Tujifunze kutoka kwenye hii video ya mwanajeshi wa Iraq miaka ya 2000 mwanzoni

Tujifunze kutoka kwenye hii video ya mwanajeshi wa Iraq miaka ya 2000 mwanzoni

Mdusi94

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2017
Posts
4,477
Reaction score
4,224
Kwenye video hii anaonekana mwanajeshi akituma salam za mwisho kwa familia yake baada ya uwanja wa mpambano kuwa wa moto , mpambano uliohusisha vikosi vya serikali dhidi ya makundi binafsi ya kujihami , huyu mwanajeshi aliamua kuaga familia yake baada ya kuwa wamezingirwa na vikundi binafsi vya kujihami.

Tujiulize ilikuwaje wakafikia huku ?
Kwenye utawala wa Sadam , kulikuwa na ubabe mwingi sana dhidi ya raia , ubabe ambao wapo waliouunga mkono (WANUFAIKA ) na wapo walikuwa wahanga ambao walikuwa wanaupiga vita ya kukemea bila mafanikio , kwa mgawanyiko huu ilihitajika miongon mwa vikosi vya jeshi vichukue hatua mapema kumtoa Sadam ili kulinda umoja wa Iraq na kuepusha na mabalaa yalikuja kutokea baadae.

Sadam alitumia dini ya uislam kama kichaka cha kujikinga na wakosoaji wake kutoka nje ya Iraq pia Sadam alitumia dhehebu lake la usuni pale alipopingwa na wa Iraq wenyew.

Hali hii ilidumu ila mwisho wa siku alianguka miaka ya 2000 mwanzon ila alikuwa kaacha nchi imepasuka vibaya mno na ngumu kuja kuungana tena.

Mpasuko huu ulipelekea kuundwa kwa vikundi ambavyo viliendeleza vita na wahanga wakubwa walikuwa ni wanajeshi wa Iraq ambao ndo walikuwa na wajibu wa kuyamaliza haya mapema ila waliona njia sahihi ni kuua wakosoaj wakiamin wataisha na hali itarejea huko mbeleni kumbe ilikuja kuwa tofaut , sabab upinzan ulizid hasa kwa machungu ya watu wao waliopotezwa na waliungana na kila aliyekuwa adui wa jeshi la Iraq wakiitumia kama fursa kulipiza kisasi .

Hii video imenifunza kuwa kila kosa lina malipo mbeleni , jitahid kutopuuzia mambo , simama kwenye ukwel na haki maana kila kitu kina malipo mbeleni pia usiiogope HATARI NDOGO maana baadae inaeza zaa JANGAA KUBWA .

JE WEWE UMEJIFUNZA NINI KWENY HUU MKASA ...

 
Kabla ya tujue,We hii story umeitoa wapi mkuu....?
 
Back
Top Bottom