Tujifunze Hapa.

malisoka

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
1,860
2,637
Ndugu wana JF.

Kifo na mazingira yake ya Bondia Thomasi mashali ni funzo kuwakumbusha watawala na serikali kwa ujumla jinsi ya kuwaenzi na kuwathani wanamichezo wetu.

Tusiweke misingi ya kuwaenzi na kuwarisisha vijana wetu katika siasa eti kwa sababu baba au mama alikuwa mkubwa wa chama au serikali. Mtindo huu unaweza kuuona wazi pale unapoona majina yanajirudiarudia katika Uongozi wa nchi na siasa yake.

Mimi sijaona na kama mtu ana ushahidi wa Mwanamichezo yeyote kwa juhudi za serikali wapo hapo walipo.

Nimeshuhudia wanamichezo mashuhuri na wenye majina makubwa wakizalilika mitaani na hata wakati mwingine wanakata tamaa ya maisha na kuwa Ombaomba na walevi wa kutubwa. Hii inasikitisha sana.

Nchi zilizoendelea kama Ulaya ma marekani Mwanamichezo akishachukua medali na kuitangaza nchi serikali inamuangalia na kumtunza ili awarisishe vizazi vijavyo. ndiyo maana wengi wa makocha na walimu wa michezo katika nchi hizi ni wanamichezo hodari wa zamani wakiendeleza vipawa vyao.

Je hapa Tanzania Viongozi wetu wa michezo wametokea wapi Je wana historia ya michezo? Je Mawaziri wetu wa Michezo, Wakurugenzi ni wale waliokuwa wanamichezo wa zamani katika ngazi ya Kimataifa?

Inasikitisha sana kuona jitu halina hata historia ya michezo lakini yupo kwa ajili ya maslahi yake binafsi.

Ningekuwa Mimi Rais wa Nchi hii ningeanza na wizara inayoshughurikia michezo je wanajua kitu wanachokiongoza, wamewahi kuwa wanamichezo katika Kimataifa au la. Kama Jibu sio Wanamichezo na hawana historia ya Michezo Ni KUWATUMBUA na kuweka wale watu ambao wanajua nini wanafanya na lengo (goal) ni nini.

Badala yake tunawaacha waliokuwa Tunu ya Taifa wakiwa walevi, Ombaomba wasiokuwa na matumaini. Tusiwafanye Wanamichezo wakaona kuwa wanamichezo ni kupoteza Muda.

Nina ushaidi wa Mwanamichezo aliyekuwa Tunu ya Taifa lakini sasa anashona viatu na kupiga dawa.

Tuwaenzi wanamichezo wetu kwa kuwapa nafasi ya kuwaendeleza wanamichezo wetu chipukizi na tuwape nafasi za masomo na kuwapa uongozi wa michezo.

Na sio wakishafariki tunajipanga msururu kutoa rambirambi na kuwapa masifa ambayo hayawasidii wakati huo.

Tuweke utaratibu wa kuwatambua/ kuwaendeleza na kudhamini muda wao walio poteza wakiwakilsha nchi yetu.


Asante.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom