Tuelimishane kuhusu Kilimo cha Pilipili Manga, kuanzia mbegu bora, magonjwa, utaalamu mpaka masoko

Pilipili Manga?

Pilipili hoho?

Pilipili kichaa?

Pilipili mbuzi?

....ipi unataka kulima
 
Wakuu habari.

WanaJF naomba ujuzi kidogo kwa mwenye uelewa juu ya soko la Pili Pili Manga.
Nataka kujikita kwenye hii biashara kwani kwa taarifa nilizopata ni kuwa bei yake huwa juu sana kwenye mwezi wa tatu.
Kama kuna member ambaye ameshawai kufanya hii biashara ningeomba anisaidie kunipa maelezo na mimi nipate mwanga zaidi juu ya hili zao.

Ahasante.
 
Wakuu kwema,

Nilisafiri kidogo kwenda maeneo ya Tanga maeneo ya Tongwe, Masimba, Zimbili kwa ajili ya kufatilia mazao ya viungo vya chakula.
Nimeona nishare na nyinyi vitu vichache ambavyo nimejifunza kuhuusa mazao ya viungo vya chakula. Kuna kipindi flani nilianzisha uzi kuhusu soko la pili pili Manga lakini sikupata jibu hivyo nikaona ni heri niende kwa wakulima kujua zaidi kuhusu Pili Pili Manga.

Pili pili Manga ni moja ya zao ambalo linauzwa kwa bei nzuri sana kwa muda sasa, hivi sasa bei ya pili pili Manga ikiwa kavu kule kwa wakulima kilo moja inaenda kwa shilingi 11,000 na huku Dar es salaam inaedna mpaka 18,000 japo sijaulizia kwenye masoko ya Kariakoo na mengine hio ni bei tu kwa wafanyabiashara wanao safirisha nje ya nchi.
Japo kuwa bei ni nzuri ila kuna shughuli kidogo ya kufanya ili uweze kufikia malengo.
Kabla ujaamua kuingia kwny zao hili ningependa ujue ya fuatayo:

- Uzito wa Pili pili Manga zikiwa mbichi na pale utakapokuja kuzikausha huwa zinapungua sana, ukikitua zimekoma ni ratio ya 3:1 na zikiwa mbichi inaweza kwenda hata kwa 10:1 hapa niki maanisha unapata kilo moja kwenye kilo tatu au kilo moja kwenye kilo 10. ina maana kama zimekoma ukanunua mbichi kilo 1000 ina maana utapata kavu kilo 300 au 350 inategemea na ukomavu wake. ila kama umepata mbichi unaweza pata kilo 150 au 200 kwny kilo 1000.
- Utajuaje kama Pili pili imekomaa au mbichi, ikiwa bado changa kwa shina lake lina kuwa na mapengo pia zile mbegu ukiziminya zinapasuka na kutoa uji mweupe. Ila ikiwa imekomaa ukiminya zile tunda za Pili pili Manga utatumia nguvu sana kuipasua unaweza ukaipasua au zingine zinaweza kukushinda kabisa kupasua, na kama ikipasuka kirahis haitatoa uji uji bali utapa kikokwa cha size ya gololi ndogo.

- Pili pili Manga ikiwa mbichi bei yake huanzia shilingi 1500 mpaka 2000 ila makubaliano ni ww na mwenye shamba mfano anaweza kukuuzia pili pili kwa shilinig 1500 ila wachumaji juu yako, wachumaji huchukua shilingi 300 kwa kilo moja au anaweza kukuuzia kilo kwa 2000 ila wachumaji juu yake wewe unakaa unasuburia mzigo tu.

- Angalizo wakulima huwa na longo longo sana na wanapandisha bei kila kukicha wakisikia jirani ameuza kilo 2500 basi wote watauza kwa 2500. mimi nilifika kilo inauzwa 2000 ila ndani ya siku 4 kilo iliuzwa 3700 wakulima wakiona wanunuzi wanakuja na kutaja makilo mengi mengi na wao hupandisha bei, pia wengine huamua kukuchumia pili pili ambazo hazijakomaa ili mradi wa wai soko.

- Kua makini na Pili pili ambazo zinalimwa maeneo ya milimani mara nyingi huwa hazikomai mapema ila huwa zinambegu kubwa zimeshiba yani ukiziaangalia kwa wasi wasi unaweza kuvutika na kuona biashara ndo hii ila kila ukitest utakuta zote ni changa.

- Kama unaweza kuingia shambani na kuangali mzigo kabla haujachumwa nalo sio jambo baya ila kama hutaweza wewe cha msingi ni kumwambia tu mkulima kuwa akileta changa huchukui maana wengine wakorofi anaweza kukuletea changa ukachukua alaf mwisho wa siku ukapata hasara wewe.

- Pili pili manga unaweza kuzihifadhi kwa muda mrefu kama tu utahakikisha zimekauka vizuri, Pili pili manga zinahitaji jua kali la siku mbili mfululizo ili ziwe kwenye ubora unaotakiwa. Kama utazihiifadhi kabla ya kukauka vizuri zitaweka ukungu na ni shida sana kuzirejesha kwenye ubora wake, ila pia unaweza zikausha kwa siku moja kama ukitaka kuziuza huko huko shambania uzito wake huwa bado uko juu kiasi flani. Pili Pili isipi kauka vizuri kama utaamua kuiweka ndani usubirie soko itaendelea kupungua uzito hivyo ni vyema kuhakikisha ina kauka vizuri ili kama unasafirisha au unaweka ndani kwa muda fulani uikute katika ubora ule ule. Pia tumia magunia ya mkonge sio ya manila kwa ajili ya kuhifadhia.

Nilichokiona kingine ni kuwa kama una mtaji wa kutosha unaweza kuchukua zikiwa kavu kwa bei itakayokuwepo ama unaweza fika kijijini ukaamua kuvuruga bei, mfano wanauza kilo 10,000 wewe labda una haraka na mzigo na mteja unaye tayari wewe unatangaza bei kuwa 11,000 kwa kilo au 10,500 kwa kilo unapata mzigo fasta sana. Changamoto ya kufata bei iliyopo itakufanya ukusanye mzigo mdogo mpaka kufikia lengo.

Ushuru- hili ni la kuzingatia usipo lipa ushuru kijijini kule jiandae kulipa ushuru muheza mjini na ushuru wake ni shilingi 300 kwa kilo. Kwa kijijini kule huchukua gunia moja kwa shilingi 5000 au elfu 10,000 inategemea na ukubwa wake.

Mazao mengine yanayopatika katika vijiji vya karibu ni Iliki ambayo ikiwa mbichi huuzwa kwa bei ya juu kabisa ni kilo moja 18,000 na ile ambayo utaikuta mkulima ameikausha inaenda mpaka 25,000 kwa kilo.

Mazao mengine ila sikufanikiwa kupewa details zaidi ni;
Mdalasani, cocoa, mchachai vyote hivi kilo 3000 mpaka 4000
Ushafirishaji ni changamoto kama una magunia machache ila kama una magunia mengi mafuso ni mengi sana unaweza ongea nao wakakufanyia bei nzuri ila mabasi pia yanabeba sema bei zao ziko juu wanaweza kuchukua 15,000 kwa gunia moja.

Soko la bidhaa hizi ni kubwa ila inabidi ulisaka haswa na uwe na connection nzuri, watanzania wengi wanapeleka Mombasa kule bei iko juu sana, sema wengi waligoma kuniambia kwa Mombasa bei ikoje waliishia tu kusema inalipa lakini hakuna aliyenipa jibu.
Wakulima ni wepesi sana kutoa taarifa zote kuhusu zao husika ila wafanyabiashara ni wagumu sana kukuelezea zao hili peleka sehemu flani bei iko vizuri. Bado naendelea kuuliza soko lake lakini kwa hali inavyoonyesha soko sio baya na ukiweza kuhifadhi mpaka kipindi ambacho zao linakuwa adimu kidogo bei yake huwa juu sana husasani tukielekea mwezi wa Ramadhani.

Wakulima walinipa ushirikiano wa kutosha sana kwa kila nilichouliza yani ndani ya siku moja nilikuwa nishajua kuna mazao gani na gani na wapi ya yanapatikana na bei zikoje na njia za kufika huko ila wafanyabiashara wengi niliokutana nao kila ukimuuliza kuhusu soko la Mombasa anaishia kukuambia tu inalipa sana.

Bado naendelea kujifunza juu ya haya mazao ila pia kama kuna mwenye uelewa zaidi na zaidi anaweza kushare hapa tuweze kujua kwa undani haswa kwenye swala la masoko ndani na nje.
 
Shukran saaana kwa somo zuri hakika umenibikiri skuwa najua chochte kuhusu hilo zao zaid ya kulikuta kwny uji wa futar tuuu
 
Nexttime utujuze na jinsi yanavyolimwa hayo mazo tajwa yawezekna tusiwe wafanyabishara but tukawa wakulima aseee.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom