Tucta sasa yataka kima cha chini kiwe Sh. 720,000

Tucta sasa yataka kima cha chini kiwe Sh. 720,000

Day pipe dream. wapewe hizo mafisadi tutaiba nini ? au wana vyanzo vyao ??????
 
MGAYA hana kosa lolote na kawapigania sana wafanyakazi na ata migomo kaiandaa tatizo ni nyie watumishi wenyewe ndo mnao mlet down...Na pia kafanya kazi na mwajiri Msanii anekimbilia mahakamani na bado mahakama iliamuru serikali ikae chini iongee na TUCTA lakini iligoma sasa yeye MGAYA ndo agome pekee ake? serikali hii kwanza mufilisi na full usanii
 
Tucta hawana lolote

Tantalila tu

Wanakula bure michango ya wanachama wao
 
Mambo mengine yanayoongelewa hayatekelezeki mojawapo ni hili pendekezo la hawa jamaa. Huu ni upuuzi kwa kuwa kuna haja gani ya kudai jambo ambalo unajua fika kuwa halitawezekana?
 
MGAYA hana kosa lolote na kawapigania sana wafanyakazi na ata migomo kaiandaa tatizo ni nyie watumishi wenyewe ndo mnao mlet down...Na pia kafanya kazi na mwajiri Msanii anekimbilia mahakamani na bado mahakama iliamuru serikali ikae chini iongee na TUCTA lakini iligoma sasa yeye MGAYA ndo agome pekee ake? serikali hii kwanza mufilisi na full usanii

Sasa kima cha chini ndo iwe laki saba
 
Poleni. Ni ndoto tu hizo tena kuelekea mwaka wa uchaguzi. Zile 350,000 hadi leo wameshapata kiwango hicho? wako busy na mishahara na posho za waheshimiwa!!!
 
Kila ikifika mei mosi ndo wanajifanya kupigania maslahi ya wafanyakazi.



Siku 364 wanafanya nini ofisini?

sio wanajifanya, wanapigania, kwanza kwa nini wapiganie? waajiri wanatakiwa watoe maslahi stahiki kwa waajiriwa, ila hawatoi lakini yanamwisho "Kuli"
 
Wakati Rais Jakaya Kikwete
akitarajiwa kuhutubia wafanyakazi
katika kilele cha Siku ya
Wafanyakazi (Mei Mosi) kwenye
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam,
Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi (Tucta), limeitaka
Serikali kupandisha kima cha chini
hadi kufikia Sh750,000.
Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolas
Mgaya alisema jana kuwa
wanahitaji kuona wafanyakazi
wakipata kiwango cha mshahara
kinachokidhi mahitaji.
Alisema kutokana na kushuka kwa
thamani ya shilingi na mfumuko
mkubwa wa bei uliopo kwa sasa,
kiwango hicho angalau kinaweza
kukidhi mahitaji muhimu ya
wafanyakazi wa kima cha chini,
ikiwamo malazi, mavazi, chakula na
mahitaji ya afya.
“Katika hali halisi, tunaona namna
bei za vitu muhimu ikiwamo
umeme, maji, mafuta, gharama za
vifaa vya ujenzi, nyumba vyakula na
gharama nyingine za maisha
zimekuwa zikipanda maradufu
katika miaka ya karibuni, lakini
hakuna namna inayofanyika kuleta
unafuu kwa wafanyakazi.
Kimsingi kima cha chini lazima
kiongezwe ili kikidhi mahitaji ya
maisha ya wakati huu,” alisema.
 
Back
Top Bottom