Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Shebbydo

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
1,176
Reaction score
1,939
Habari Wanajukwaa

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima bukheri.

Kuna tangazo moja la redio la malaria huwa linanivutia sana, mtoto anamuuliza baba yake kuhusu ndege inavyoweza kupaa angani. Mzee kutokuwa na elimu hata kidogo tu ya aviation anajitetea kwa kumwambia mwanaye hayo ni maarifa ya juu sana.

Ndege nini! Ndege ni chombo ambacho kinasafiri angani kwa kutumia kani mnyanyuo (Lift force) inayozalishwa hasa kwenye mabawa kutokana na uhusiano wa mwendo kati ya hewa na ndege yenyewe.

Ndege ina sehemu kuu tano, yaani; Injini (Power plant), bodi la ndege (fuselage), mabawa (wings), Mkia (Empennage) na Mfumo wa matairi (Landing gear).

1: POWER PLANT; hii ni sehemu ya ndege inayohusika na uzalishaji wa kani msukumo (Thrust force). Hii ndiyo kani (force) inayoisogeza ndege kutoka point A kwenda point B ikiwa angani.

2:FUSELAGE; Hii ni sehemu ya ndege ambapo sehemu zingine zimeunganishwa kwayo. Pia nyiyo sehemu ambapo abiria, wafanyakazi wa ndege na mizigo hukaa.

3:MABAWA; Hii ni sehemu ya ndege yenye umbo la "aerofoil" ambayo inahusika na kuzalisha kani mnyanyuo (LIFT FORCE). Hii ndiyo kani inayoifanya ndege ielee angani.
Aerofoil ni umbo ambalo huzalisha kani-mnyanyuo kutoka na tofauti ya mgandamizo wa hewa wa chini na juu ya umbo hili. Hii ni kutokana na utofauti wa ukubwa wa eneo la chini na juu. Eneo la juu huwa kubwa zaidi ya lile la chini, hivyo kusababisha hewa ya juu kusafiri kwa kasi zaidi ya ile inayopita chini ili kuweza kukutana pamoja katika muda ule ule (LAW OF CONTINUITY). Kasi ya hewa ikiongezeka basi mgandamizo wake hupungua (PRESSURE)

Hiki ndicho kinachotokea kwenye mabawa ya ndege. Mgandamizo wa hewa chini unakuwa mkubwa kuliko juu, hivyo kani-mnyanyuo kuzalishwa. Ikumbukwe kwambo umbo zima la ndege lipo katika aerofoil. Hivyo nalo huchangia kani-mnyanyuo japo kwa kiasi kidogo ikilinganishwa na ile inayozalishwa kwenye mabawa.

4:EMPENNAGE; Hii ni sehemu ya ndege kwayo kunapatikana maumbo yanayoipa ndege "U-stable" katika mihimili yake na vifaa vinavyoifanya ndege iweze kutembea (move) katika mihimili yake. (Tutaangalia huko mbele mihimili ya ndege ni nini). Katika sehemu ndipo kuna "horizontal na vertical stabilizers".

5:LANDIND GEAR; Huu ni mfumo mzima wa matairi ambao unaohusika na kuisaidia ndege kutembea juu ya njia ya kurukia (RUNWAY) wakati wa kuruka na kutua, vilevile wakati wa kwenda sehemu ya matengenezo (HANGAR)

Kwa leo tuishie hapo, sehemu itakayofuata tutaangalia kan (FORCES)i zilizopo kwenye ndege na mihimili ya ndege (MOTION ALONG AIRCRAFT AXES). Mwenye swali lolote kuhusu ndege unakaribishwa.


==========


Baada ya kuangalia sehemu muhimu za ndege, nimeona ni busara tuangalie kifaa kimojawapo ambacho ni muhimu katika uchunguzi wa ajali. Ni baada ya kuwa nimeona kimetajwa sana kwenye comment kwa lake ambalo ni maarufu japo kwa lugha ya kindege kinafahamika kwa jina jingine. Hiki ni kifaa cha kuhifadhi taarifa mbalimbali za ndege iwapo safarini. Kifaa hiki kinaitwa Flight Data Recorder (FDR) maarufu kwa jina la " Black Box".

