kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,687
Katibu Mkuu wa Tucta,Nicholaus Mgaya.
Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi (Tucta) limesema kitapaleka kilio chao cha kima cha mshahara kiwe angalao 720,000 kwa ajili ya kukidhi maisha ya sasa kwa mujibu wa utafiti walioufanya.
Aidha, limesema kilio hicho kitaililia serikali katika Sikukuu ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei mosi mwaka huu na kwamba kero ambazo bado zinawakabili wafanyakazi nchini ni mishahara duni, kodi kubwa na kiwango kidogo cha pesheni.
Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholaus Mgaya, alipokuwa akizungumza na NIPASHE kuhusiana na maandalizi ya Mei Mosi mwaka huu.
Alisema sherehe hizo kitaifa zitafanyika Jijini Dar es Salaam na Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uwanja wa Uhuru.
Mgaya alisema kauli mbiu mwaka huu ni ¡®Utawala bora utumike kutatoa kero za wafanyakazi.
CHANZO: NIPASHE
my take:
*Kwa kauli hii, kwa uongozi wa sasa wa Tucta ni sawa usemi umesemao "maneno matupu hayavunji mfupa"
AU
*Ni sawa na usemi usemao "Kelele za chura..."