Tujifunze Kitu wana JamiiForums


friendfx

friendfx

Senior Member
Joined
Oct 16, 2017
Messages
190
Likes
135
Points
60
friendfx

friendfx

Senior Member
Joined Oct 16, 2017
190 135 60
Walimuuliza mtu mmoja mwenye umri mkubwa: Umejifunza nini kutokana na umri wako uliopita?

Akajibu:
Nimejifunza kwamba dunia ni karadha na deni

Nimejifunza kwamba aliyedhulumiwa lazima atashinda japo baada ya muda

Nimejifunza kwamba mshale wa usiku haukosei

Nimejifunza kwamba maisha yanaweza kumalizika wakati wowote huku tukiwa tumeghafilika

Nimejifunza kwamba maneno matamu na uso wenye bashasha na ukarimu ni rasilimali za tabia

Nimejifunza kwamba tajiri kuliko matajiri wote duniani ni yule ambaye anamiliki afya na amani

Nimejifunza kwamba anayepanda kitunguu hatavuna mawaridi

Nimejifunza kwamba umri unamalizika lakini shughuli hazimaliziki

Nimejifunza kwamba anayetaka watu wamsikilize basi na yeye awasikilize

Nimejifunza kwamba kusafiri na watu ni zana bora ya kugundua tabia zao

Nimejifunza kwamba ambaye anaongea sana (anasema mimi, mimi) huyo ni mtupu ndani yake

Nimejifunza kwamba ambaye madini yake ni dhahabu atabaki dhahabu, na ambaye madini yake ni chuma atabadilika na kuchuja

Nimejifunza kwamba wote waliozikwa makaburini walikuwa na mashughuli na maagano na kwenye nia zao walikuwa na mengi ambayo hawakuyatimiza

Nimejifunza kwamba sisi tunatandika kitanda na tunabaridisha chumba ili tuneemeke na mauti madogo, lakini je tumeratibu matendo yetu na kubaridisha makaburi yetu kwa kufanya twaa ili tuneemeke na mauti makubwa?

Anasema mmoja wa watu wema; Nimestaajabishwa na watu wanajihadhari na baadhi ya vyakula kwa kuogopa maradhi, lakini hawajihadhari na dhambi kwa kuogopa moto

Nimeyasoma, yakanivutia na nikapenda niyatume kwa nafsi njema
 
Nalendwa

Nalendwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2016
Messages
7,235
Likes
12,363
Points
280
Nalendwa

Nalendwa

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2016
7,235 12,363 280
 

Forum statistics

Threads 1,236,284
Members 475,050
Posts 29,252,931