Tujadiliane juu ya ugonjwa unaokusumbua na namna ulivyopambana kuukabili mpaka sasa

Pole sana!
Jifunze hekima itakusaidia katika maisha yako.Naamini kuna siku utakuja na shida ambayo huko hosp utakuwa umeshindwa kuitatua na nitakusaidia.Kuna wengi walikosa hekima kama wewe pia.
Yaani unisaidie kipi hasa. Mimi naamini sayansi tu. Wadanganye mabwege wasiojua nini maana ya kuwa duniani.
 
Yaani unisaidie kipi hasa. Mimi naamini sayansi tu. Wadanganye mabwege wasiojua nini maana ya kuwa duniani.
Mkuu mm pia naamini sayansi tatizo tafiti nyingi bado hazina suluhisho la kisayansi.mfano ukianza tumia sindano ya insulin kisayansi hakuna tiba.ila nakuapia kwenye dawa za asili unapona.
Mtu kama huyu hajasema njoo inbox kaamua kusaidia unakuja mvunja moyo haifai mkuu
 
Habari ya leo!

Niko hapa kukusaidia wewe mwenye ugonjwa sugu. Kama una ugonjwa wowote ambao umehangaika nao kwa muda mrefu na umepambana sana kutafuta tiba mbalimbali na bado hujafanikiwa, tafadhali andika hapa tujadiliane kuhusu namna unavyoweza kupata ufumbuzi.

Nina utaalamu na uzoefu mkubwa wa kutibu magonjwa mbalimbali, hususani yale ya mtindo wa maisha ya kila siku kwa kutumia mimea tiba. Ninaomba tujadiliane hapa juu ya ugonjwa unaokusumbua na namna ulivyopambana kuukabili mpaka sasa.
GERD
 
Vidonda vya tumbo inategemeana na kisababishi:Vingine ni kuzidi kwa asidi tumboni inayosababisha kukwangua kuta za tumbo na kusababisha vidonda vyenye maumivu makali,lakini pia inaweza kuwa ni mdudu(bakteria) anayesababisha madonda ya tumbo(H.pyrol)
Fanya mambo haya kwa sasa
1.Jizuie kutumia vyakula vyote vinavyoweza kuongeza asidi nyingi tumboni wakati wa mmeng'enyo wa chakula
2.Jizuie na msongo wa mawazo unaoweza kusababisha uzalishwaji mwingi wa nyongo na hivyo kuchochea ongezeko la asidi tumboni.
3.Pendelea kunywa maziwa fresh kila siku asubuhi mchana na jioni kuanzia sasa.
4.Tafuta mimea ile ya mashona nguo chemsha vizuri na utumie kunywa asubuhi mchana na jioni glass
5. Mwisho tafuta unga wa mizizi ya mjafari ulioandaliwa vizuri kabisa unakuwa unatumia kijiko cha chai katika maji moto asubuhi mchana na jioni.

Mungu akupe wepesi!
Hayo mashona nguo unachemsha mizizi, matawi au majani?
 
Tupe ya nguvu za kiume wanaume wa dar chips zimetuharibu na vitambi
Ukosefu wa nguvu za kiume ni matokeo ya mambo mengi kwenye mfumo wa mwili.Tunapotibu tatizo hili lazima kujua chanzo hasa ili liweze kutibika vizuri.Mfano magonjwa kama presha,kisukari,tezi dume huathiri moja kwa moja mfumo wa nguvu za kiume.Kuna vitu kama lehemu kwenye damu,mzunguko hafifu wa damu pamoja na mishipa ya damu kusinyaa huleta changamoto ya nguvu za kiume.Magonjwa sugu ya zinaa pamoja na chango ikiwemo ngiri ni baadhi ya vitu vinavyoweza kusababisha ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume.Kwa hiyo ili uweze kujitibu vyema ni lazima kufahamu kwanza chanzo cha tatizo ndipo utapata suluhisho lenye ufanisi.
 
Back
Top Bottom