Histtoria yake:
Kizazi cha kwanza cha kifaa hiki inaanzia miaka ya 1950 ndipo kilianza kutumika kufuatia uhitaji wa wana anga kuwa na kifaa ambacho kinaweza kutoa angalau abc za ajali husika, kutokana na nature ya ajali za ndege mara nyingi hupoteza watu wote wanaokuwepo kwenye ndege. Hivyo kukosa hata kujua chanzo cha ajali nini! Mpaka mwaka 1965 kifaa kilikuwa kikihifadhiwa kwenye kisanduku chenye rangi nyeusi, ndiyo sababu ya kujulikana kama "Black box". Mwaka 1965 shirika la kusimamia mambo ya anga la dunia (International Civil Aviation Organization) liliamuru kifaa hiki kiwekwe kwenye kisanduku cha rangi ya njano angavu au rangi ya orange angavu (bright yellow or bright orange) ili kurahisisha uonekanaji wake wakati wa kukitafuta pindi inapotokea ajali.
Katika kizazi hiki cha kwanza ilikuwa ni tape ambayo ipo katika mfumo kama ule wa redio ya kanda.

Kizazi cha pili cha kifaa hiki kilianza miaka ya 1970. Hapa tape iliboreshwa kidogo ikawa na urefu wa futi 300-500, inaweza kurekodi data kwa takribani masaa 25 na ikiwa ni magnetic tape. Vifaa vya kizazi hiki bado vinatambuliwa na ICAO, hivyo bado vinaweza kutumika kwenye ndege.

Pamoja na kuboreshwa kwa uwezo wa kuweza kurekodi data kwa muda mrefu, bado FDR hii haikuweza kuhimili data zinazotoka kwenye sensor mbalimbali kwenye ndege kwa wakati mmoja. Hivyo miaka ya 1980 kuligunduliwa kifaa kingine ambacho kinasaidia kupokea data kutoka kwenye sensor mbalimbali. Pia wakati huo FDR ilikuwa imeboreshwa na kurekodi data katika mfumo wa digital. Kifaa hicho ni Flight Data Acquisition Unit (FDAU).

Hadi sasa teknolojia ya kifaa hiki ni kizazi cha tatu ambayo ni Solid State Technology, yaani maana ni kwamba kifaa hiki utunzaji wake wa kumbukumbu upo katika solid memory storage. Hii ni kama unavyoona hizi memory cards na flash disks. Hiyo ndiyo solid state memory storage.
Uwezo wake sasa hivi ni mkubwa sana, kinaweza kupokea signal kutoka kwenye sensor mbalimbali takribani 88 kwa wakati mmoja.

JINSI KINAVYOFANYA KAZI:
Flight Data Recorder ikisaidiwa na Flight Data Acquisition Unit ambayo inafanya kazi kama interface (kiunganish) hupokea na kuhifadhi taarifa mbalimbali kutoka kwenye sensor za vifaa vya ndege. Taarifa hizi ni kama;
Uelekeo wa ndege, speed ya ndege, mwinuko wa ndege, power ya injini na position ya vifaa vinavyotembea vya ndege vinavyosaidia ndege kupata kani-mnyanyuo (lift force). Endapo ndege itapata ajali basi taarifa hizi zilizohifadhiwa zitasaidia kujua chanzo cha ajali ni nini. Kama ni makosa ya rubani, matatizo ya mifumo ya ndege ama ni sababu kutoka nje, kama vile upepo mkali na vinginevyo.

Pamoja na kifaa hiki pia kuna kifaa kingine ambacho pia husaidia uchunguzi wa ajali. Kifaa hiki hurekodi sauti za mazingira ya cckpit. Kifaa hiki kinaitwa Cockpit Voice Recorder (CVR). Vifaa hivi huweza kuwa vimehifadhiwa katika kisanduku kimoja ama tofauti. Mbali na uchunguzi wa ajali, pia FDR husaidia kujua hasa injini imefanya kazi kwa muda gani. Kifaa hiki kila mwaka lazima kikaguliwe na mamlaka ya anga.

SIFA ZA KIPEKEE ZA FLIGHT DATA RECORDER;
Kifaa hiki kimehifadhiwa kwenye " enclosure" ambayo ina sifa hizi:
1: Kinaweza kuhimili moto mkubwa wenye jotoridi 1100°C, kikiwa 100% kwenye moto huo, kikahimili kwa dakika 30. Endapo enclosure itakuwa na kiwango cha ED 56 Test protocol (Hiki ni kiwango cha juu sana cha material kuhimili joto), basi kinaweza kudumu katikati ya moto huo kwa saa 1 yaani dakika 60.
Kwenye moto wa kiwango cha chini 260°C (Oven test), kinahimili moto huo kwa masaa 10
2: Athari za kuanguka kwa kishindo; Kinaweza kuhimili impact shock ya kiwango cha 3400g(g ni kipimo cha shock) yaani kiwango hicho ni kikubwa sana cha shock. Kifaa hiki kipo strong.
3:Kifaa hiki kina life span ya kukaa ndani ya maji ya bahari kwa siku 30 bila matatizo.
Ili kurahisisha upatikanaji wake, kifaa hiki hakitafutwi kwa macho tu, hivi sasa kimeboreshwa, kikiwa popote hata majini kinatoa frequency ambazo zinaweza kupokelewa na receiver.

Hiyo ndiyo Flight Data Recorder Al-maarufu Black Box.
 
Hivi mafuta ya ndege yanatengenezwa na nini?
Asante kwa swali lako mkuu
Mafuta ya ndege hayatokani na vitu tofauti na haya mafuta tunayoyajua. Ni yale yale isipokuwa yanaongezwa chemical fulani tu ili kuongeza sifa fulani kama vile corrosion inhibitors ambazo zinasaidia matank yasipate kutu. Chemical nyingine ni kuongeza ignition point ya mafuta yaani yawahi kulipuka kwenye process za injini. Kwa mfano Injini za ndege aina ya gas turbine engine zinatumia mafuta ya taa, yakiisha ongezwa vitu jina linabadilika linakuwa Jet A. Nazo zimegawanyika. Kwa hiyo mafuta ya ndege nayo ni hydrocarbon fuel.

Sent from my itel it1508 using JamiiForums mobile app
 
Ok. Kinachosababisha ndege kukata kona ikiwa hewani ni nini?
Hili swali lako umewahi kuuliza kwa sababu nilipanga kuelezea yote haya katika "Motion along aircraft axis" anyways kwa kuwa umewahi kuuliza ngoja niieleze hapa hapa japo ni maelezo marefu kidogo.

Ndege ina mihimili mitatu, nayo ni;

1:LONGITUDINAL AXIS; huu ni mhimili (axis) ambao umelala kuanzia sehemu ya mbele ya ndege (NOSE) kuelekea nyuma kwenye mkia. Yaani unaigawa ndege katika sehemu mbili kwa ulalo. Mwendo (MOTION ALONG LONGITUDINAL AXIS) unaotokea hapa unaitwa "ROLL". Yaani ndege inaweza kuinamia upande wa kulia ama kushoto. Kinachosababisha mwendo huu kutokea ni matokeo ya kazi inayofanywa na " structure" ambazo zimeunganishwa kwenye mabawa zinaitwa AILERONS. Zipo mbili, moja bawa la kushoto jingine bawa la kulia. Rubani akitaka ndege iinamie kulia basi huinamisha aileron ya kushoto na ile ya kulia huinuka juu zaidi. Hivyo kutokana na nguvu za hewa (upepo) huisukuma ile iliyoinuka na kusababisha upande huo kuinama kuhusiana na huo mhimili(LONGITUDINAL AXIS)

2:LATERAL AXIS; Huu ni mhimili ambao unapita katikati ya mabawa. Kuanzia mwanzo wa bawa moja hadi jingine. Mwendo kuhusiana na mhimili huu (MOTION ALONG LATERAL AXIS) unaitwa "PITCH". Yaani ni ile hali ya ndege kuinua ama kushusha uso wake. Kuna pitch up and pitch down. Kwa mfano, wakati wa kuruka uso wa ndege huwa juu, hii ni pitch up na wakati wa kutua uso huelekea chini(PITCH DOWN). Motion hii ni matokeo ya " CONTROL SURFACE" iliyopo kwenye Empennage, ambayo inaitwa "ELEVATOR". Rubani akitaka ku-pitch up basi huifanya elevator ipande juu. Kutokana na nguvu au kani za upepo (AIR FORCES), nguvu hizi huisukuma kuelekea chini, hivyo basi ndege huku mkiani huinama na mbele huinuka (pitch up) na hivyo hivyo kinyume chake.

