Tuition imeua vipaji vya wanafunzi

Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
182
Jamani kama kuna shimo la kufukia vipaji, na uwezo wa kufikiri kwa wanafunzi wetu ni TUITION. Sijui wazo hili lilitoka kwa nani. Tution ilizaliwa miaka ya 1990s na mbaya zaidi baada ya mwaka 2000.
Tuition inafanya wanafunzi wasijiamini kabisa. Wanaona mwalimu wake darasani hawezi kumfundisha hadi aelewe na ndio maana anamtafuta mwalimu mwingine huku akijua msemo wa kiswahili usemao, wapishi wengi huharibu mchuzi.

Wanafunzi wa siku hizi hawapewi tena HOME WORK, badala yake akitoka shule akienda nyumbani anamkuta mwalimu mwingine akimngojea. Wanafunzi wetu hawajui kujisomea wenyewe au kutumia maktaba, hata kufungua vitabu na kutafuta mada anayokusudia hawajui, maana muda mwingi wanazunguka na vipeperushi vilivyochakachuliwa na waalimu wa Tuition. Vitabu vya literature ambavyo enzi za 1980s tulivisoma vizima kama vile MINE BOY, THINGS FALL APART, THE RIVER BETWEEN, nk siku hizi wanafunzi hawavijui hata sura yake kwani wanasoma vipeperushi tu. Uwezo wa watoto wetu umewekwa kapuni.
Enzi zangu nikitoka shule nikenda nyumbani nilikabidhiwa jembe kulima ili kuchangia ada. Siku hizi wanafunzi wetu hawana nafasi ya kazi za mikono maana wamezungukwa na waalimu pande zote. Wamezoea kulishwa tu, SPOON FEEDING. Tunakwenda wapi.
Zamani tulifundishwa na kuzoeshwa kuwa ili ufaulu 60% ni juhudi ya mwanafunzi mwenyewe na 40% ni msaada wa mwalimu. Siku hizi wanafunzi wetu wamegeuzwa, wanajitegemea 20% na 80% ni kutegemea mwalimu. Wanafunzi hata wenye uwezo hawajiamini kufaulu bila dudu hili TUITION.
Ninaomba serikali ifute mchezo huu mchafu wa TUITION kwani HUUWA VIPAJI NA UWEZO WA WANAFUNZI WETU KUFIKIRI. Serikali ilipe waalimu vizuri ili nao wafundishe vya kutosha na si ovyo ovyo kama ilivyo sasa na hatamae wanawaelekeza wanafunzi kuwa ukitaka kujua zaidi njoo jioni. Hii njoo jioni mabinti zetu hugeuzwa kuwa wake za waalimu. Mnafahamu hilo?

mwasemaje?
 
Swala la kufeli, kwanza linatokana na mtu mwenyewe, kuna watu Tuition zimewasaidia. Mimi tangu nianze chekechea mpaka leo hii nipo chuoni, sijawahi kwenda tuition hata siku moja, but nimesoma na watu ambao bila tuition (hasa za kina ustaadhi..mtegetwa) hawafaulu. So inategemea na mtu.

Kiukweli kwa sasa elimu inaonekana inazidi kuwa easy, yaani nashangaa topic kama glaciation, transport and communication zinafutwa tu, mtihani wa la saba wa hisabati una multiple choice, mtihani wa form two wastani unaotakiwa 25% na wengine wamefutiwa mchujo...sasa tunaelekea wapi?

Miaka ijayo, wahitimu watakuwa na shida sana kwenye kupata ajira. Nawapa pole sana.
 
Watu wanakula tuition hadi unashangaa wana ubongo gani hawa hawaelewi tu! hahahha, mimi madogo zangu nawapiga mkwara kila siku kuhusu tuition! Nawanunulia vitabu wanajisomea, wakikwama wananiuliza mie mwenyewe! Pamoja na hayo extra duty ni mhimu kuwajenga upande mwingine.
 
Elimu imebaki kuwa ilimu,nimeshangaa leo nimeona paper ya form four history mwanafunzi anaambie explain six points,three points,five reasons kwenye maswali ya essay nikajiuliza hivi tunaenda wapi yaani unamlimit mwanafunzi kufikiri Elimu imebebakwa Kawambwa where are you?
 
Back
Top Bottom