Tujifunze Nini Toka Tume ya Uchaguzi Kenya

Mabbyjr

Member
Aug 19, 2007
29
1
Nimesoma habari toka kwenye gazeti la Tanzania Daima kuwa Tume ya uchaguzi Kenya yakiri kuwa ililazimishwa kutangaza ushindi kwa Mh. SANA na ni kweli alifanya hivyo kama habari inavyosema hapo chini. Lakini sasa mambo yamekuwa moto bin hot kwa Mh.Kibaki baada ya huyo mwenyekiti wa Kenya Electoral Commision kukiri kuwa nguvu ya dola ilitumika kwa njia moja au nyingine kumlazimisha yeye kutangaza mshindi. Sasa utamu ni pale ambapo sasa akiri kuwa ushindi wa Mh. SANA haukuwa legitimate kulingana na sababu alizozitaja.
Swali kwa Tanzania Electoral Commission ya Bongo, tunajifunza nini hasa kutoka kwa huyu Mwenyekiti wa hiyo commission pale anaposimama kidete kuelezea umma ukweli kuwa wakubwa walicheza rafu uwanjani. Mie naamini pale kwenye ukweli lazima tupatetee bila kujali nafasi ya mtu serikalini. Mh. Prezidaa ukilamba kura bila ridhaa ya wananchi inabidi uelezwe ukweli. Sasa sijui Mh. Jaji Makame na Ndg. Kiravu mnasemaje hapo??????? Gazeti ni kama ilivyo hapo chini:-

Tume sasa yaukana ushindi wa Kibaki


na Mwandishi WetuWAKATI vurugu zinazoendelea nchini Kenya zikikaribia kufikia kiwango cha mapiganio ya kikabila, uhakika wa ushindi wa Rais Mwai Kibaki umeingia katika majaribu makubwa, baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo (ECK), Samuel Kivuitu, kusema kuwa hana uhakika iwapo Kibaki alishinda katika uchaguzi huo.
Kivuitu amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa hana uhakika na matokeo aliyoyatangaza na kuwa aliyatangaza kutokana na shinikizo na kubanwa na wanasiasa kutoka vyama vikubwa viwili vya PNU cha Kibaki na ODM cha Odinga.

Kivuitu alizidi kubainisha maajabu aliyoyafanya alipoeleza kuwa alikipeleka cheti cha ushindi wa Kibaki Ikulu baada ya baadhi ya watu kutishia kuwa watakichukua na kukipeleka, wakati jukumu hilo ni lake.

"Nilipofika Ikulu wakati napeleka cheti, nilimkuta Jaji Mkuu akiwa tayari kumuapisha rais," Kivuitu alinukuliwa na vyombo vya habari akisema.

Alikiri kuwa wakati wote wa harakati za kujumlisha matokeo yaliyokuwa yakipokewa kutoka katika vituo mbali mbali, wanasiasa na viongozi wa PNU na ODM walikuwa wakimbana kwa kumpigia simu mara kwa mara wakimtaka atangaze matokeo hayo.

Alisema kwa upande mwingine, alikuwa pia akibanwa na baadhi ya mabalozi na wanadiplomasia pamoja na Maina Kiai wa Tume ya Haki za Binadamu, wakimtaka asiyatangaze matokeo hayo, mpaka matatizo yote yaliyojitokeza yatakapopatiwa ufumbuzi.

"Nilikuwa nimefikiria kujiuzulu, lakini nilighairi kwa sababu sikutaka watu wanione mwoga," alisema muda mfupi baada ya kikao chake na makamishna 22 wa tume hiyo.

Alisema kwa hali ilivyo, mpaka sasa hana uhakika iwapo mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi huo ni Kibaki wa PNU au Raila Odinga wa ODM.

Kutokana na hali hiyo, alisema upo umuhimu wa suala hilo kufikishwa katika vyombo vya sheria, hususan mahakama na iwapo hilo litatokea, mahakama inapaswa kutoa maamuzi mapema iwapo mshindi ni Kibaki au Odinga, ili kukomesha vurugu zinazoendelea kusababisha mauaji ya mamia ya Wakenya.

Alikiri kuwa alifanya maamuzi ambayo yameiingiza nchi katika matatizo. Hata hivyo, alisema kuwa alilazimika kuyatangaza matokeo hayo kwa sababu tume yake haina mamlaka kuchunguza kasoro zilizoelezwa.

Alisema hivi sasa tume imeanza kuwasiliana na wanasheria ili washauri ni nini kifanywe ili kulimaliza tatizo lililojitokeza kisheria.

Alisema kama tume, wao pia ni watuhumiwa katika sakata lililoibuka na ingekuwa vema iwapo tume huru ingeachwa kuchunguza makosa yaliyojitokeza.

Katika kukabiliana na matatizo hayo, tume hiyo imewaalika wataalamu wa uchaguzi kutoka Afrika Kusini, ambao wanatarajiwa kuwasili nchini humo leo.

Wakati huo huo, dunia imeonyesha kushtushwa kwake na vurugu zinazoendelea nchini Kenya kutokana na kuonekana kuwa na mwelekeo wa kuingia katika hatua ya mapigano ya kikabila.

