Tuhuma za ukabila/ Ukanda zafutika CHADEMA

Tuhuma za ukabila/ Ukanda zafutika CHADEMA

Msulibasi

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
5,957
Reaction score
8,005
Nimefuatilia hoja na shutuma za wabunge waliosigishana na wengine aidha kuondolewa au kujiondoa Chadema.

Jambo la kujivunia ni kwamba wote hawajatoa shutuma za ukanda ama ukabila. Kero kubwa wanayozungumzia ni misimamo mikali ya mwenyekiti Mbowe na Ruzuku.

Katika kipindi cha nyuma tungalisikia ooo uchagga ooo ukaskazini nk . Lijualikali, Silinde Cecil Mwambe Mashinji,Patrobas wote hoja yao ni Mbowe, Ruzuku Michango.

Inawezekana vyama vingine kikiwemo chama tawala vimekosa moral authority kuishutumu au kuchokonoa mambo ya ukanda na ukabila kwani huwezi rusha jiwe ukiwa kwenye nyumba ya kioo.

Inawezekana pia kuna ukweli uliotukuka kuwa mambo hayo ya ukabila hayopo katika chama hicho.

Vyovyote iwavyo Chadema ni mfano wa kuigwa kwa vyama vyote ikiwemo chama tawala kwa kuwa na sura ya kitaifa bila ubaguzi wowote.

Sent from my SM-T337V using JamiiForums mobile app
 
Hizo tuhuma zilipedwa, sasa hivi mashambulizi yote ni kwa Mwenyekiti wao, maana imeandikwa mchape Mchungaji ili kondoo watawanyike...

Wanachokosea ni kwamba Je wana uhakika Mh Mbowe anaowaongoza kondoo ba si Mbuzi...
 
Tumeibiwa vya kutosha, tujengeni nchi, ukabila piga chini, ukanda pia kemea, wizi nao tupambaneni nao hata kwenye Vyama vyetu, mmadicteta hatuwataki, na huu Wakati wa mdoloro wa Uchumi duniani, Tumwambie Raisi awashike wote waliodaiwa/wanaodaiwa kukwapua pesa za Watanzania na kuzificha ughaibuni, huu ndio Wakati wa wao kufanyiwa udicteta, walete pesa zetu tuimarishe Uchumi wetu

Sisi sote tunataka nchi isonge, Kwa pamoja tujengeni nchi yetu,

Mwacheni Mbowe, anayemdai aende ofsini kwake au ampeleke mahakamani, Sisi tunachotaka na tunahasira ya kujenga nchi yetu tu
 
Nimeona Mbowe akikwaruzana na Kina Selasini na yule director of finance Komu ambao kimsingi ni wa mkoa wa Kmanjaro lakini akipata ufuasi mkuu kutoka kwa kina Lisu, Sugu, Heche, Bulaya ambao ni nje ya Knjaro. Hii inadhihirisha kuwa migogoro chanzo chake ni maslahi mengine si ukanda

Sent from my SM-T337V using JamiiForums mobile app
 
" Kwamaana hiyo unapenda jinsi chuki za kikabila zinavyoenezwa juu ya chama??? nini dhamira yako kama jambo halikujitokeza katika matamko ya wabunge hao?? means kama usingalisema tusingali fikiri juu ya hayo. LISEMWALO LIPO.
 
Hizo tuhuma zilipedwa, sasa hivi mashambulizi yote ni kwa Mwenyekiti wao, maana imeandikwa mchape Mchungaji ili kondoo watawanyike...

Wanachokosea ni kwamba Je wana uhakika Mh Mbowe anaowaongoza kondoo ba si Mbuzi...
Za ndani ni kuwa mashambulizi kwa Mbowe yanapamba moto sana baada ya Mbowe kuudhihirishia ulimwengu huu kuwa kamuacha mbali sana Jiwe katika broad knowledge, hekima, busara, hata ujanja wa mjini.
Mpango wa kumshambulia Mbowe binafsi ni kwa sababu Jiwe mwenyewe ndio jambo linalomfurahisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada swala ukabila na ukanda ndani ya Chadema lilikuwepo miaka ya nyuma kidogo.

Ilifikia hatua mpaka Makamu Mwenyekiti wa Chadema miaka hiyo Marehemu Chacha Wangwe aandike waraka mzito kuhusiana na Chadema na moja ya mambo aliyoyatuhumu tena kwa ushahidi mzito ni pamoja na Ukabila/Ukanda na matumizi mabovu ya pesa za ruzuku na michango ya wanachama ktk chama hicho cha chadema ( Tafuta waraka wa Chacha Wangwe uusome).

Kwahyo kwa nyakati za hivi sasa, angalau cdm imejitahidi kubalance mizania ktk kupunguza ukabila/Ukanda isipokuwa matumizi ya fedha bado ni changamoto!!
 
Acha kauli za kujifurahisha!

Kamuachaje mbali ilhali mmoja hapo ni Raisi wa Nchi mwenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya Taifa hili wkt Mbowe ni kiongozi wa Chama ambacho kila kukicha kinakimbiwa na viongozi, wabunge na wanachama wake!!??

Mmoja sasa hivi kaongeza ushawishi mara dufu zaidi kwa wananchi ndani na nje ya nchi baada ya kukataa lockdown ilhali mwingne alikuwa ana force lockdown isiyoungwa mkono na wananchi walio wengi

Acheni kufananisha Buggati na Passo
 
Mleta mada swala ukabila na ukanda ndani ya Chadema lilikuwepo miaka ya nyuma kidogo.

Ilifikia hatua mpaka Makamu Mwenyekiti wa Chadema miaka hiyo Marehemu Chacha Wangwe aandike waraka mzito kuhusiana na Chadema na moja ya mambo aliyoyatuhumu tena kwa ushahidi mzito ni pamoja na Ukabila/Ukanda na matumizi mabovu ya pesa za ruzuku na michango ya wanachama ktk chama hicho cha chadema ( Tafuta waraka wa Chacha Wangwe uusome).

Kwahyo kwa nyakati za hivi sasa, angalau cdm imejitahidi kubalance mizania ktk kupunguza ukabila/Ukanda isipokuwa matumizi ya fedha bado ni changamoto!!
Nafurahi kusikia kuna chama cha ushindani kinachokubalika Tanzania nzima. Tufahamu kuwa chama tawala kinaweza kuwa na sifa mbaya ya ukabila lakini kikapata wafuasi kwa kutumia nguvu ya dola yaani mikwala ya polisi au kwa kutumia nafasi yao ya kugawa raslimali za nchi. Naamimi CCM ya sasa nje ya dola ingenuka ukabila na ukanda

Sent from my SM-T337V using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom