Tujifunze kuwapongeza watenda haki na wafuata shEria kama Salum Rashid Hamduni

TOFU

JF-Expert Member
Aug 26, 2012
573
196
Mungu ni mwema wana jamvi .
Nawasalim

Kwa unyenyekevu mkubwa kabisa napenda kuwasilisha uzi huu mahususi nikimlenga moja kwa moja Man of the match POLISI SALUM RASHID HAMDUNI.

Kwa mara kwanza kabisa nialianza kumfahamu polisi huyu pindi alpokuwa RPC Mkoani Kilimanjaro.

Alishuhulika na mambo meengi kwa jamii na pia akashuhulika na changamoto mbali mbali zinazowakabili ndani ya jeshi la polisi ...!!!

Chaajabu alipoingia offic ya RPC pale Moshi alikutana na ma files lukuki ya Askari wasikuwa na maadili kazini kama kutokuja kazini bila taarifa na wengine walevi mda wa kazi na ukosefu wa maadili yoote ndani ya jeshi la polisi.

Ofisi yake ilisheheni ma file ya walikuwa na barua za kuonywa kulingana na matendo yao maovu yanayojirudia rudia.
Sasa huyu Bwana Hamduni hakusita kuwashuhulikia bila hiyana wale wote waliokuwa na ukosefu wa maadili na wengine kutolewa kabisa ndani ya jeshi la polisi baada ya kuonywa mara kwa mara na kupelekea file lake kufika offic ya RPC kwaajili ya hatua zaidi.
Jambo hili lilishangaza sana baadhi ya askari kwa uwamuzi wake mgumu wakutoweza kuvumilia mambo yasiyokuwa na msingi ndani ya Jeshi letu.!

Wengi walisema Askari huyu labda ni pandikizi ndani ya jeshi la polisi kwa ujasiri na maamuzi yake magumu na kujiamini maana walikuwa hawajazoea.

Tusisahau sakata la uwizi wa mataruma ya reli pale wilayani Hai ..
Ni nadra sana tena kwa utawala wa mwenda zake ukaona RPC anasimama tofauti kabisa na matakwa ya DC ..!!
Alichunguza jambo lile na moja kwa moja akakanusha mchana kweupe na kuaibisha utawala dhalimu wa kijana yule DC.
Ni jambo la ajabu sana ..
Kwani angeweza kukaa kimya au kubambikizia watu kesi ili Sebaya asionekane kasema uongo na kuamua kuungana na kijana yule DC.!!

Lakini Afande yule alisimamia maadili ya kazi yake na akatoka na kukanusha tuhuma zile ...!!

MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU KAMISHNA WA POLISI SALUM RASHID HAMDUNI AKABIDHIWA OFISI RASMI


Hakika Mama Samia na amiri wetu wa Jeshi letu mkuu hakukosea kumchagua bwana huyu kwenye taasisi nyeti na yakutenda haki kama takukuru.

Hoja yangu ya msingi apa ni sisi kama wanajamvi tujifunze kuwapongeza watu hawa adimu kabisa kwenye taifa letu ..!!

Kwani tukitoa 500/= kwa kila kichwa kwa watu 100,000 hiyo ni M50 tayari ..!!
Tumpatie kama zawadi imsaidie kwenye mambo yake na familia yake ..!!

Wengi wetu tumefundishwa kushukuru pindi mtu anapokufanyia jambo jema ...!!
Sioni ubaya kumshukuru bwana huyu ili pia tuonueshe jamii yetu kuwa tunawatambua na kuwaheshimu wale wote waliopewa jukumu la kusimaia sheria na wamejitoa na kusimamia kwa haki kama bwana huyu Afande afanyavyo.


Napendekeza mmoja wetu apewe jukumu lakuchangusha mia tano zetu na tumpongeze japo kwa kidogo lakini kikubwa analolifanya bwana huyu Afande ..!!
Maana jeshi letu limekuwa likilalamikiwa kwa mambo mengi lakini akitokea mmoja kama huyu basi tumshukuru na kumpongeza mchana kweupe bila aibu.!!


Asanteni wakuu
Japo najua sio muandishi mzuri lakini matumaini yangu nimeeleweka na mtanisamehe kwa ilo.
Naomba kuwasilisha kwenu wakubwa zangu
Na Mungu awabariki sana
255712215520_status_b8ad0fc38a66492c9ef232f09e8664ee.jpg
 
Niwajubu wake..
jaribu kuandika vizuri maana sioni sababu ya kuwaharaka kupost uzi
 
Niwajubu wake..
jaribu kuandika vizuri maana sioni sababu ya kuwaharaka kupost uzi
Wengi wamepewa wajibu huo lakini hawajatekeleza majukumu yao ipasavyo badala yake wametizama jukumu lile kama fursa kwao na maisha yao ..!!

Japo bado naheshimu sana mawazo yako Mkuu

Niombe radhi kwa mara nyingine tena ..
Si muandishi mzuri wa makala
Apo nimeji switch hadi mwisho mkuu wangu.
 
Back
Top Bottom