Tuiangalie avg 9.0 kidogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuiangalie avg 9.0 kidogo

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Nov 15, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tafauti na version 8 mpaka 8.5 ambayo wakati unapotaka kuingiza kwenye computer ni lazima ufunge vitu unavyofanya kwenye computer yako kama unaangalia tovuti Fulani au kama unatumia programu ya word kusoma au kuchapa kitu kwanza ndio ikubali usipofanya hivyo basi itazifunga yenyewe , unapokuwa unataka kuinstall version 9.0 hautokuuliza suala la kuzima programu zingine au vile vitu ulivyokuwa unafanya wakati huo ingawa ni muhimu kufanya hivyo ili unapostart settings ziwe tayari intalled .

  Nimejaribu kuscan external harddrive yangu yenye data za zaidi ya GB 900 imetumia nusu ya muda wa toleo lililopita la AVG ,

  Kwa wiki nzima sasa nimekua naitumia Antivirus hii ile free edition ambayo ni bure pamoja na professional edition hii inauzwa pamoja na internet security , kitu kingine nilichoangalia ni kama inasema uwongo kuhusu baadhi ya tovuti .

  Kama kawaida nilivyoinstall kwenye computer nikaenda kwenye search engine nikatafuta tovuti moja hivi ambayo ni haramu kweli AVG ikaniambia tovuti hiyo ni haramu nilipojaribu kuichungulia ikaniambia tovuti ninavyoingilia sio salama chochote kinaweza kutokea kama naingia basi ni kwa kutaka kwangu mwenyewe , sasa ukiwa na antivirus nyingi ambazo zina matoleo mapya sasa hivi haziwezi kutambua tovuti hiyo kama si salama kwenye avg kuna kitu kinaitwa Link scanner ndio inaweza kufanya hivyo .

  Pamoja na hiyo inaweza kuzuia computer yako kudownload programu ambazo hazitakiwi hizi ni pamoja na zile zinazokusanya taarifa binafsi za watu bila ya wao wenyewe kujua na kuzifuta moja kwa moja kwa kukupa taarifa ambayo ina popoup kwenye taskbar .
  Kitu ambacho hupati kwenye hii free edition ni firewall ambayo ni kama ukuta wako kuzuia wengine wasiweze kukuona kwenye mitandao ingawa kama unatumia windows basi ina firewall yake ingawa haina ufanisi kama hizi zingine kama unataka firewall nzuri mimi huwa natumia zonealarm pia jua hii imenunuliwa na kampuni moja ya huko Israel sasa watu wa mashariki ya kati wanaiogopa sana wanahisi kwamba labda inatumika dhidi yao ila ni moja ya firewall nzuri zaidi duniani haijawahi kushuka kimasoko toka imeanzishwa .

  Pia huwezi kupata msaada wa bure toka kwa AVG wenyewe ingawa kuna sehemu ya forum ambayo unawezakuungana na watumiaji wa AVG wa sehemumbalimbali duniani kubadilishana nao mawazo na maswali na game mode hii ina weza kukusaidia pale unapocheza game kwa njia ya mtandao kukulinda dhidi ya shambulio lolote kwa njia ya games .

  Avg Technologies imekuwa inalinda watu dhidi ya virus , spyware na aina nyingine ya matishio kwenye computer toka mwaka 1991 , huwezi kuamini kwamba kampuni hii iko kwa miaka 18 sasa tofauti na kampuni zingine ambazo zimekuwa sokoni kwa kipindi kidogo lakini huduma zake kwa siku za karibuni zimeonekana kusuasua kwa kasi .

  Naamini kuna vitu ambavyo hujaelewa unapenda kuuliza maswali , kuongezea , kusahihisha na mengine zaidi , usisite kuendeleza mjadala huu kwa manufaa ya wengine wengi wanaopenda kusoma na kujua

  Usiku mwema

  www.askmaro.blogspot.com
   
 2. k

  khalids19 Senior Member

  #2
  Nov 20, 2009
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Man AVG is the worst antivirus in the world dont u ever !!!!! Ever! think that AVG is an antivirus!
   
 3. C

  Chuma JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  shy ....sina hakika nimeona ktk post moja unahusika na web ya Ikulu ni kweli?
   
Loading...