Tujadili: Mid Life crisis

Tujadili: Mid Life crisis

Kaunga

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Posts
12,529
Reaction score
13,502
Wapendwa, baadhi yetu tumeshafikia huko,, wengine tunakaribia na wengine huenda baado sana. Lakini ni vizuri tufahamu kuhusu huyu mdudu ambaye wenzetu wanamuita 'mid-life crisis'. Hii ni hali ambayo watu wazima huanza kufikiria kuhusu kifo, nini hawajafanikisha (kufanya) na muda gani wa maisha uliobaki. Kipindi hiki kinasemekana huanzia kati ya miaka 37 hadi 50 hivi, ingawa wengine wanasema kinaweza kuanzia miaka 35.

Sasa kuna tabia zinazoambatana na kipindi hiki ambazo kwa namna moja au nyingine huathiri mahusiano ya watu hasa pale tunaposhindwa kutambua kuwa mwenzi wetu yuko katika kipindi gani.

Baadhi ya tabia zinazoashiria MID LIFE CRISES kwa Wanaume ni pamoja na:-
  • Kuwa bored na kazi unayoifanya na ulikuwa unaipenda, unakuwa na hamu ya kujaribu kitu kingine; inaweza kuwa unaona haikulipi kwakuwa unataka kuhakikisha unakamilisha malengo yako mengi kabla hujafa, lakini pia hata kama ulikuwa successful basi itakuwa haikupi hamasa iliyokuwa unaipata mwanzoni.
  • Kufikiria kuwa na mahusiano mengine, kwa wale ambao walikuwa say waaminifu muda huo ndipo anapowazia kuwa na kanyumba ndogo na mara nyingi huchukua vibinti vidogo zaidi ili kujihakikishia kuwa bado yumo yumo
  • Kutumia pesa sana, kipindi hiki mwanaume kwa kujua kwamba mwisho unakaribia; basi anaamua ku 'live life to the fullest' 'kwanini kujibania bwana maisha yenyewe mafupi haya'. Anaweza nunua gari ambalo ni most expensive; take vacation na kidada n.k
  • Unaweza usiamini, hata mwanaume anakuwa obssesed na jinsi anaonekana (looks), new hair cut, anatumia muda wa kutosha kwenye mirror. (BTW nilikuwa nagombea na X wangu time kwenye dressing table)
  • Mabadiliko hata kwenye sex life, na hasa akipata nyumba ndogo ndipo humuoni kabisa mume.
  • Anaamua kuishi kwenye past zaidi, anahamia kwenye mtaa wa memory; anakumbuka marafiki zake wa zamani na kuanza kuwatafuta, anamfikiria sweetheart wake wa zamani na kuanza kufikiria kwamba ingekuwaje kama angemuoa yule na vitu kama hivyo.
  • Kubwa lingine ni depression

Tabia zinazoashiria MIDLIFE CRISES kwa Wanawake ni pamoja na:
  • Depression na kujitenga, hana furaha na kujihisi yuko tupu na amepotea
  • Kuwa bored na ndoa na maisha kwa ujumla
  • Anakuwa detached emotionally hafurahii tena yale yote waliyokuwa wakiyafanya na mumewe
  • Anaweza sema anampenda mumewe lakini hahisi mapenzi
  • Kutokujua unachotaka maishani (kuwa mke au) unahisi kama unataka ku run away
  • Ukimuuliza anasema 'l am going thru something' na anataka ku-take a break
  • Anataka kuwa mwenyewe na afanye maamuzi yake mwenyewe
  • Anaanza kuangalia weight na shape yake, safari za gym zinaongezeka
  • Ana pay attention kwa looks zaidi na hata nguo anazo nunua zinakuwa za kitoto zaidi
  • Anavaa kimitego tego na anaflirt a lot
  • Hasira na kuudhika kirahisi
  • Anatoka out na vijana wadogo zaidi (hata kama ni wadada)
  • Anaweza awe na affair ofisini na vijana wadogo

Hii umeisahau " WANAANZA KUHUDHURIA NYUMBA ZA IBADA KWA BIDII ON BOTH SIDES"
 
Bora umeleta hii topik

Wanawake hawana hii kitu? Na je inahusiana vijitabia au dalili za menopause kwa wanawake?
 
Niliona lipost litakuwa refu sana ndio maana nimetenganisha!
 
Mid life crisis is waking up in bed with a woman whose name you hardly remember, wondering how you got home after heavy drinking at the club. Sigh of relief, sighting used condoms on the floor. Oh God never ever again ,yet knowing too well you wont keep the promise.
 
Yaani, nadhani mie ndio inaishia

Mawazo ya ukifa watoto itakuwaje? Ndugu itakuwaje? Wosia unaeleweka? Uzikwe wapi?

Watoto umewawekea akiba za kutosha?

Anyway wanasema the best njia ya kupambana nayo ni kuikubali hiyo hali.
 
IM TOO YOUNG FOR THIS!!!!!!!!! Ngoja nirudi kwenye MADA YA ZOMBIII!!!!!! (Najua na mimi nitazeeka ila for now CUT ME SOME SLACK!!!!!!!)

Mchaga hajafikisha 35?
It can be triggered unajua, mf. Loss of your loved ones can make you start thinking of what are doing in the world. Ila shosti enjoy your youth si unaona tunavyojitahidi kuurudisha kwa ma make up na vitop! LOL
 
Mid life crisis is waking up in bed with a woman whose name you hardly remember, wondering how you got home after heavy drinking at the club. Sigh of relief, sighting used condoms on the floor. Oh God never ever again ,yet knowing too well you wont keep the promise.

I love the humor in your definition. LOL
 
Mchaga hajafikisha 35?
It can be triggered unajua, mf. Loss of your loved ones can make you start thinking of what are doing in the world. Ila shosti enjoy your youth si unaona tunavyojitahidi kuurudisha kwa ma make up na vitop! LOL

Mchaga bado sanaaaa! Naye dogo tuuuu. Anyway kuna siku NAWAZAGA UJUE MWISHO WANGU UTAKUAJE?
 
Wapendwa, baadhi yetu tumeshafikia huko,, wengine tunakaribia na wengine huenda baado sana. Lakini ni vizuri tufahamu kuhusu huyu mdudu ambaye wenzetu wanamuita 'mid-life crisis'. Hii ni hali ambayo watu wazima huanza kufikiria kuhusu kifo, nini hawajafanikisha (kufanya) na muda gani wa maisha uliobaki. Kipindi hiki kinasemekana huanzia kati ya miaka 37 hadi 50 hivi, ingawa wengine wanasema kinaweza kuanzia miaka 35.

Sasa kuna tabia zinazoambatana na kipindi hiki ambazo kwa namna moja au nyingine huathiri mahusiano ya watu hasa pale tunaposhindwa kutambua kuwa mwenzi wetu yuko katika kipindi gani.

Baadhi ya tabia zinazoashiria MID LIFE CRISES kwa Wanaume ni pamoja na:-
  • Kuwa bored na kazi unayoifanya na ulikuwa unaipenda, unakuwa na hamu ya kujaribu kitu kingine; inaweza kuwa unaona haikulipi kwakuwa unataka kuhakikisha unakamilisha malengo yako mengi kabla hujafa, lakini pia hata kama ulikuwa successful basi itakuwa haikupi hamasa iliyokuwa unaipata mwanzoni.
  • Kufikiria kuwa na mahusiano mengine, kwa wale ambao walikuwa say waaminifu muda huo ndipo anapowazia kuwa na kanyumba ndogo na mara nyingi huchukua vibinti vidogo zaidi ili kujihakikishia kuwa bado yumo yumo
  • Kutumia pesa sana, kipindi hiki mwanaume kwa kujua kwamba mwisho unakaribia; basi anaamua ku 'live life to the fullest' 'kwanini kujibania bwana maisha yenyewe mafupi haya'. Anaweza nunua gari ambalo ni most expensive; take vacation na kidada n.k
  • Unaweza usiamini, hata mwanaume anakuwa obssesed na jinsi anaonekana (looks), new hair cut, anatumia muda wa kutosha kwenye mirror. (BTW nilikuwa nagombea na X wangu time kwenye dressing table)
  • Mabadiliko hata kwenye sex life, na hasa akipata nyumba ndogo ndipo humuoni kabisa mume.
  • Anaamua kuishi kwenye past zaidi, anahamia kwenye mtaa wa memory; anakumbuka marafiki zake wa zamani na kuanza kuwatafuta, anamfikiria sweetheart wake wa zamani na kuanza kufikiria kwamba ingekuwaje kama angemuoa yule na vitu kama hivyo.
  • Kubwa lingine ni depression

Tabia zinazoashiria MIDLIFE CRISES kwa Wanawake ni pamoja na:
  • Depression na kujitenga, hana furaha na kujihisi yuko tupu na amepotea
  • Kuwa bored na ndoa na maisha kwa ujumla
  • Anakuwa detached emotionally hafurahii tena yale yote waliyokuwa wakiyafanya na mumewe
  • Anaweza sema anampenda mumewe lakini hahisi mapenzi
  • Kutokujua unachotaka maishani (kuwa mke au) unahisi kama unataka ku run away
  • Ukimuuliza anasema 'l am going thru something' na anataka ku-take a break
  • Anataka kuwa mwenyewe na afanye maamuzi yake mwenyewe
  • Anaanza kuangalia weight na shape yake, safari za gym zinaongezeka
  • Ana pay attention kwa looks zaidi na hata nguo anazo nunua zinakuwa za kitoto zaidi
  • Anavaa kimitego tego na anaflirt a lot
  • Hasira na kuudhika kirahisi
  • Anatoka out na vijana wadogo zaidi (hata kama ni wadada)
  • Anaweza awe na affair ofisini na vijana wadogo

Hii umeisahau " WANAANZA KUHUDHURIA NYUMBA ZA IBADA KWA BIDII ON BOTH SIDES"

Umetulia unapo leta kwa mada humu kana kua na akili! Mchana mwema
 
Mid life crisis is waking up in bed with a woman whose name you hardly remember, wondering how you got home after heavy drinking at the club. Sigh of relief, sighting used condoms on the floor. Oh God never ever again ,yet knowing too well you wont keep the promise.

maisha matamu lakini mafupi...! By Fundi Konde
 
hehehhehhe
umenikumbusha jirani yetu aisee
Huyu baba kumbe alikua anapambana na mid life crisis!?
At the age of 50+ alianza kuvaa vijikaptura vifupiii, akanunua MG sports car kibandawazi.Gari ilikua inakimbai hiyo!!
Mradi alikua anaonekana kichekesho.Mwisho wake ulikua mbaya sana maana kamdudu kalimtembelea katika harakati za kurukaruka na vibinti vidogo kama vijukuu vyake.R.I.P Jirani
 
Back
Top Bottom