Tujifunze Kutoka Libya

..umeeleza vizuri sana kwamba ukivunja HAKI unahatarisha AMANI.

..amani ya Libya ilitoweka baada ya Gadaffi kuanza kukanyaga HAKI za wenzake.
Kwamba kumshika wakili ndiyo ghafla pakazuka vikundi vyenye silaha na NATO wakaleta jeshi?
 
Mkuu kwa upepo unavyoelekea wananchi wanataka kuingia msituni hawataki mazungumzo na maandamano yameshindikana kwa kua wanapigwa risasi.. Hii ni hatari ikitokea tuu vijana wakipata training kidogo ya silaha hali itakua mbaya sana ngoja tuone..

maandamano nyie key body ni watu selfish
 
Mkuu kwa upepo unavyoelekea wananchi wanataka kuingia msituni hawataki mazungumzo na maandamano yameshindikana kwa kua wanapigwa risasi.. Hii ni hatari ikitokea tuu vijana
 
Wananchi jua kwamba nasi ikifikia hatua hiyo ya machafuko,wazungu wataingilia kati ,si kwakuwa wanatupenda ila kwa ajili ya Kuja kuvuna rasilimali za Tanzania
Ikiwa wazungu wanavuna rasilimali zetu si sawa kabisa. Nauliza inakuaje MTZ mwenzako anavuna na wewe hufaidiki vile unavyostahili?

Ndio maana mkaambiwa kabla ya kuhubiri AMANI hakikisheni mnawatendea mema na HAKI, hii Amani itakuja tu.
 
Yaani mpigane wenyewe halafu mje mlaumu wanao waachanisha muache kupigana. Marekani wana mpaka military base South Korea lakini South Korea haijaanguka. Sanasana ndo inazidi kuendelea. Wana military base Kenya pia. Kenya haijaanguka. Hizo nchi za hovyo ulizotaja ni za hovyo hata bila Wazungu kuingilia. Think critically mkuu, acha kuwa mjinga kama mleta mada.
 
Hivi kwa nini humwambii mama abdul kutenda haki? Umekazana tu kutuhuburia amani fake.
 
Soma alama za nyakati na kuzielewa.
Unaweka picha za jeshi wakati tatizo ni sisi kutotatua changamoto za vijana.
Kaa chini, fikiri na kuziona dynamics za nyakati.
 

Usisome mambo juu juu Ila USA hana msaada wowote kwa Africa
 
Hahaha hatuhitaji maji au umeme wa bure, haki na usalama wetu kwanza, na Libya naturally is very rich state, yeyote mwenye akili kidogo anayeelewa haki angeweza kuifanya nchi tajiri na nzuri sana , Gaddafi was good lakini aliifanya Libya kama mali yake binafsi na familia yake, acha watwangane tuu ili waheshimiane na kuheshimu haki ya kila mtu
 
Hawa vijana safari hii wakiingia road kupinga serikali wakishikwa wawekwe nondo za moto makalioni.
Amani gharama yake kubwa kuliko haki.
Haki unaweza kuijenga kwa siku moja but amani hujengwa kwa miaka mingi
Mnafundishwa na kushikilia upumbavu.

Utaipata wapi amani ya kulazimisha watu waikubali kwa shinikizo la mitutu ya bunduki?
 
Usisome mambo juu juu Ila USA hana msaada wowote kwa Africa
Kama hana msaada wowote ndiyo nasi tusijitoe kutafuta haki zetu wenyewe?
Mara unatutisha CCM; sijui majeshi yote ni CCM! Kwa hiyo unataka tufanye nini, tukubali tu Samia na Genge lake wafanye wanachotaka wenyewe?

Hatutegemei, na wala hatutaki hao Marekani waje hapa. Kazi ya ukombozi wa nchi yetu ni yetu wenyewe. Hao wazungu wakitaka kusaidia kuzima mitutu ya bunduki mnayotumia kuwaua waTanzania wakati wanatafuta ukombozi wao, kwa nini tusikubali msaada huo. Kwa nini hili linakutisha sana wewe na wenzako?
 
Issue sio SSH mkuu ukijua tatizo la nchi ni MFUMO wa CCM

Hata wewe ukiwa Rais kwa tiketi ya CCM hakuna utakaachobadilisha

Sisi wananchi wazalendo hatutaki vijana wetu waandamane ili wauliwe Ila tunataka mazungumzo yafanyike.

Njia ya kuandamana haina matokeo chanya
 
Wewe unang'ang'ana na CCM. wakati mimi nakueleza kuwa hakuna CCM; kuna kundi la waovu, Samia akiwa miongoni mwao. Hakuna cha mfumo wala nini; ni kundi la majambazi walioteka taifa zima na kufanya uovu wao wakitumia dola.

Hata kama utaiita hali hiyo kuwa ni "mfumo"; sasa unataka waTanzania wabweteke tu kwa vile ni mfumo?
Watu wafanye "mazungumzo" na mfumo ili mfumo huo ndio uamue kuwahurumia waTanzania wanaonyimwa haki zao?
Mawazo yenu haya yatakuwa yana kasoro kubwa sana.

Kwa nini hutaki watafute njia za kujitoa kwenye hiyo hali ya umateka; huku ukitetea hali hiyo izidi kuimarika!

Hii inaingia akilini? Unayo maslahi gani na huo mfumo wewe?

Wewe hukuwahi kusikia uwepo wa "mazungumzo ya maridhiano"; na wala hujawahi kusikia waTanzania wakimsihi Samia awe na subira ili pawepo na marekebisho ya sheria za uchaguzi? Wewe na wenzako mnataka mazungumzo na Genge lilelile ambalo limekwisha onyesha wazi kabisa nia yake ni nini juu ya taifa hili!
Hicho wanachotafuta hao Genge ndicho mnachokuja humu JF kukipigania.

Halafu mnajivisha "uzalendo"!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…