Tuendelee au nimuache aende zake

Tuendelee au nimuache aende zake

Kwa huu mwandiko tayari ushamkubalia kurudiana,hapa umekuja kututafutia lawama tu!the truth is,alipata njemba imemburuza na kumubwaga so anapooza machungu kwako vile anajua unampenda na hufurukut!...anyway just trust her na ukufe na distance love!
 
Kuna mambo ukikubali kudanganywa hata anaekudanganya anakuona ni jinsi gani alikuwa sahihi kukufanyia alivyokufanyia. 2 yrs mtu kakuacha alafu anakuja na uongo huo unajishauri, sijui unajishauri nini ila hakustahili hata kama bado unampenda.
Pole.
 
Kama utaweza kusahau yote aliyofanya hiyo miaka miwili rudiana naye kama hutaweza usirudiane naye

Akilini weka hii kitu "Fimbo ya mbali haiui nyoka"
Ni miaka 2 Sasa toka nikate mawasiliano na aliyekuwa mchumba wangu. Jmosi iliyopita amenitafuta baada ya hiyo miaka 2! Tulidumu kwenye mahusiano km miaka 3 na miezi kadhaa kutokana na changamoto za maisha tulikuwa tunakaa Sehemu tofauti.Baada ya yy kihamia mkoa mwingine mawasiliano yalianza kuwa ya shida.Alikuwa anakaa hata mwezi bila kuongea na mm.Hii hali ilikua inaniumiza na nilijaribu Kila namna kurekebisha ila baadae yalikata kabisa! Nikawa najaribu kumtafuta Hadi kupitia marafiki zake wakawa wanasema watamfikishia taarifa ila hakuwahi kunitafuta! Ni mtu ambae tulikuwa tunaendana kwa vitu vingi na nilimpenda sana! Wakati wote huo ambao alikuwa hapatikani nlikokuwa ni mtu mwenye mawazo, huzuni, hasira,kulia,kisirani na nikawa mtu wa tofauti kbs!Nikaona kuwa ndio mwisho wetu na tumeshaachana. Ilininichukua muda sana kukubaliana na hali hali hallisi hadi Kuna wakati niliugua sana na kukonda.Hadi hii juzi ndio amenitafuta baada ya ukimya wa miaka 2! Nilimuuliza kwnn alipotea ghafla alinielezea stori ndefu ila ni kwamba alipata changamoto nyingi na baadae kuhama nchi. Alipata kazi nchi nyingine ( hapa Africa)na Hadi Sasa anafanya kazi huko na amekuja kwa ajili ya likizo' kisha atarudi huko.Ameniomba msamaha na anahitaji turudiane. Nilimuuliza kuhusu mawasiliano yetu itakuaje akasema atayaboresha na atakuwa anakuja kuniona Kila likizo. Akili inakuwa ngumu sana kumuamini japokuwa bado nampenda.Nikifikiria hali ngumu niliyopitia Hadi kuwa sawa naona ni ngumu kuamini tena.Katika hii miaka miwili ambayo hatukuwa pamoja,nimekuwa na mahusiano kadhaa ambayo mengine hata mwezi haufiki tunaachana.Nikubali tuanze upya na kuamini tena? au ni mpasha kiporo nimuache aende zake tu? Nikimuamini af azingue tena mtanisindikiza Mirembe🤌😂) Wadau niamue nini??
Wenzio wamechezea muda wote huo naww kwakua penda penda umemkubalia tyr maana humu hakuna majibu ila yaliopo kichwani mwako ndio majibu na umemkubia tyr.
Mwenzio anatafuta maisha anapoona yanasogea anaweka nanga sasa zamu yako akikuchoka anasepa
 
Kiuhalisia wanaume wengi huwa hatuwezi kumtamkia moja kwa moja mwanamke kuwa "sikupendi" hasa tukionyeshwa na wanawake kuwa tunapendwa kuna muda huwa tunawatafutia makosa ili tuachane tukikosa hayo makosa huwa tunaanza kujitenga kwa kukata mawasiliano.
 
Back
Top Bottom