Tuelimishane kuhusu Kilimo cha Pilipili Manga, kuanzia mbegu bora, magonjwa, utaalamu mpaka masoko

M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
151
Mwenye kujua hali ya hewa inayoruhusu hili zao kustawi na kuzaa kwa wingi tafadhali anijulishe.

Na ni sehemu gani Tanzania hili zao linastawishwa kwa wingi?

Asanteni


Katika kuabarishana fursa lukuki zilizoko kwenye maeneo tofauti tofauti ndani ya inchi yetu leo Muungwana Blog tunakuletea fursa ya kilimo katika zao la pilipili aina yab mtama (Pilipili Mtama) kwa lugha ya kingereza inajulikana kama black pepper.

Katika kuangalia fursa hii tutagusia maeneo yafuatayo:
  • Utangulizi,
  • Upandaji,
  • Uvunaji,
  • Masoko,
  • Hitimisho

UTANGULIZI
Pilipili mtama ni zao ambalo kitaalamu linajulikana kama Piper nigram ambalo asili yake ni upande wa mashariki ya mbali.Zao hili kwa lugha ya kingereza linajulikana kama BLACK PEPPER.

Yapo baadhi ya mikoa au maeneo watu wamekuwa wakijishughulisha na kilimo hichi lakini makala nyingi zinaonesha kuwa kilimo hichi kwa hapa Tanzania hulimwa kwa wingi Zanzibar na mkoani Tanga.

Aina hii ya pilipili imekuwa ikitumiwa zaidi kama kiungo kwenye vyakula mbalimbali hapa kwetu Tanzania na kwa inchi za wenzetu na kwa baadhi ya sehemu kubwa za mashariki ya mbali ni moja katika baadhi ya viungo vinavyofanya vyema sana kibiashara.

Labda kutokana na kuchangia katika mmengenyo wa chakula inapotumiwa kama kiungo katika chakula ndio sababu inafanya kiungo hichi kupendwa zaidi.

UPANDAJI
Ili kupanda zao hili ni lazima kuzingatia mambo kadhaa ili kuweza kupata mazao yakutosha.Mambo hayo ni kama:
  • Hali ya hewa,
  • Udongo,
  • Mbegu bora,
  • Mbolea,
  • Nafasi katika zoezi la upandaji.
  • Miti ya kusimika.
  • Mambo tajwa hapo juu ni lazma yazingatiwe ili kuhakikisha unapata mazao bora yanayokidhi mategemeo yako kibiashara na yanayoendana na malengo yako.
Hali ya hewa ya wastani wa nyuzi 24-26 ndio nyuzi joto zilizoshauriwa katika makala mbalimbali pia ikiwa na wastani wa mvua za mililita 1500 mpaka 2000 kwa mwaka.Pamoja na hali ya hewa inayokidhi ni lazma swala la udongo lihakikishwe limechekiwa .Udongo wenye rutuba na unaopitisha maji.

Tunashauri pia kuwa na utaratibu wa kupima udongo kwa wataalamu wanaotambuliwa ili kuweza kufahamu pH ya udongo wako ili kulinganisha na pH inayotakiwa kwaajili ya kilimo cha zao hili ambayo makala nyingi zinasema ni pH=6.5 .Pia zoezi hili litakusaidia kufahamu baadhi ya wadudu waharibifu wanaoweza kuwepo kwenye udongo ili kuja na njia madhubuti za kukinga kabla ya kuanza kilimo au wakati wa zoezi la ulimaji na hii itasaidia kupata mazao bora.Zoezi hili kama litakuwa ni la umwagiliaji unaweza pia kijiridhisha pia kwa kupima maji yako pia.

Katika kuchagua aina ya mbegu ni vyema kuwashirikisha maafisa/wataalamu wakilimo ili kuepusha kupata hasara kwa kutokuwa na uhakika lakini tofauti ya mbegu hizi huwa hata kwenye umbile la matunda.Lakini uchaguzi wa mbegu huzingatia mambo yafuatayo:
  • Urefu wa pingili na ukubwa wa majani,
  • Ufupi wa pingili na udogo wa majani.
Mbolea nalo ni swala muhimu hakikisha kupima udongo wako ili kujua aina ya mbolea itakayotumika pamoja na wingi/kiwango cha mbolea.Katika ulimwengu wa sasa nyakati za kubahatisha zimepita ni vyema kuzingatia taratibu za kilimo bora ili kupata mazao bora.

Katika zoezi la upandaji ni vyema kuhakikisha nafasi kati ya mche na mche inaanzia mita mbili mpaka tatu. Ni vyema pia kuandaa miti ya kusimika ili zao husika liweze kukua kwa kujizungusha kwenye miti husika.Ni vyema kuhakikisha zoezi la kupunguza majani linafanyika kila msimu ili kupunguza giza katika mimea.

Makala mbalimbali zinaeleza kuwa miche ikishafikia umri wa miezi 18 inapaswa kupunguzwa kwa kukatwa sehemu za juu za miche ili kusaidia matawi mengine yachipue kwa chini.Kiutaalamu wanashauri miche iwe na urefu wa mita tatu mpaka tatu na nusu.

UVUNAJI
Uhalisia wa kilimo hichi unaonesha maua ya kwanza hutokea baada ya miezi 24 yaani baada ya miaka miwili wastani tokea kupandwa.Na matunda yake hukomaa miezi tisa hadi kumi.Zoezi la uvunaji linaweza chukua mzunguko mitano mpaka sita.

Utafiti Muungwana Blog ulioufanya unaonesha endapo zao hili baada ya kuchumwa na kuweka kwenye chombo kisichopitisha hewa basi inaweza kukaa muda mrefu sana bila kuharibika.

MASOKO
Soko la fursa ya zao hili imezidi kukua kwa kasi sana na ndio maana inchi zinazozalisha kwa wingi zao hili kama Vietnam, Indonesia na India na kuchangia katika vyanzo vya ajira na pia katika kuchangia katika biashara mbalimbali zinazochangia katka uchumi.

Fursa ya masoko kwa zao hili bado ni kubwa sana kulinganisha na kiwango cha uzalishaji kilichoko kwa sasa hapa inchini.Masoko ya zao hili yapo kwa wingi hapa inchini kutokana na matumizi ya zao hili kama kiungo na pia soko lake lipo kubwa sana ichi za jirani na Tanzania na mashariki ya mbali.

HITIMISHO
Fursa hii bado ni fursa pana na nafasi kubwa kwa wale wote wanaopenda kilimo cha zao hili. Japokuwa kidunia bado tunaona wazalishaji wakubwa kwa sasa ni Brazil, India, Indonesia, Malyasia, na Sri Lanka ambao hizi ndizo zinazotambulika na jumuiya ya kimataifa ya IPC (International Pepper Community).

Inchi yetu bado ipo katika wazalishaji wadogo wa pilipili mtama kidunia. Bado uzalishaji mkubwa unaitajika kukidhi soko la ndani na kulenga soko la nje kwa lengo ya kutanua biashara yako na kufanya biashara kimataifa.

Nilichojifunza kuhusu Pilipili Manga

Wakuu kwema,

Nilisafiri kidogo kwenda maeneo ya Tanga maeneo ya Tongwe, Masimba, Zimbili kwa ajili ya kufatilia mazao ya viungo vya chakula.
Nimeona nishare na nyinyi vitu vichache ambavyo nimejifunza kuhuusa mazao ya viungo vya chakula. Kuna kipindi flani nilianzisha uzi kuhusu soko la pili pili Manga lakini sikupata jibu hivyo nikaona ni heri niende kwa wakulima kujua zaidi kuhusu Pili Pili Manga.

Pili pili Manga ni moja ya zao ambalo linauzwa kwa bei nzuri sana kwa muda sasa, hivi sasa bei ya pili pili Manga ikiwa kavu kule kwa wakulima kilo moja inaenda kwa shilingi 11,000 na huku Dar es salaam inaedna mpaka 18,000 japo sijaulizia kwenye masoko ya Kariakoo na mengine hio ni bei tu kwa wafanyabiashara wanao safirisha nje ya nchi.
Japo kuwa bei ni nzuri ila kuna shughuli kidogo ya kufanya ili uweze kufikia malengo.
Kabla ujaamua kuingia kwny zao hili ningependa ujue ya fuatayo:

- Uzito wa Pili pili Manga zikiwa mbichi na pale utakapokuja kuzikausha huwa zinapungua sana, ukikitua zimekoma ni ratio ya 3:1 na zikiwa mbichi inaweza kwenda hata kwa 10:1 hapa niki maanisha unapata kilo moja kwenye kilo tatu au kilo moja kwenye kilo 10. ina maana kama zimekoma ukanunua mbichi kilo 1000 ina maana utapata kavu kilo 300 au 350 inategemea na ukomavu wake. ila kama umepata mbichi unaweza pata kilo 150 au 200 kwny kilo 1000.
- Utajuaje kama Pili pili imekomaa au mbichi, ikiwa bado changa kwa shina lake lina kuwa na mapengo pia zile mbegu ukiziminya zinapasuka na kutoa uji mweupe. Ila ikiwa imekomaa ukiminya zile tunda za Pili pili Manga utatumia nguvu sana kuipasua unaweza ukaipasua au zingine zinaweza kukushinda kabisa kupasua, na kama ikipasuka kirahis haitatoa uji uji bali utapa kikokwa cha size ya gololi ndogo.