Mwendelezo wa vurugu hizo unaonyesha kuwa makabila makubwa mawili nchini humo, Waluo na Wakikuyu, yanawindana na kushambuliana.

"Sasa inaonekana kuwa haya ni mauaji ya kimbari yaliyopangwa ili kulimaliza kabila fulani, ambayo yamefadhiliwa na viongozi wa Orange Democratic Movement kabla ya uchaguzi mkuu," ilisema taarifa iliyosomwa na Waziri wa Ardhi, Kivutha Kibwana, kwa niaba ya wenzake.

Wakikuyu ni kabila kubwa kuliko yote nchini Kenya, ambalo Rais Kibaki, ambaye ushindi wake katika uchaguzi wa hivi karibuni ndio ulianzisha vurugu hizo, anatokea. Waluo ni kabila la pili kwa ukubwa, na mgombea wa upinzani anayepinga ushindi wa Kibaki, Odinga, anatokea katika kabila hilo.

Wakati huo huo, wanajeshi wamesambazwa katika maeneo kadhaa yaliyokumbwa na vurugu, wakati kukiwa na wasiwasi wa kuibuka kwa mauaji ya kikabila.

Msemaji wa serikali, Dk. Alfred Mutua, alikiri kusambazwa kwa wanajeshi lakini akasema kuwa wanajeshi hao watakuwa na jukumu la kusambaza misaada ya kiutu katika maeneo yaliyoathiriwa na vurugu.

"Hii si mara ya kwanza kufanya hivi, mara nyingi jeshi limetusaidia katika masuala kama haya na hali ya sasa imetulazimisha tulitumie tena," alisema.

Katika kile kilichoonekana kama kikwazo kwa jitihada za kimataifa kutatua mgogoro ulioibuka, Dk. Mutua alisema kuwa Kenya haipo tayari kuwaita wasuluhishi wa kimataifa kama njia ya kumaliza mgogoro uliotokana na matokeo ya uchaguzi mkuu.

"Hatujafikia hatua kama ya Somalia, hivyo hatuhitaji wasuluhishi waje nchini mwetu," alisema na kubainisha kuwa Rais Kibaki yupo tayari kwa mazungumzo ili kumaliza tofauti zilizojitokeza.

Dk. Mutua alitoa kauli hiyo wakati taarifa zikionyesha kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Ghana, John Kufuor, alipanga kuwasili nchini humo jana, kusuluhisha mgogoro ulioibuka.

Wakati huo huo, makumi ya maelfu ya Wakenya wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na vurugu hizo, ambazo zimesababisha vifo vya watu kadhaa.

Polisi jana walisema kuwa idadi ya watu waliokufa imefikia 178, wakati vyanzo vingine mbalimbali vinaeleza kuwa idadi ya vifo inazidi watu 300.

Hayo yanatokea wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Condoleezza Rice na yule wa Uingereza, David Miliband, wametoa taarifa ya pamoja wakiwataka wanasiasa nchini Kenya kukomesha vurugu zinazoendelea.

Waliwataka kufuata njia za kisheria kutatua matatizo yaliyojitokeza ili kumaliza vurugu kubwa kuwahi kutokea nchini humo tangu mapinduzi yaliyoshindwa ya mwaka 1982.

Nao maofisa uhamiaji wa Uganda walieleza kuwa mamia ya watu wa kabila la Kikuyu walikuwa wakivuka mpaka kuingia nchini humo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, naye aliungana na viongozi wengine wa kimataifa na kueleza masikitiko yake kutokana na vifo vya watu nchini humo.

Aliwataka wanasisa na viongozi wa vyama kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa matatizo yaliyojitokeza nchini humo ili kukomesha mauaji hayo.

Wakati huo huo, wizara ya elimu nchini Kenya ililazimika kusogeza mbele tarehe ya kufunguliwa kwa shule za sekondari hadi Januari 14 na 15.

Naye Rais Kibaki, aliwaalika wabunge wote wateule na kuwataka kufika Ikulu jana jioni kukutana naye.

Naye waziri wa sheria, aliwataka wanasiasa wa kambi ya upinzani ambao hawakubaliani na matokeo ya uchaguzi huo kwenda mahakamani, kwani ndiyo yenye mamlaka ya kutoa maamuzi kuhusu mabishano ya matokeo ya uchaguzi wa rais.

 
Huyu Ndie Wa Kukata Shingo Kabisa Ndugu Zanguni Na Ndie Anaeifanya Kenya Hapa Ilipo:hapa Ni Kujisafisha Tu Ili Watu Wasimpunguze Kwenye Ulimwengu Au Familia Yake ,ila Amini Nakwambia Kama Wakenya Ndio Hawa Wanochinjana Leo Hii Huyo Bado Tumpe Muda ,,,,alikuwa Ana Uwezo Wa Kukataa Kutaja Matokeo,,whyyyy Kwannini???????????mbona Zanzibar Walichelewesha Mpaka Kifimbo Akaamua Kuingia Front Mchezo Ukaisha,,

2)ananchanganya Zaidi Ati Alilazimishwa Kwamba Apeleke Cheti Cha Ushindi Ikulu Akakuta Jamaa Wako Full Mkoba Kuapishwa Duuh Akabaki Hoi,,kama Nilivyosema If U Cant Them Join Them Ikabidi Jamaa Awe Kwenye System,,huyu Ni Nyoka Kabisa Kabisa Sio Wa Kumwacha ,,hatuitaji Was***i Kama Hawa Hata Siku Moja Kwenye Africa,,najua Wengine Watamsifia Ila Anajihami Kwa Ujinga Wake,,kama Alikuwa Na Uwezo Wa Kusema Hajui Nani Mshindi Kwanini Hakuwa Na Uwezo Wa Kukataa Matokeo..

Hili Lenyewe Tu Kukiri Hajui Matokeo Nani Alishinda Msumari Tosha Kwa Maisha Yake Na Familia Tena Wa Kiunoni Asubiri Utakavyomchoma..kwenu Wanablogu
 
Mimi nimejifunza mambo mawili;
1. Mwenyekiti wa Tume ni mnafiki. Nasema hivi kwasababu najiuliza kwanini ameona sawa kusema hivyo sasana sio kabla hajatangaza ili wale observers na jumuiya ya kimataifa umlinde. Angeweza hata kumpigia mmoja wa mabalozi simu amuambie kuwa analazimishwa na hataki akimbilie huko ubalozini apate hifadhi na watu wajue kuwa kulikuwa na huo uchafu unaandaliwa; and that would have been the end of the election exercise na haya yanayotokea yasingetokea; waliomlazimisha wangekuwa wanajibu tuhuma sasa na pengine uchaguzi ungekuwa unarudiwa au kura zingekuwa zinahesabiwa chini ya uangalizi mkali..He had all the alternatives and yet he chose the worst; sasa dhamiri inamsuta anatafuta sympathy

2. Hizi tume za chaguzi zisiachwe peke yao at any point katika zoezi zima; wafungiwe wote mahali pamoja, tume, observors kutoka vyama na kwingineko; no phone calls; no emergencies at home etc hadi zoezi liishe; afterall haichukui masiku mengi kukamilisha; let them be lawfully confined in one place and under strict surveilance from start to end.

3. Uteuzi wa tume nayo iwe issue ya vyama vyote; sio Raisi achague mtu wake halafu tutegemee asimtii
 
Makubwa haya,toka nimezaliwa sijaona wakumfananisha na huyu jamaa.
Duuh! mimi hoi
Hivi hii iko kwene chombo gani cha habari?kama hata jari kinipa jina la mwandishi wa habari hii
 
..kwamba african institution are not matured and stable.

..we have a long way into building trust for these institutions.

..wengi wetu hatuwezi kusimamia misingi ya kazi zetu.

..wengi wetu hatuna busara,hekima na ujasiri wa kutosha kuwaokoa wenzetu dhidi ya hali yeyote mbaya inayoweza kuwatokea.

..na kwa haya tutaendelea kunyonywa,kutawaliwa na kuonewa na walio nje ya afrika!kwakuwa hatuwezi kujiongoza!
 
Sioni sababu ya kuwa na wasi wasi TANZANIA haswa ukizingatia the so called UPINZANI Tanzania.

Wako Kimya kuhusu sakata la MAHUJAJI

WAKO KIMYA KUHUSU breach OF OUR NATIONAL SECURITY

Wako kimya kuhusu serkali ya ZNZ kutumia wanajeshi kwenye shughuli za kidini

wako kimya kuhusu balozi za nje kukusanya DNA za watanzania Dar

wako kimya kuhusu MAUAJI huko Kenya

wako kimya kuhusu WATANZANIA WALIOTELEKEZWA huko Kenya


sasa what makes you think in your righful mind kuwa TUME YA UCHAGUZI TANZANI Itawapa CCM?

with upinzani like CUF & CHADEMA....CCM does not need kuiba kura wala kupendelewa na Tume ya Uchaguzi

 
Cha kujifunza hapa ni kwamba tume hizi haziki huru na wala hazistahili kauminiwa kabisa na wapiga kura na vyama vya upinzani.

Inabidi tumpongeze huyu Mwenyekiti wa ECK Bw Samuel Kivuitu kwa kuwa mkweli, vinginevyo angeweza kujinyamazia kimya wakati watu wanaendelea kuchinjana.
 
..yeye ndiye aliye-facilitate kuanza kwa fujo na maangamizi,kwa uoga wake na unafiki wake!

Kunguru muoga hukimbiza bawa lake. Unapowekwa kwenye shinikizo la kutangaza matokeo ambayo wewe kama mwenyekiti bado hujayathibitisha ni lazima uogope kwamba uhai wako uko mashakani. Siungi mkono alichokifanya lakini uhai una raha zake.
 
Cha kujifunza hapo, usiamini mtu yeyote aliyeteuliwa na rais kwamba atatenda haki pale ambapo maslahi ya rais yako hatarini kuanguka.

Kwani tume ya uchaguzi lazima iteuliwe na rais? Ifike mahali hii kazi iwe ya
kujaza application na screening kufanywa na indepent body.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom