Tufanyeje jamani hapo Mwananyamala?

Tufanyeje jamani hapo Mwananyamala?

mmakonde

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2009
Posts
965
Reaction score
69
Mwananyamala.jpg
 
Wajawazito kulala na kukaa chini ni moja ya matatizo makubwa ya sekta ya afya nchini.

Viongozi wetu wanaona na kusoma mambo haya?
 
inatia hasira kibinadamu, but any way tukibadirika kifikra na kujikomboa kiakili
na serikali itabadirika maana watapatikana viongozi wenye utu watakaopatikana kwa
kuchaguliwa na watu waliobadirika na kujikomboa kutoka kwenye akili na fikra kandamizi
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Toweni CCM madarakani kwani jibu hamlijui?

Biliioni hamsini zinazochangiwa CCM zingenunua vitanda vingapi, zingejenga wodi ngapi, zingelipa madaktari wangapi hivi watanzania macho yetu kwa nini tumeweka ulimbo hadi tusione, hivi watanzania kwa nini masikio yetu tumeweka pamba hadi hatusikii, hivi kwa nini Watanzania midomo yetu kumeweka pattex hadi hatusemi na mwisho kwa nini watanzania hatutaki taabu ya kufikiri leo ili tupate raha kesho? Kunapenda raha ya leo kwa taabu za kila miaka mitano???????
 
Toweni CCM madarakani kwani jibu hamlijui?

hilo si tatizo mkuu
kama watu hatujitambui, hatuwezi kusonga mbele, maana tutaitoa ccm na kuingiza bomu jingine
kikubwa ni kila Mtanzania kuanza kuangalia sasa, na kujichunguza kama fikra zake ziko huru, anajijua, anafahamu
ametoka wapi, yuko wapi, kwa nini hajafika, amekwamishwa na nini,

tuondokane na hilo ili tutoke kwenye siasa za ujuha, ....maisha bora kwa kila mtanzania.....
huku hatupewi vyelelezo yatapatikana vipi, kazi kupiga makofi.....MUNGU na alaani hii tabia..
 
inatia hasira kibinadamu, but any way tukibadirika kifikra na kujikomboa kiakili
na serikali itabadirika maana watapatikana viongozi wenye utu watakaopatikana kwa
kuchaguliwa na watu waliobadirika na kujikomboa kutoka kwenye akili na fikra kandamiz
i

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Lini anyisile? kama kweli tuna mapenzi na nchi yetu basi kitu hiki kifanyike oktoba 25 miezi mitano toka leo. je wapiga kura wameamka kiasi hicho au ni maneno tu?
 
Ningekuwa WM Pinda ningewaita TCRA, EWURA, SUMATRA, NSSF, PPF na taasisi nyingine za UMMA zinazokusanya mapesa kwa mujibu wa sheria zilizozianzisha wamalize tatizo hili mara moja. Wanajenga tu maghorofa huku Watanzania kwa mamilioni wanateseka kwa huduma muhimu kama hizi!
 
Lini anyisile? kama kweli tuna mapenzi na nchi yetu basi kitu hiki kifanyike oktoba 25 miezi mitano toka leo. je wapiga kura wameamka kiasi hicho au ni maneno tu?
Ni kweli Ngambo Ngali
tatizo, sehemu kubwa ya Watanzania, tumekuwa akina Esau, kuuza utu kwa sababu ya njaa tu
tena ya siku moja ambayo hulisumbua tumbo kwa mda mfupi,
kumbuka kuwa ccm inawategemea sana majuha na wajinga ambao ni wengi mno nchini
maana mi hainingii akilini kuona ccm inazidi kujitanua katikati ya watu ambao imewatesa,
na inaendelea kuwatesa, ama hii ni kwa sababu ya ubaridi wa raia?
 
Watanzania tunaendekeza sana matumbo, njaa za siku moja ndo sababu ya matatizo ya miaka mitano, tuwaelelze hivyo wananchi mweleze mwanao, kaka yako, dada yako jirani yako, nyumbani, kwenye basi, sokoni msikitini, kanisani mueleze kuwa kama miaka 50 baada ya uhuru watu wanalala chini hospitali, waafunzi hawana madawati, barabara hakuna mijini na vijijini je wataweza kujenga miaka mitano tutakayoongeza?

Kama hapo mwanzo tulifanya makosa kuwa na imani na chama kisicho na mwelekeo wa maendeleo hatuna budi kusahihisha makosa hayo na njia pekee ya kufanya hivyo ni kuchagua chama kingine.
 
Ngambo Ngali

Leo mkuu unahasira sana na hawa jamaa zetu walio madarakani!
 
Ningekuwa WM Pinda ningewaita TCRA, EWURA, SUMATRA, NSSF, PPF na taasisi nyingine za UMMA zinazokusanya mapesa kwa mujibu wa sheria zilizozianzisha wamalize tatizo hili mara moja. Wanajenga tu maghorofa huku Watanzania kwa mamilioni wanateseka kwa huduma muhimu kama hizi!

Hata hawa TIGO,ZAIN ,VODACOM,NMB and the like wana uwezo mkubwa sana wa kuchangia hizi huduma za muhimu tena bila ya hasara.mbona kwenye umisi TZ,mipira na kuwaleta akina J-Martins wapo mstari wa mbele?
Wafanye marketing zao hata mwananyamala hospital tutawaona wa maana.
 
Ndio mafanikio yenyewe hayo mawaziri wanataka kuanza ziara kuyaelezea!!!mweeee nji hii!

Ukishawishiwa jambo baya na SISiem waambie Baba hapendiiii
 
Ndio mafanikio yenyewe hayo mawaziri wanataka kuanza ziara kuyaelezea!!!mweeee nji hii!

Ukishawishiwa jambo baya na SISiem waambie Baba hapendiiii
hahahahahaaa.Sisiemu kama wanatumia vimizizi vile kurubuni watu.Mfano hao wasanii wanashawishiwa na wanakubali kinyume na maneno yao ya harakati za mapinduzi.
 
Watanzania tunaendekeza sana matumbo, njaa za siku moja ndo sababu ya matatizo ya miaka mitano, tuwaelelze hivyo wananchi mweleze mwanao, kaka yako, dada yako jirani yako, nyumbani, kwenye basi, sokoni msikitini, kanisani mueleze kuwa kama miaka 50 baada ya uhuru watu wanalala chini hospitali, waafunzi hawana madawati, barabara hakuna mijini na vijijini je wataweza kujenga miaka mitano tutakayoongeza?

Kama hapo mwanzo tulifanya makosa kuwa na imani na chama kisicho na mwelekeo wa maendeleo hatuna budi kusahihisha makosa hayo na njia pekee ya kufanya hivyo ni kuchagua chama kingine.
yaaa hiyo itasaida sana mi najaribu usema kuendelea kutawaliwa na ccm ni janga
sana sawa na kuendele kuteswa na watu waloshika fimbo kama siraha zao wakati sisi tumeshika mapanga, majembe, mikuki kama siraha za kujihami, akili, fikra na ufahamu tukiviamsha, tunaweza kuwakatilia mbali na wakashangaa,

hatuwezi kusubiri mtu mwingine aje atufundishe jinsi ya kuzitumia siraha hizo ni jukumu letu sote
kuhakikisha tunaamka Oct na kuwaondoa hawa matapeli wa uchumi wa nchi,
 
Back
Top Bottom