Tucta wamtaka rais Kikwete kuvunja bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tucta wamtaka rais Kikwete kuvunja bunge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Technician, Jan 19, 2012.

 1. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [FONT=&amp] TUCTA WAMTAKA RAIS KIKWETE KUVUNJA BUNGE [/FONT]

  [FONT=&amp]CHAMA cha Wafanyakazi nchini (TUCTA), kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mdai kwamba limeshindwa kusimamia na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Umma, badala yake Bunge limegeuka kuwa kinara wa kuidhinisha matumizi makubwa ikiwa ni pamoja na posho kubwa kubwa kwa vigogo Serikalini.[/FONT]

  [FONT=&amp]TUCTA imesema, Wabunge wa Bunge la sasa wanaonekana kujali zaidi maslahi yao binafsi, badala ya Watanzania na maendeleo ya taifa kwa ujumla, hivyo chombo hicho kimepoteza sifa ya kuwa mhimili mkuu wa nchi, kwani kimeonekana dhahiri shahiri kushindwa kabisa kuisimamia Serikali kwa mujibu wa sheria za nchi, hivyo Rais hana budi kulivunja na kuitisha Uchaguzi mwingine.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mwandishi wa mtandao huu kutoka Jijini Mwanza, Sitta Tumma anaripoti kwamba; Kauli hiyo imetolewa hii leo Jijini Mwanza na Katibu wa TUCTA Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Mwendwa, wakati alipokuwa akizungumzia na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake kuhusu mwenendo wa Bunge na mstakabali maendeleo ya taifa na wananchi wake.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kwa mujibu wa Mwendwa, wabunge wengi waliopo Bungeni wanaonekana kuwa na lengo la kuwatalawa wananchi wao, na si kuwahudumia na kuwasilisha mawazo yao katika chombo hicho, na kwamba wamekuwa vinara wakubwa wa kuidhinisha matumizi makubwa ya posho zao na vigogo wengine waliopo katika taasisi na Wizara mbali mbali.[/FONT]

  [FONT=&amp]"Tanzania ya leo ipo kwenye wakati mbaya sana. Bunge limeshindwa kabisa kuisimamia Serikali juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma, badala yake limegeuka kuwa chombo cha kuidhinisha matumizi makubwa posho zao na vigogo wengine Serikalini.[/FONT]

  [FONT=&amp]"Wabunge wengi wanaonekana wapo kwa ajili ya maslahi yao bungeni. Hawawajali kabisa wananchi waliowachagua....hivyo tunamuomba sana Rais Kikwete ni bora alivunje hili Bunge maana Watanzania hawatapona kwa mtindo huu wa posho ya 200,000", alisema Katibu huyo wa TUCTA Mkoa wa Mwanza.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mwendwa ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti nchini (RAAWU), Kanda ya Ziwa alikwenda mbali zaidi na kusema: "Kwa sasa Bunge linaonekana kumtumikia kafiri ndiyo maana wameshindwa kuidhibiti Serikali kwa sababu nao wanajali zaidi maslahi yao binafsi".[/FONT]

  [FONT=&amp]Alisema, wapo baadhi ya wabunge ni wajumbe wa bodi za taasisi au idara fulani zaidi ya tano, na kwamba kwa hali hiyo wamekuwa wakiwaza vikao tu ili walipane posho, na alitoa angalizo kwa wabunge kuacha mara moja kujipendelea wao wenyewe, bali waishinikize serikali iwalipe mishahara mikuwa watumishi wa Serikali na si kama ilivyo hivi sasa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Akizungumza kwa kujiamini, Mwendwa alisema nchi yoyote duniani ikiwa na wezi kamwe wananchi wala taifa halitapata maendeleo, na kwamba inavyoonekana hata Rais wa nchi ameshindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria za nchi, hivyo taifa la Tanzania linakabiliwa na ombwe la uongozi na inatakiwa Katiba mpya haraka iwezekanavyo.[/FONT]

  [FONT=&amp]"Tumeona Rais Kikwete ameshindwa hata kutoa ufafanuzi wa kama ameidhinisha posho za wabunge sh. 200,000 kwa siku kama ambavyo wanalipwa sasa. Yupo kimya wakati wananchi wake wakimlilia. Kwa hali hii ni dhahiri ameshindwa kutekeleza kabisa majukumu yake", alisema Katibu huyo wa TUCTA Mkoa wa Mwanza.[/FONT]

  [FONT=&amp]Hata hivyo, Mwendwa alitumia fursa hiyo kumpongeza Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa kueleza ukweli kupitia habari iliyoandikwa na Tanznaia Daima ya leo, juu ya hali halisi ya nchi na matumizi makubwa ya fedha za walipakodi, na kwamba hoja ya kiongozi huyo inatakiwa kuungwa mkono maana ni ya kizalendo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Aliitaka pia Serikali kusikiliza kilio cha wafanyakazi wake, ikiwa ni pamoja na kuwaongezea mishahara na marupurupu, na kusema madakrati, walimu, askari polisi, watumishi wa kawaida na hata maofisa kilimo na mifufugo wanalipwa ujira kidogo sana ikilinganishwa na kazi kubwa wanazozifanya kila siku.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mwisho.[/FONT]
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Alishawaambia hataki kura za wafanyakazi sasa mnahitaji nini tena?
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wafanyakazi hao ndo wanasubiri uchaguzi ukifika wakawe wasimamizi wa vituo vya kupiga kura, na wakati huo wa kura wanasahau matatizo yao ya miaka yote na kuwaza tu posho za usimamizi wa kura!
   
 4. FuturePresident

  FuturePresident JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 322
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii posho ya 200 k ukiitizama vizuri ni kama rushwa vile kwa hawa jamaaaa....ili wasitimize wajibu wao.....wachape usingizi vizuri ndani ya mjengo na kupiga madesk tuuu.....kila kitu kiwe....ndiyoooooo......wangapi wameafiki ndiyoooooo.....!!!!! ha ha ha ha ha ha ..Bongo... du, Mungu wa mbinguni tusaidie.....hivi hivi hawajamaa watatuuua
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Alisema hataki kur zenu n mlimpa n kusimmi kur zake na bado kawatosa kwa sababu aliwahidi kuwa hawapendi........sasa fanyeni kingine sio kumlilia yuleyule aliyeema hawataki.............
  Lakini kikwete ni rais msikivu sana n ndiyo maana akisikia msiba lazima aende.....akisikia kun wawekezaji marekani hata akiambiwa saa moja asubuhi anaondoka muda huo huo kwa kuwa tu ni msikivu sana,,,,,,kwa usikivu wake huo bila shaka atavunja bunge
   
 6. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,171
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  intelegensia ya bunge ikinasa tu, watamuwahi yeye!
   
 7. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  TUCTA kwani KIKWETE anawafahamu? mnampigia mbuzi ngoma acheze? wabunge walipima upepo wakaona yeye kila siku MAREKANI wenyewe ndo wahangaike ikabidi wajipandishie mahela ya kutosha kwani umeona yeye mpaka leo kashatoa kauli yoyote kuhusu posho? kimsingi TUCTA na myie km mtaweza ni kudai ata posho km za wabunge tena iwe kila siku mfanyakazi anapoenda kazini nadhani apo itafaha kwa wote....tatizo lenu nyie TUCTA mnanunuliwa kiurahisi hasa viongozi wenu wa juu yani siku hizi ndo hawapo kabisaaa ukiachilia ugumu wa maisha unaowakumba wafanyakazi....NIGERIA, SOUTH AFRICA mbona wanaweza kwanini nyie TUCTA zero always?
   
 8. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  angalau TUCTA wametoa tamko, kuliko kukaa kimya tu.
  Its better than nothing mazee...
   
 9. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Lol!! umenikumbusha nilikuwa nimesha sahau
  anadharau huyu ******
   
Loading...