Mkuu umegonga sehemu moja ambayo huwa inanisumbua sana ninapowasiliana na watu mbalimbali kwetu. Mwaka juzi tulikuwa tumegundua fedha fulani za USAID ambazo zingeweza kufanya kazi nzuri sana kwenye chuo fulani huko Tanzania; sheria ya congress inataka pesa zote za USAID zitumike 3rd world. Tulipowasiliana na chuo kile wakatujibu utumbo wa ajabu kweli bila hata kujua kuwa wanaongea na nani; ilikuwa ni aibu sana kwangu niliyeweka contact ile ila kwa bahati kwa bahati nzuri tulikuwa tumweka sample kubwa ya vyuo, hivyo tukawasliliana na chuo kingine kama hicho hicho huko Kenya ambao walitupa ushirikiano wa hali ya juu sana na mwishowe wakachukua zile pesa. Ingawa hazikuwa pesa nyingi sana ($160,000), lakini ilikuwa ni bora kuliko kutopata kitu. Faida yake kwetu sisi ilikuwa ni kuwa bosi wangu aliweza kwenda Kenya free; nilikuwa ninataka aende Tanzania.
Elimu ya mawasaliano ni ndogo sana kwa watu wetu. Watu wengi ni dhaifu sana wa kujenga hoja na kujibizana na wengine. Urithi tulioachiwa na Nyerere katika mawasliano haupo kabisa siku hizi.
Nadhani vyuo karibu vyote vya marekani vinafundisha soma la "Public Speaking" kama mojawapo ya general education courses ambazo ni lazima mwanafunzi alipitie kabla hajapata digrii yake bila kujali fani yake. Course hii pamoja na mambo mengine huwa inasisitiza logic kiasi kuwa matu unapoonegea na watu lazima mawazo yako yawe yamepangiliwa kwa utaratibu fulani ambao unamfanya msikilzaji apende kukusikiliza na kufahamu unaloongea bila kukosea. Course hii ya public speaking inafanana kidogo na course ya zamani iliyokuwa inatolewa pale UDSM ikijulikana kama Communication Skills ambayo ilikuwa ni lazima kila mwanafunzi aipitie bila kujali yuko kitivo gani. Kosa lilitokea baadaye ni kuwa wanafunzi wengi walikuwa wanaingia chuoni huku kiingereza kinawagonga sana na kusababisha waalimu wengi wa CSU wawe wanatumia muda mwingi kufundisha grammar na sentence structures zaidi ya logical flow of ideas.
Tukumbuke kuwa, kuwa na mawazo mazuri bila kujua namna ya kuyapitisha mawazo hayo kwa watu wengine ni sawa na kutokuwa na mawazo kabisa.