngoma lililopo wilayani Ngoma mashariki mwa Rwanda na inasemekana waliambukizwa baada ya kutengamana na watu walio karibu na mpaka wa Rusumo unaotenganisha Rwanda na Tanzania.

Kwa maana hiyo rekodi ya wagonjwa wa Corona nchini humo imepanda mara dufu na kufika wagonjwa 1001, huku waliopona wakiongezeka na kufika watu 443 ambao wako hospitali ni 556 vifo bado ni viwili.

Ikumbukwe huku idadi ya wagonjwa wa Corona ikizidi kuongezeka, baadhi ya mitaa iliyokutwa na maambukizi makubwa jijini Kigali katika siku za hivi karibuni, imewekwa karantini ili kuzuia kuenea Zaidi kwa virusi hivyo katika maeneo mengine ya mji mkuu wa Rwanda Kigali.

Ugonjwa huo ulipoanza kusambaa kwa kasi nchini humo, serikali ilipiga marufuku watu kutembelea wafungwa ili usienee magerezani na wengi wanahoji, imekuwaje wafungwa wakaambukizwa virusi hivyo na hali hawatembelewi? Yamkini hili likawa ni swali tata ambalo wengi wetu hatuwezi kulipatia majibu.
Corona ni ya kila mtu Lockdown ama Unlocked down
 
Waache kuihusisha Tanzania na maambukizi kwani gereza Hilo lipo Tanzania, basi waiseme China maana ndo chanzo cha huo ugonjwa
 
Back
Top Bottom