Tujadili hili janga kuokoa Walimu Nchini

Tujadili hili janga kuokoa Walimu Nchini

Akili Pesa

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2014
Posts
617
Reaction score
854
Soma na Utafakari:

Ndugu zangu nilivyosikia kwa mara ya kwnza wiki iliyopita kuwa walimu wote wakatwe tsh.10,000/= ktk mishahara yao nchi nzima nilidhani ni jambo tu lililovumishwa katika mitandao ya kijamii yetu hizi lakin kumbe serikali hii ya kidhalimu imedhamiria kumuadabisha mtu wa hali ya chini na kuzidi kudidimiza.

Ndugu zangu haiingii akilini kwa watu wazima tena wachumi na viongozi wenye kumjua mwalimu ni mfanyakazi mwenye kulipwa mshahara wa chini sana kuamua kumuambia mwalimu eti akatwe mshahara wake kiduchu kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara mashuleni!

Naomba kujua vitu viwili vitatu hivi;

1. Ilani ya ccm(2010-2015) imetamka hivyo kuwa maabara za shule zitajengwa kwa kuchangiwa na mwalimu mwenyew?

2. Kama haikutamka hivyo serikali ya ccm inaongoza nchi kwa kutumia ilani ya chama gani?

3. Walimu hawa wao ni wazalendo kiasi gani mpaka kubeba mzigo huo huku wawekezaji wakisamehewa kodi katika mikataba yao ya uwekezaji?

4. Kwa tamko hili unadhani Mheshimiwa Rais amepata washauri wazuri kweli?

5. Kodi ya kila mwezi anayokatwa mwalimu inapelekwa wapi?

Nahis huu ni mfumo mpya wa maendeleo kuwa kila mfanyakazi kuchangia maendeleo ya sekta yake mfano pengine tutasikia madaktari na manesi wakikatwa mishahara kuchangia madawa na mengineyo ilihali kodi anakatwa kama raia mwngne.

Nionavyo mimi, Hii ni pesa inayokusanywa pengine kwa ajili ya uchaguzi wa mwakani 2015. Walimu tuamke kupinga udhalimu huu sio haki hata kidogo. Tumuezi baba wa Taifa (Mwalimu by professional) mwaka huu 14/10/2014 kwa kupinga hadharani bila kificho huku ni zaidi ya kudhalilishana jamani.
 
mi stoi ng'ooo
labda km nimefoji vyeti ila km vyangu
waende zao
 
Juzi chadema walipopanga maandamano ya kupinga katiba haramu tuliwacheka na kuwabeza chichiem wakafanikiwa kupitisha katiba yao baada ya hapo watawala wameota mapembe na bado ngoja katiba ipite matatunyoa nywele kwa kuwa sisi wananchi ni mambulula koko si walimu si mwananchi wa kawaida. Na bado.
 
Waswahili walisema, "Ukiona mwenzako ananyolewa, wewe anza kutia maji". Kama waalimu wameanza kukatwa mishahara yao, basi watumishi wengine wa Umma na Serikali wajiandae kupitiwa na wembe ule ule. Kweli CCM ni kiboko.
 
Nyie walimu ndio mnaisadia CCM kuiba kura na mkatwe mpaka muone rangi zote.

hujitambui. unadhani walimu wote ni CCM?
Halafu mwanao au nduguyo akifeli unaema walimu hawafundishi
tulia, tafakari. katika nchi yoyote ile, sekta moja inapoyumba, nchi nzima huangamia.
wanaongaamia ni pamoja wewe unaejisikia raha kubonyeza buttons kuandika mawazo mufilisi kushadadia upuuzi huu.
 
mi stoi ng'ooo
labda km nimefoji vyeti ila km vyangu
waende zao

hakatwi mtu hapa
tukishindwa kuzuia janga hili, nitaingia benki yoyote. nakopa hela kibao halafu naendelea na mambo mengine. ualimu itakuwa mwisho.
 
SOMA NA UTAFAKARI: Ndugu zangu nilivyosikia kwa mara ya kwnza wiki iliyopita kuwa WALIMU WOTE WAKATWE TSh.10,000/= ktk mishahara yao nchi nzima nilidhani ni jambo tu lililovumishwa ktk "Social Network" zetu hizi lakin kumbe serkali hii ya kidhalimu imedhamiria kumuadabisha mtu wa Hali ya chini na kuzidi kudidimiza.. Ndugu zangu haiingii AKILINI kwa watu wazima tena wachumi na viongozi wenye kumjua mwalimu ni mfanyakazi mwenye kulipwa mshahara wa chini sana kuamua kumuambia MWALIMU ETI AKATWE MSHAHARA WAKE KIDUCHU KWA AJILI YA KUSAIDIA UJENZI WA MAABARA MASHULENI.!! Naomba kujua vitu viwili vitatu hivi. 1. Ilani ya CCM(2010-2015) imetamka hivyo kuwa maabara za shule zitajengwa kwa kuchangiwa na mwalimu mwenyew?? 2. Kama haikutamka hivyo serkali ya CCM inaongoza nchi kwa kutumia ilani ya chama gani? 3. Walimu hawa wao ni wazalendo kiasi gani mpaka kubeba mzigo huo huku WAWEKEZAJI WAKISAMEHEWA KODI KTK MIKATABA YAO YA UWEKEZAJI?? 4. Kwa tamko hili unadhani mh.RAIS amepata WASHAURI WAZURI Kweli? 5. Kodi ya kila mwezi anayokatwa mwalimu inapelekwa wap?. Nahis huu ni mfumo mpya wa maendeleo kuwa kila mfanyakazi kuchangia maendeleo ya sekta yake mfano pengine tutasikia MADAKTARI NA MANESI wakikatwa mishahara kuchangia madawa na mengineyo ilihali Kodi anakatwa kama RAIA mwngne. Nionavyo mim hii ni pesa inayokusanywa pengine kwa ajili ya uchaguzi wa mwakani 2015. WALIMU TUAMKE KUPINGA UDHALIMU HUU SIO HAKI HATA KIDOGO. TUMUEZI BABA WA TAIFA(MWALIMU BY PROFESSIONAL) MWAKA HUU 14/10/2014 KWA KUPINGA HADHARANI BILA KIFICHO HUKU NI ZAIDI YA KUDHALILISHANA JAMANI..!!

Na ni vema tukatafakari zaidi ya mara moja hii kauli ya Mwigulu eti anadhibiti watumishi wanaolipwa mishahara hewa kwa hiyo mishahara yote ya Watumishi italipiwa kupitia hazina, kwanza kabisa tangu utaratibu huu uanze hakuna Salary Sleep zilizopelekwa halmashauri ili watumishi wajue uhalisia wa mishahara yao kwa hiyo Mwigulu amefanya hivi makusudi ili watumishi wakatwe fedha wakiwemo hao walimu pasipo kugundua na kufanikisha malengo yao ya kampeni za 2015.
 
Na ni vema tukatafakari zaidi ya mara moja hii kauli ya Mwigulu eti anadhibiti watumishi wanaolipwa mishahara hewa kwa hiyo mishahara yote ya Watumishi italipiwa kupitia hazina, kwanza kabisa tangu utaratibu huu uanze hakuna Salary Sleep zilizopelekwa halmashauri ili watumishi wajue uhalisia wa mishahara yao kwa hiyo Mwigulu amefanya hivi makusudi ili watumishi wakatwe fedha wakiwemo hao walimu pasipo kugundua na kufanikisha malengo yao ya kampeni za 2015.


Duuuuh nilijuaga umeenda shule hata kidogo kumbe papai tu kichwani?

Salary sleep ndo kitu gani? ndo maana mna poor reasoning Sana maana hamna akili...


siku nyingine usirudie inaitwa Salary Slip
 
Duuuuh nilijuaga umeenda shule hata kidogo kumbe papai tu kichwani?

sary sleep ndo kitu gani? ndo maana mna poor reasoning Sana maana hamna akili...


siku nyingine usirudie inaitwa Salary Slip

Hovyooo!
 
Duuuuh

sary sleep ndo kitu gani? ndo maana mna poor reasoning Sana maana hamna akili...

...sary, najiaminisha ulitaka kuandika salary.
Ni suala la typo tu hasa kwenye viscreen tachi vyetu
 
...sary, najiaminisha ulitaka kuandika salary.
Ni suala la typo tu hasa kwenye viscreen tachi vyetu


Nilikuwa namrekebisha yule punguani ktk hali ya kawaida msomi huwezi andika salary sleep...
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Jk na serikali yake wameamua kuwakamua walimu ili ajaribu kujenga maabara kwenye sekondari za kata ambazo watoto wengi wanajiunga na kidato cha kwanza ilhali hawajui kusoma wala kuandika. Tunaomba kikwete amalize muda wake mapema ili rais ajaye aifufue elimu yetu inayoelekea kufa.
 
Walimu umoja hawana... maana wangekuwa wamoja wangeandama nchi nzima kupinga.
haa haa,mkuu nasikia walimu ndo wanaoongoza kuisaidia ccm kwa kuchakachua kura wakati wa uchaguzi ili ishinde kwa kishindo!
 
Let them learn a lesson... Maana wakiambiwa CCM ni hatari kuliko UKIMWI wanafikiri masihara....
 
Duuuuh nilijuaga umeenda shule hata kidogo kumbe papai tu kichwani?

sary sleep ndo kitu gani? ndo maana mna poor reasoning Sana maana hamna akili...


siku nyingine usirudie inaitwa Salary Slip

Ila mbongo ni mtu wa ajabu sana ona linamsimanga mwenzake wakati na lenyewe limeandika Sary, wakati mkosolewaji aliandika Salary
 
Back
Top Bottom