Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Kama Bunge litapitisha mswaada wa kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa miwili badala ya mifuko mingi iliyopo sasa na baadae Raisi kutia saini,,unadhani nini zitakuwa faida na hasara za mabadiliko haya?
Mimi binafsi naona kutakuwa na hasara zifuatazo:
1.Kupungua wa ushinda na kusababisha huduma ziwe duni.
2.Kuongezaka kwa urasimu na kuwa chanzo cha kero kwa wafanyakazi/wastaafu.
3.Waendeshaji wa mifuko hii watapunguza ubunifu kutokana na kukosekana kwa ushindani na hivyo kupunguza uwekezaji wa kibiashara wa mifuko hii.
4.Kupunguza/kufuta ajira zitakano na uwepo wa mifuko hii kwa baadhi ya waajiriwa wa mifuko hii
5.Kuondoa umuhimu wa uwepo wa taasisi ya kudhibiti mifuko ya hifadhi ya jamii(SSRA) na hivyo kutishia ajira za waajiriwa wa taasisi hii.
6.Wafanyakazi wanakatwa viwango tofauti kulingana na mishahara yao ila sidhani kama kwenye kulipa mafao tofauti hii itazingatiwa sana.
7.Formulae ya kukukokotoa mafao ikibadilishwa kuna watakaoathirika kwa mafao yao kupungua ingawa kuna watakaofaidika.
Unaweza kuongeza ingawa mengi tutayajua baada ya sheria ya kuunda na kusimamia mifuko hii itakapotungwa na kupitishwa pamoja na kanuni zake.
Muswaada husika utakuwa ni kipomo tosha cha uwezo wa wabunge wetu katika kujadili maswala nyeti na yenye maslahi kwa watanzani na Taifa kwa ujumla.