TUCTA yamvaa Makonda kwa udhalilishaji wa Wafanyakazi

Hao ndo wanapenda mfumo wa kuabudiana uendelee. Yaani unakuwa na watumishi wazembe kama wale halafu unataka walelewe....Watanzania bwana hawajui wanataka nini.
Mkuu umeajiriwa au umejiajiri? Vipi umechelewa mara ngapi kufika kituo chako cha kazi? Makonda angekusweka ndani mara ngapi?
 
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limelaani watendaji wa Serikali katika ngazi mbalimbali kuwakandamiza na kuwadhalilisha wafanyakazi kwa kisingizio cha kaulimbiu ya Rais John Magufuli ya ?Hapa Kazi Tu?.

Akitoa tamko hilo Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Hezron Kaaya alisema hivi karibuni vimeibuka vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji dhidi ya wafanyakazi hususan wa serikalini, jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za kazi.

Alisema watendaji hao wakiwamo wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na viongozi wengine wamekuwa wakitoa vitisho na kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji wafanyakazi walio chini yao kwa madai ya kutekeleza agizo la kufanya kazi.

Akitolea mfano tukio la hivi karibuni la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuwaweka ndani kwa saa sita maofisa ardhi waliochelewa kufika katika eneo la kazi kama ilivyotakiwa.

Alisema kitendo cha kuwaweka ndani wafanyakazi hao ni kinyume na haki za binadamu kwani walistahili kuwajibishwa kwa utovu wa nidhamu si kuswekwa mahabusu.

?Kosa walilofanya ilikuwa ni utovu wa nidhamu kazini, hivyo walipaswa kuadhibiwa kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kazi siyo kuwadhalilisha namna ile, ndiyo maana tunamtaka Makonda kuomba radhi.

Kaaya aligusia pia na suala la wafanyakazi wa mkoa wa Kilimanjaro kuzuiwa kwenda likizo na kudai kuwa agizo hilo ni kinyume na taratibu za kazi.

Mkuu hizi porojo zako zina mshiko kiasi. Kwa taarifa yako hizo njia pendekezwa ndio sahihi lakini hazijawahi kuleta tija yeyote.

Makonda ni tatizo na simuungi mkono.

Lakini pia hatuwezi kuleana na kubembelazana hapa kama PIMBI.

Pale inapobidi DRILL lazima itumike.

Selema selema alija..!!
 
Kwa jinsi nilivyoona ile move, mimi nigewaweka masaa kumi na mbili, nchi hii tumefika hapa tulipo kwa sababu ya kufanyakazi kwa mazoea, kulindana, tukijifanya tunajua sheria na kujitetea sana ili kupoteza muda mwingi katika hali hiyo, wakati mwingine tukitunga sababu za uongo uongo.
Haiwezekani wananchi wote hao mpaka mkuu wa wilaya wamefika nyie tuliowajiri kwa kodi zetu na magari yetu ili mtutumikie mnajifanya wajuaji kiasi hicho. Mimi nafikiri wangefukuzwa tu mbona vijana wengi wanamaliza chuo hawana kazi, tukae tunahangaika kubembeleza watu wawili. Hapana bwana!!!!!! Ifike mahali tusiruhusu kufikiri kama jana kila wakati!!!!!!
 
halafu hao tucta badaka watetee wafanyakazi wasolipwa haki zao makazini wao wanaleta mambo ya ajabu.
makonda wachape
Pamoja na huko kulaani kitendo hicho ndiyo kutetea kwenyewe! Sheria haziko holela kihivyo, inamaana nayeye Makonda akichelewa atangulie mwenyewe Lupango?
 
Kwa jinsi nilivyoona ile move, mimi nigewaweka masaa kumi na mbili, nchi hii tumefika hapa tulipo kwa sababu ya kufanyakazi kwa mazoea, kulindana, tukijifanya tunajua sheria na kujitetea sana ili kupoteza muda mwingi katika hali hiyo, wakati mwingine tukitunga sababu za uongo uongo.
Haiwezekani wananchi wote hao mpaka mkuu wa wilaya wamefika nyie tuliowajiri kwa kodi zetu na magari yetu ili mtutumikie mnajifanya wajuaji kiasi hicho. Mimi nafikiri wangefukuzwa tu mbona vijana wengi wanamaliza chuo hawana kazi, tukae tunahangaika kubembeleza watu wawili. Hapana bwana!!!!!! Ifike mahali tusiruhusu kufikiri kama jana kila wakati!!!!!!

Kama ni rahisi kwa jinsi unavyofikiria si kubadirisha tu sheria na kanuni za kazi! ushabiki mwingine hata hauna maana!
 
haohao Tukta ndio wamesababisha watumishi wa umma kulewa madaraka na kufisadi mabilioni ya fedha na ukwepaji wa kodi, kwa tabia yao ya utetezi tuu usio na tija,. tukta acheni ujinga huu Tanzania haiwezi kuendelea kwa kutetea ujinga huu. tupo nyuma sana kimaendeleo wacha watu wanyooshwe kwanza. warudi kwwnye mstari. imagine hivi sasa asilimia 35 ya watumishi wa umma wameambukizwa tabia ya kifisadi. tulieni! !!
 
Watanganyika kweli vigeugeu, Mara hii mmegeuka??? Mlimsifia sana makonda imekuaje tena??? Acheni unafiki
 
makonda bado anamwota kikwete na ritz huyu ni Magufuri haangalii uso wa mbuzi hata siku moja.
 
viongozi wakilegeza buti tunawaita lege lege,wakikaza buti tunawaita wadhalilishaji,it is high time that we be sure of what we real need and stop calling them names.Tuache kulialia tujipange.
 
Kuna mtu mmoja anadai mambo ya sheria tuyaweke pembeni!!! Ana akili timamu huyu? Yaani tuishi kiholela bila kufuata sheria. Aisee ni umburula uliopitiliza. Kama mama au dada au ndugu yako akibakwa utasema sheria isifanye kazi. Huu ni moja ya mchango wa hovyo kabisa!
 
Hapa kazi ni lazima , mapungufu madogo madogo ni ya kurekebishana na kusameheana, lakini inchi hii ilikuwa inataka mbabe ili watu wanyooke. Sasa hizo ni side effects za hapa kazi tu
 
hizo ni side effect za hapa kazi tu lakini watu wateelewa polepole, ni mambo ya kuvumiliana tu.
 
Mkuu umeajiriwa au umejiajiri? Vipi umechelewa mara ngapi kufika kituo chako cha kazi? Makonda angekusweka ndani mara ngapi?

Naomba Mkuu kwa niaba ya MKuu SAIZI YANGU nikujibu kama ifuatavyo:

Nimeajiriwa serikalini, muda wa kufika kazini ni saa 1:30 na kuondoka kazini ni saa 9:30 (Kanuni F.1(1) ya Kanuni za Kudumu 2009). Masaa 8 ya kazi huwa nayatumia kwa kazi za mwajiri tu. Nikipanga au kupangiwa ratiba huwa ninaifuata bila kusukumwa wala kufuatwafuatwa na kiongozi wangu.

Kwa mwenendo wangu huu, Makonda asingenisweka ndani hata siku moja!

Go go go Makonda, watumishi mizigo ni lazima watupishe maana #Hapakazitu , #Hereworkonly , #Haimbombotu, #Henahamilimoduhu.
 
Maswali yangu mawili kwa kaka YANGU PAUL ....

NILICHAMBUA ORALLY JUU YA FASILI YA KAULI MBIU ya Mh. Rais
###HAPA KAZI TU... Katika kuhamasisha Weledi na Ufanisi Kwa wananchi na Viongoz kwa ujumla katika kutuletea maendeleo nchini .... ......

Kama Trade Unionist (nadeclare interst )

Video hiyo inanizalishia maswali mawili makubwa ya kutafakari kwa kaka Paul ..

1. Alifanya mawasiliano nao akajua kipi kiliwasibu kabla ya kuwahukumu??
(Nb, kama ndio ingekuwa ndio suala la kwanza kujibu kwenye mahojiano yake Kuwa walichelewa kwa sababu hizi ambazo sio za msingi)

2. Sheria na KANUNI za utumishi wa UMMA zinaeleza nini..... Endapo MTUMISH akichelewa.... Kazini au kikaoni.....

Kuna kitabu kizuri kinachoelezea... Nyerere na Ujamaa nacho kina kichwa "NYERERE WAS NOT DEFEATED BUT BETRAYED "

Kilielezea namna ambavyo... Mwalimu hakushindwa KUTEKELEZA sera ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA Ila alisalitiwa na Viongoz wa chini ambao walishindwa kuwaelewesha wananchi juu ya sera hiyo.... Pia usaliti wa Viongoz kujilimbikizia Mali za Jamii badala ya kuzitumia kwa mijibu wa KANUNI .....

MAANA YANGU ;
Naipenda SANA KAULI MBIU ya Mh. Dr. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia naamini ni Kauli MBIU STAHIKI kwa wakati tulionao... Kwani suala la utendaji kwa watumishi wa UMMA lilikuwa changamoto..... Kwa Kila idara Kuwa na kero na Ufanisi mdogo.

Ili Kauli MBIU hiyo isijepwaya au kuleta NEGATIVE IMPACT kwa jamii, Viongoz na Watendaji ni vizuri Kila mmoja akatekeleza Kauli mbiu hiyo kwa umakini mkubwa..... Huku tukifuata Sheria, kanuni, Taratibu na Busara ..

Kaka Paul Kuna umuhimu ujisahihishe (wazo ambalo Mwalimu Nyerere alisisitiza mara Viongoz wanapoteleza )

Pia ni vizuri kwa Viongoz wengine kutafakari kwa kina kabla ya kuchukua hatua katika maeneo yetu (TO ADHERE POSITIVISM IDEOLOGY after digesting the matter accordingly )

#Team#PasuaMajipu#

Ibrambeya@gmail.com
 
Hapa kazi ni lazima , mapungufu madogo madogo ni ya kurekebishana na kusameheana, lakini inchi hii ilikuwa inataka mbabe ili watu wanyooke. Sasa hizo ni side effects za hapa kazi tu

Hata quinine ni chungu: husababisha kichefuchefu, kutapika, kizunguzungu n.k. lakini ndiyo dawa pekee inayoweza kumaliza homa ya malaria, maadam mtu akiugua malaria kali ni sharti quinine itumike licha ya side effects zake.
 
Naomba Mkuu kwa niaba ya MKuu SAIZI YANGU nikujibu kama ifuatavyo:

Nimeajiriwa serikalini, muda wa kufika kazini ni saa 1:30 na kuondoka kazini ni saa 9:30 (Kanuni F.1(1) ya Kanuni za Kudumu 2009). Masaa 8 ya kazi huwa nayatumia kwa kazi za mwajiri tu. Nikipanga au kupangiwa ratiba huwa ninaifuata bila kusukumwa wala kufuatwafuatwa na kiongozi wangu.

Kwa mwenendo wangu huu, Makonda asingenisweka ndani hata siku moja!

Go go go Makonda, watumishi mizigo ni lazima watupishe maana #Hapakazitu , #Hereworkonly , #Haimbombotu, #Henahamilimoduhu.

Mkuu heshima mbele. Umenijibu saa ngapi hii msg? Naona saa saba na dk 32 mchana. Je, hii ni sehemu ya kazi ulizopangiwa na serikali? Tuwe wakweli basi. Sio kukariri vifungu, kama hivyo chini vya biblia.
 
Mkuu Ozzie kumbuka kuwa mtumishi ana siku 28 kila mwaka za kupumzika (likizo). Sasa hivi Mkuu niko likizo hivyo niko nje ya majukumu ya mwajiri wangu. Asante sana kwa udadisi wako. Tuchape kazi tuache uvivu, uzembe na visingizio.

#Hapakazitu , #Hereworkonly , #Haimbombotu, #Henahamilimoduhu.
 
Back
Top Bottom