- Pili pili Manga ikiwa mbichi bei yake huanzia shilingi 1500 mpaka 2000 ila makubaliano ni ww na mwenye shamba mfano anaweza kukuuzia pili pili kwa shilinig 1500 ila wachumaji juu yako, wachumaji huchukua shilingi 300 kwa kilo moja au anaweza kukuuzia kilo kwa 2000 ila wachumaji juu yake wewe unakaa unasuburia mzigo tu.

- Angalizo wakulima huwa na longo longo sana na wanapandisha bei kila kukicha wakisikia jirani ameuza kilo 2500 basi wote watauza kwa 2500. mimi nilifika kilo inauzwa 2000 ila ndani ya siku 4 kilo iliuzwa 3700 wakulima wakiona wanunuzi wanakuja na kutaja makilo mengi mengi na wao hupandisha bei, pia wengine huamua kukuchumia pili pili ambazo hazijakomaa ili mradi wa wai soko.

- Kua makini na Pili pili ambazo zinalimwa maeneo ya milimani mara nyingi huwa hazikomai mapema ila huwa zinambegu kubwa zimeshiba yani ukiziaangalia kwa wasi wasi unaweza kuvutika na kuona biashara ndo hii ila kila ukitest utakuta zote ni changa.

- Kama unaweza kuingia shambani na kuangali mzigo kabla haujachumwa nalo sio jambo baya ila kama hutaweza wewe cha msingi ni kumwambia tu mkulima kuwa akileta changa huchukui maana wengine wakorofi anaweza kukuletea changa ukachukua alaf mwisho wa siku ukapata hasara wewe.

- Pili pili manga unaweza kuzihifadhi kwa muda mrefu kama tu utahakikisha zimekauka vizuri, Pili pili manga zinahitaji jua kali la siku mbili mfululizo ili ziwe kwenye ubora unaotakiwa. Kama utazihiifadhi kabla ya kukauka vizuri zitaweka ukungu na ni shida sana kuzirejesha kwenye ubora wake, ila pia unaweza zikausha kwa siku moja kama ukitaka kuziuza huko huko shambania uzito wake huwa bado uko juu kiasi flani. Pili Pili isipi kauka vizuri kama utaamua kuiweka ndani usubirie soko itaendelea kupungua uzito hivyo ni vyema kuhakikisha ina kauka vizuri ili kama unasafirisha au unaweka ndani kwa muda fulani uikute katika ubora ule ule. Pia tumia magunia ya mkonge sio ya manila kwa ajili ya kuhifadhia.

Nilichokiona kingine ni kuwa kama una mtaji wa kutosha unaweza kuchukua zikiwa kavu kwa bei itakayokuwepo ama unaweza fika kijijini ukaamua kuvuruga bei, mfano wanauza kilo 10,000 wewe labda una haraka na mzigo na mteja unaye tayari wewe unatangaza bei kuwa 11,000 kwa kilo au 10,500 kwa kilo unapata mzigo fasta sana. Changamoto ya kufata bei iliyopo itakufanya ukusanye mzigo mdogo mpaka kufikia lengo.

Ushuru- hili ni la kuzingatia usipo lipa ushuru kijijini kule jiandae kulipa ushuru muheza mjini na ushuru wake ni shilingi 300 kwa kilo. Kwa kijijini kule huchukua gunia moja kwa shilingi 5000 au elfu 10,000 inategemea na ukubwa wake.

Mazao mengine yanayopatika katika vijiji vya karibu ni Iliki ambayo ikiwa mbichi huuzwa kwa bei ya juu kabisa ni kilo moja 18,000 na ile ambayo utaikuta mkulima ameikausha inaenda mpaka 25,000 kwa kilo.

Mazao mengine ila sikufanikiwa kupewa details zaidi ni;
Mdalasani, cocoa, mchachai vyote hivi kilo 3000 mpaka 4000
Ushafirishaji ni changamoto kama una magunia machache ila kama una magunia mengi mafuso ni mengi sana unaweza ongea nao wakakufanyia bei nzuri ila mabasi pia yanabeba sema bei zao ziko juu wanaweza kuchukua 15,000 kwa gunia moja.

Soko la bidhaa hizi ni kubwa ila inabidi ulisaka haswa na uwe na connection nzuri, watanzania wengi wanapeleka Mombasa kule bei iko juu sana, sema wengi waligoma kuniambia kwa Mombasa bei ikoje waliishia tu kusema inalipa lakini hakuna aliyenipa jibu.
Wakulima ni wepesi sana kutoa taarifa zote kuhusu zao husika ila wafanyabiashara ni wagumu sana kukuelezea zao hili peleka sehemu flani bei iko vizuri. Bado naendelea kuuliza soko lake lakini kwa hali inavyoonyesha soko sio baya na ukiweza kuhifadhi mpaka kipindi ambacho zao linakuwa adimu kidogo bei yake huwa juu sana husasani tukielekea mwezi wa Ramadhani.

Wakulima walinipa ushirikiano wa kutosha sana kwa kila nilichouliza yani ndani ya siku moja nilikuwa nishajua kuna mazao gani na gani na wapi ya yanapatikana na bei zikoje na njia za kufika huko ila wafanyabiashara wengi niliokutana nao kila ukimuuliza kuhusu soko la Mombasa anaishia kukuambia tu inalipa sana.

Bado naendelea kujifunza juu ya haya mazao ila pia kama kuna mwenye uelewa zaidi na zaidi anaweza kushare hapa tuweze kujua kwa undani haswa kwenye swala la masoko ndani na nje.
 
mwenye kujua hali ya hewa inayoruhusu hili zao kustawi na kuzaa kwa wingi tafadhali anijulishe. Na ni sehemu gani Tanzania hili zao linastawishwa kwa wingi?
Asanteni

Pili pili hiyo inamea na kuzaa sana milima ya Matombo huko Mvomero. tatizo barabara ya kwenda hapo mlimani, ni mbaya sana siku mvua ikinyesha.
 

Jumuiya ya Wakulima wa Kilimo Hai Usambara Mashariki (JUWAKIHUMA) ni chama kinachounganisha vijiji sita vilivyopo milimani Usambara Mashariki wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.

Wakulima wa maeneo haya wanalima sana mazao ya viungo vya chakula hasa pilipili mtama, iliki na karafuu. Karafuu inayolimwa eneo hili ubora wake ni mkubwa kuliko karafuu inayolimwa Pemba na Unguja. Pia eneo hili yapo mashamba makubwa ya serikali ya miti ya mipira, iliyokuwa inatumika kama malighafi kwa kiwanda cha matairi cha General Tyre, Arusha.

Pilipili mtama ndilo zao la kwanza nchini lenye bei nzuri kwenye soko la ndani, bei yake kwa sasa ni kati ya shilingi 400,000/= hadi 600,000/= kwa gunia la kilo 100, sokoni Kariakoo.

Serikali ya Marekani kupitia shirika lake la misaada la USAID limewasaidia sana wakulima wa vijiji hivi sita, kuendeleza mazao yao, kiasi kwamba hali ya maisha ya wakulima imebadilika sana, na kila eneo utakalopita utakuta wakulima wanapanua mashamba na vitalu vya miche mbalimbali vikiwa mashambani, vikisubiri msimu wa kupanda.


https://lh3.googleusercontent.com/-f5DbakWscH8/Sq-VJDcPeII/AAAAAAAAO2E/_CMOVEuT4gI/s800/P1020187.JPG


https://lh6.googleusercontent.com/-RwmEeWtO59c/Sq-VMfTJ5oI/AAAAAAAAO2Q/CdZHm0UYOW0/s800/P1060002.JPG


https://lh6.googleusercontent.com/-I_huoY_M6Vk/Sq-VKarFQuI/AAAAAAAAO2I/cr4l1zb9pww/s800/P1020195.JPG
 
Mrdash1 umenichekesha sana..............umenikumbusha mara ya kwanza kulisikia jina hili likitamkwa na watu wazima nilipata wakati mgumu kidogo.

Tukirudi kwenye maada ni maeneo managapi nchini zao hili linaweza kustawishwa?
 
Mimi ni mfanyabiashara mkubwa wa pilipili manga ila kikwazo kinachokwamisha biashara hii hapa kwetu Tanzania hamna soko la uhakika.

Kama kuna mtu yupo tayari na aina hii ya viungo basi tuonane tufanye biashara!

0712720080 au +254721207560
 
Wadau jamvini habari zenu?

Kwa yeyeto mwenye kujua hivi vitu vinatoka mkoa gani kwa wingi? Maana nahitaji kwa wingi (tons) au kwa mtu mwenye kuweza kusupply kwa wingi tuwasiliane kwa maelezo zaidi.
 
Wadau jamvini habari zenu??
Kwa yeyeto mwenye kujua hivi vitu vinatoka mkoa gani kwa wingi? Maana nahitaji kwa wingi (tons) au kwa mtu mwenye kuweza kusupply kwa wingi tuwasiliane kwa maelezo zaidi.

Call:

0784 887 599
0784 422 571
0713 769 379
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom