Duh maswali magumu haya, tumuite na
EMT pia huenda akatusaidia. Ila mimi nafikiri kama sijapewa sababu ya kutomtrust mtu basi sina sababu ya kutomtrust. Sasa kwa kiwango gani nitamtrust itategemea namtrust na kitu gani? Mfano l want to do business with you, ninapaswa kutrack record yako of course baada ya wewe kunipa maelezo yako. Baada ya kujiridhisha then sina machaguo zaidi ya kukutrust with my money.
Kaunga,
Hili suala ni deep. Kama alivyowahi kusema
S. S. Phares kwenye
thread moja, "Watanzania "asilimia ya kutosha ku-notice" walioko mijini ni kweli sio waaminifu. Huo ndio ukweli na wala sio majungu wenyewe mnajua. Huko vijijini ni mmoja mmoja sana kukuta sio waaminifu."
Mazingira akasema yake kuwa "Taarifa zisizo rasmi ni kuwa mojawapo ya sababu za kufungwa kwa Shoprite ya pale Lumumba ni kwamba wafanyakazi wao walikuwa wanawaibia sana."
Katika kudhibitisha haya
Kang akasema "Hili tatizo lipo, sijui kama ni unique to Tanzania lakini lipo. Mama yangu ana bishara yake ndogo, kila mtu (
100%) aliyejaribu kumwajiri pale alimwibia, sasa hivi ameona akae peke yake maana ni hasara tu."
Kuhusiana na kufungwa kwa Shoprite kwa sababu ya tatizo la uaminifu, akasema "Hili ni kweli, kuna siku nilikuwa nimetoka kununua kitu mle, mmoja wa wafanyakazi akanivuta pembeni akasema kuwa anaweza akawa ananitolea vitu nje kwa bei ndogo zaidi."
WomanOfSubstance nae akamwaga razi zake kuwa "Sasa hivi kuna utamaduni mbaya umejengeka kwa wa Tanzania - kutaka utajiri/mafanikio ya haraka haraka bila kuvuta subira na kusota. Siyo mahotelini tu. Ni kila mahali. Ukianzia kwenye makampuni ya simu, mabenki, na kwingineko utaona kamtindo fulani kwamba watu wanatafuta mashindano kwa kukwapua fedha kwa njia za wizi na ushahidi wa wazi upo. Kibaya zaidi ni vijana ndio wanaotaka take off ya haraka bila kujikongoja wakisahau kuwa hata ndege kabla haijapaa inaenda mwendo wa pole na baadae kuongeza kasi hadi kupaa. Hili tusilifumbie macho kabisa.Tukubali kuwa Tanzania uaminifu sehemu za kazi bado haupo.Waajiri wengi hata wa Tanzania wenye biashara zao, wanaona afadhali uajiri mgeni kwa gharama za juu kidogo ili uwe na amani kwa maana MTZ MWENZIO ATAKULIZA!"
Kama umejijengea mazingira ya kuwa trusted, watu wengine wataku-trust. Lakini kama unaishi kimachale, watu wengine nao wana haki ya kuishi na wewe kimachale. They will never trust you. Matokeo yake ni kuwa na jamii ambayo siyo trustful. Ndiyo jamii tuliyonayo Tanzania. Niambie ni Watanzania wangapi ambao wakirudishiwa chenji zaidi ya wanayostahili huwa wanamrudishia mwenye duka?