Tujadili, Tangazo la biashara la Coca cola "onja msisimko"

Tujadili, Tangazo la biashara la Coca cola "onja msisimko"

Wadau habarini ya Jumapili!!

Nimeona Leo tujadili kuhusu hili Tangazo la coca cola la onja msisimko.

Kimsingi nimefurahishwa sana na ubunifu uliotumika katika Tangazo hili. Ambalo linaonyesha jinsi vijana wa familia moja ambavyo kaka mkubwa alivyokuwa akimtesa mdogo wake, ambapo katika utoto huwa ni kawaida mkubwa kumnyanyasa mdogo wake kwa ubabe, ambapo kimsingi huwa ni michezo ya utani.

Kwenye tangazo hili, linaonyesha jinsi, kaka anavyomsumbua mdogo wake kwa ufupi wa kimo, pale anapotaka kuchukua earphone ambazo zipo juu ya kabati na mdogo mtu kwa ufupi wake hawezi kufika, Hivyo kaka mtu anaamua kuzihamisha na kuziweka juu zaidi ili dogo ahangaike, pia kaka mtu anamkanyaga miguu mdogo wake wakati wa kula ili kumsulubu tu, na mwisho kaka mtu anakuja kumsaidia mdogo wake pale anaponyanyaswa na watu wengine kwa kumchukulia chupa yake ya Coke!! Dogo haamini wema aliofanyiwa na kaka yake.

My take:
Tangazo hili linanikumbusha jinsi kaka yangu alivyokuwa akinifanyia utemi, kisa yeye ni mkubwa!! Lakini ilipokuwa inatokea nipo shuleni watu wananinyanyasa kaka alikuwa akija kunisaidia ili kuninusuru na kipigo.

Hongera Coca cola kwa ubunifu huu.
Karibuni kwa mjadala wadau.
sijapenda pale alipoisukuma chupa ya soda ,wote tunaijua coca ingeingemwingia puani dogo yangekua majanga tu. Imeonesha ukatili fulani mwishoni. Bro jipu.
 
Back
Top Bottom