3:NORMAL AXIS; Mhimili huu unaweza pia kuuita vertical axis. Huu ni mhimili ambao upo wima na ndege. Yaani kutoka chini kwenda juu ya ndege. Mwendo uliopo hapa {MOTION ALONG VERTICAL AXIS) unaitwa " YAW". Yaw ni mwendo wa ndege kukata kushoto au kulia kuhusiana na huu mhimili (vertical axis). Mwendo huu ni matokeo ya "CONTROL SURFACE" inaitwa "RUDDER". Usichanganye na Radar, hivi ni vitu viwili tofauti kabisa. Rudder ipo kwenye mkia wa ndege. Rubani akitaka kukata kona kushoto basi huifanya rudder iegemee kushoto. Nguvu za upepo huisukuma kuelekea kulia. Hivyo mkia huelekea kulia na uso wa ndege huelekea kushoto na kinyume chake.
Hivyo kwa swali lako. Kinachoifanya ndege kukata kona angani ni hiyo RUDDER lakini pia kuna control surfaces nyingine ambazo zinafanya kazi mbili. Inaweza kuwa roll na yaw. Hivyo tutaongelea siku tukiangalia CONTROL SURFACES.
 
kipi hufanya baadhi ya ndege kurudi reverse?
Asante mkuu kwa swali.
Hili swali lilishawahi kuulizwa humu lakini si mbaya tuliangalia tena vizuri.

Katika kuongelea sehemu kuu za ndege nilianza na POWER PLANT. Power planr (yaani injine na mifumo yake) ndiyo hutoa kani-mjongeo (Thrust force)
Zipo aina mbalimbali za power plant. Siku moja tutaongelea kwa undani zaidi. Lakini leo niegemee kwenye swali lako zaidi. Kuna ndege zinaweza kujongea kwa kutumia propeller lakini zikiwa na aina ya injini inayoitwa gas turbine engine. Kwa mfano ATR na Bombardier Q series, yaani inaweza kuwa Q300 au Q400. Hizi ndizo ndege zinaweza kurudi nyuma(reverse). Kivipi? Fuatilia hapa chini.

Propeller huzungushwa na injini ili kuzalisha thrust force kwa kusukuma hewa (AIR MASS) nyuma. Hivyo kutokana na sheria ya "nature" iliyogunduliwa na Sir Isaac Newton. Inasema "To every action there is equal and opposite reaction. Maana yake ni nini! Propeller ikisukuma hewa nyuma reaction inasukuma kwenda mbele. Hivyo ndege inakwenda mbele. Sasa aina ya ndege nilizozitaja hapo juu zinaweza kubadili " BLADE ANGLE" ya propeller. Badala ya kusukuma hewa nyuma, propeller inasukuma hewa mbele hivyo reaction inaisukuma ndege nyuma. Kwa hiyo ndege inaweza kurudi numa (reverse).
 
Helcopta nayo ina mfumo kama hizi aeropalane?
 
swali: je turbulence inaweza kuangusha ndege iwapo angani?
Jibu ni ndiyo inaweza kuangusha ndege. Kwanza turbulence ni nini. Turbulence inatokea pale ambapo strealine air flow imepotea hivyo kunakuwa na loss of LOSS OF LIFT. Ukipoteza lift unategemea nini rafiki yangu, vinginevyo urudishe lift iliyoanza kupotea. Sasa inategemea na sababu ya hiyo turbulence. Kwa mfano ndege ndogo ikiifuata ndege kubwa kwa karibu zaidi, ndege ndogo inaweza kuanguka kwa ajilivya kupoteza streamline flow kutokana na vortices za ndege kubwa.
 
Ni materials gani yanaunda bodi ya ndege
Umeliweka swali lako katika ujumla sana hivyo nashindwa kujua ni structure gani unamaanisha. Kwa maana kwamba ni unamaanisha fuselage structural members au skin. Lakini kwa ujumla sehemu kubwa ya ndege ni Aluminum alloys. Japo kuna ndege nyingine sasa hivi wanatengeneza ni composite materials tupu.
 
Helcopta nayo ina mfumo kama hizi aeropalane?
Hapana, japo zote zinafanya kazi katika kanuni moja. Helicopter yenyewe lift force (Kani-mnyanyuo) inazalishwa na rotor blade (lile panga la juu). Haina mabawa. Helicopter inaweza kujongea pande zote, yaani mbele, nyuma, kushoto na kulia. Rubani anacheza na tilt angle tu. Kitu ambacho airplane haiwezi
 
Back
Top Bottom