kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,687
Eti! Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limesema halitatasita kuchukua hatua zaidi kwa Serikali kama itaendelea kupuuza madai mbalimbali ya wafanyakazi. Alisema hayo jana' Rais wa shirikisho hilo Bw. Omar Juma, na kusisitiza kuwa hivi sasa hawapo tayari kurudi nyuma kwani wamepata uzoefu wa kutosha. Alisema kuwa TUCTA inataka Serikali iongeze mishahara ya wafanyakazi ktk sekta ya umma kwa asilimia 100% ili waweze kumudu gharama za maisha. Pia alisema kuwa wanataka serikali ichukue hatua madhubuti za kuhakikisha mfumuko wa bei unakuwa chini ya 10% kabla ya April 2013. Pia amesema mishahara na marupurupu kwa sekta binafsi yatangazwe kabla ya April 2013 na KUPUNZA KODI YA MAPATO YA AJIRA NA KUFIKIA KIWANGO KISICHOZIDI ASILIMIA 11%. Na amesema kuwa Serikali iweke wazi mikakati ya kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira badala ya kuendeleza porojo za kupeana matumaini. Source by: majira jumatano. My take: Je kweli TUCTA ina nia ya dhati na madhubuti kuwa tetea na kuwasaidia wafanyakazi watanzania ambao wamekuwa wakikandamizwa kwa muda mrefu miaka nenda rudi? au nao ni porojo tu?