Asante
JF-Expert Member
- Dec 18, 2009
- 2,084
- 1,076
umuiya ya Wakulima wa Kilimo Hai Usambara Mashariki (JUWAKIHUMA) ni chama kinachounganisha vijiji sita vilivyopo milimani Usambara Mashariki wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.
Wakulima wa maeneo haya wanalima sana mazao ya viungo vya chakula hasa pilipili mtama, iliki na karafuu. Karafuu inayolimwa eneo hili ubora wake ni mkubwa kuliko karafuu inayolimwa Pemba na Unguja. Pia eneo hili yapo mashamba makubwa ya serikali ya miti ya mipira, iliyokuwa inatumika kama malighafi kwa kiwanda cha matairi cha General Tyre, Arusha.
Pilipili mtama ndilo zao la kwanza nchini lenye bei nzuri kwenye soko la ndani, bei yake kwa sasa ni kati ya shilingi 400,000/= hadi 600,000/= kwa gunia la kilo 100, sokoni Kariakoo.
Serikali ya Marekani kupitia shirika lake la misaada la USAID limewasaidia sana wakulima wa vijiji hivi sita, kuendeleza mazao yao, kiasi kwamba hali ya maisha ya wakulima imebadilika sana, na kila eneo utakalopita utakuta wakulima wanapanua mashamba na vitalu vya miche mbalimbali vikiwa mashambani, vikisubiri msimu wa kupanda.
Kama simu nizokupa hazipatikani inabidi ufunge safari hadi Handeni Tanga, kutoka handeni ni muda wa saa moja kufika milimani Usambara Mashariki, uliza ofisi zao zinaitwa JUWAKIHUMA.