Peter Stephano 809
Senior Member
- Feb 29, 2020
- 120
- 162
Siku za hivi karibuni ameibuka mtu anaevalia mavazi ya kujificha "Spiderman" ambae anazunguka mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam akikata mauno na kuuza vitu mbalimbali ikiwemo matunda na vitafunwa.
Mtu huyu aliyepewa jina la Spiderman wa bongo amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na aina ya ubunifu wake na kuchezacheza kwenye mabasi, sokoni na mtaani.
Watu wengi wanaonekana kuvutiwa na kununua bidhaa zake huku wengine wakipenda sana burudani ya kucheza.
Lakini kuna kundi la watu ambao hawapendi kumuona kwa sababu mbalimbali walizonazo.
Mtu mmoja anaejulikana kwa jina la Shaban Miyangi, akitoa maoni yake kupitia gazetu la Mwananchi anasema "hii nchi uhuru umezidi kuna watu wanautumia vibaya huyu jamaa anatudhalilisha sana watanzania na haswa wanaume"
Kadhalika msanii wa filamu Tanzania Wema Sepetu anasema anakerwa na Spiderman wa bongo pasipo kutoa sababu za kero hiyo.
Rodgers Rodriguez Charles anasema duniani ukitaka ufanikiwe haupaswi kutaka kumfurahisha kila mtu bali fanya kile unachoona kina faida na huvunji sheria za nchi.
Tuachane na mitazamo ya watu mbalimbali tuje kwenye uhalisia wa maisha, tujiulize Spiderman wa bongo anafanya yale kwa kusudi gani?
Jibu tutakalo lipata ni kwa kumtazama anazunguka akifanya nini je kinampa faida?
Jibu ni kwamba anazunguka kucheza na kuuza bidhaa hasa matunda na vitafunwa.
Jibu hili linatosha kusema Spiderman wa bongo yupo kifaida ametumia ubunifu kuchuma pesa mtaani ili familia yake ile nyumbani.
Tujikumbushe kidogo miaka ya hivi karibuni hapa nchini kuna Watu walipata umaarufu kwa kuvujisha picha za utupu hii leo wanapiga pesa na kupewa madili ya ubalozi wa mipango ya serikali.
Kuna watu walisifika kwa ulevi wakapata fursa ya kusafiri na timu za taifa maeneo mbalimbali nje ya nchi na kulipwa posho nono.
Kwa kumbukumbu hii bado tumtukane Spiderman wa bongo na kumuona hafai kabisa?
Hapana tutakuwa tunakosea anaihangaikia familia yake bila kuvunja Sheria yoyote hapa nchini.
Kama nilivyosema mwanzo kuwa hapa nchini watu wa ovyo kuliko Spiderman wa bongo wamepewa fursa nyingi tena za kulipwa mamilioni na serikali.
Nakumbuka kuna siku aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alinukuliwa akisema "tatizo moja tulilo nalo nchini ni kuwapa nafasi watu wa ovyo ovyo".
Spiderman wa bongo hajavuka mipaka ya kuwa mtu wa ovyo Kama wale aliowasema Makonda bali anapambana na maisha magumu ya sasa hususani mfumuko wa bei.
Badala ya kumuona kero tujifunze kutoka kwake namna ya kupambana na ugumu wa maisha na kusaidia familia zetu.
Peter Mwaihola