Tuisusieni mlimani tv | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuisusieni mlimani tv

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Raia Fulani, Nov 14, 2009.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Wakati harakati za kuanzisha mlimani tu zinaendelea niliona kuwa haya ni mapinduzi ya kitaaluma. Kinyume chake ni tofauti. Nasikia kwa vile wachina wana mkono wao hapo basi kila nikiifungua nakutana na cctv na simulizi za kichina. Hii ni hasara na matusi kwa jamii ya wasomi. Wanavyuo wana mambo lukuki ambayo wangeyafanya kupitia tv hiyo kutegemeana na fani zao. Mfano wale wa FPA wangetuonyesha sanaa, wale wa uhandisi wangetuonyesha ufundi wao. Wa siasa wangetuonyesha midahalo na namna ya kujenga hoja, n.k. Pia wanavyuo wana matatizo mengi. Nawaona muda wote. Accomodation kwao ni tatizo sugu. Sio kwa sehem ya kulala tu, pia viwango vya malazi ni duni. The issue of flexing capacity when demand is high. Wazungumzie library na nini kifanyike kuiboresha. Wazungumzie ubora wa walimu. Sasa wanawaachia wachina tu, na sie tutawaachia tv yao. Tunataka watengeneze vipindi vinavyoakisi yale wanayojifunza. Bila hivyo watz hasa wasomi watajua sarakasi za kichina na tamaduni zao kuliko tamaduni za kitanzania. Kwa maana hiyo hakuna sababu ya kuendelea kuingalia hii 'cctv'
   
 2. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Good Observation....nimeipenda!I join issues with you.Nafikiri hii ndo tatizo la watanzania kujikomba kwa wachina au tuseme mkataba wa kusaidiwa kupata hiyo station ya TV umetufunga kiasi cha kutulazimisha kuwaonesha wachina kila dakika...sitaki kuamini hivyo!
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Yap, tubadilike watanzania. Tusirubuniwe kwa pipi
   
 4. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #4
  Nov 14, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  acheni ujinga ...roma haikujengwa kwa siku moja....hamuoni fahari ...chuo kikuu cha pili afrika ya mashariki baada ya sua kuwa na tv yenu????...kiongeni mkono ...kuandaa vipindi ni gharama ....ni jukumu pia la wanafuzi kubuni mbinu nafuu za kuandaa vipindi kwa gharama nafuu....

  mnajuwa kama china walisaidia vifaa kwenye uanzishwaji wa tv mlimani....mlitaka tv mliamani wawe wanaji align na cnn??????

  tangu lini mlimani wanafunzi wanaji align na mabeberu???
   
 5. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...Mkuu, muanzisha mada ana hoja. kinachoendelea pale sasa hivi pale Mlimani si TV yetu! ni tawi la CCTV. Ndio kitakachotokea pia Teleisheni ya Taifa. Tusiwe wanyonge kiasi hicho! Naamini kuwa Mengi alianzisha kituo chake cha TV kwa mikopo ya Benki, lakini hii haikuwa sababu ya kufanya matangazo ya Benki yaonyeshwe kwenye kituo hicho 24/7!
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  Anza na tbc kwanza tuko nyuma yako
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kama phillemon mikael alivyosema tatizo ni kuandaa vipindi. Mbona mengi alikuwa anatuonyesha isidingo mpaka leo mbona hamsemi? Mlimani TV navyojua mimi imepewa vifaa na wachina, sasa mnategemea nini??

  Hayo ndo matunda ya CCM au mnataka nini zaidi??
   
 8. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,390
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kutumia jicho lako la tatu vyema,mimi naungana na wewe,na sioni umuhimu wa kuangalia hii tv tena bora niangalie miyeyusho ya kina joti!!
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ondoa fikra mgando. Roma haikujengwa siku moja ndio ila hakuna anaetangaza maslahi katika roma kama si waroma wenyewe. Nadhani huwajui wachina vizuri. Kupewa msaada sio tiketi ya kukaliwa kichwani. We ukipewa msaada na jirani yako ni sawa kwake kuja kushinda na taulo sebuleni kwako kisa alikusaidia?
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mie nilidhani ni tv station ya wachina ina train wanafunzi wa udsm
   
 11. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  CCTV ni miyeyusho sana... Habari zao hazi-reflect chochote katika jamii yetu,Bora hata Al-Jazeera. Zamani TBC walikuwa wanatuonyesha documentary za miaka ya uhuru hadi miaka ya 80 hivi kwa kweli wangevirudisha vipindi vile...
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hujakosea. Ni wachina wanawafundisha wasomi wetu chinese civilization
   
Loading...