beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA, Said Wamba amesema Wafanyakazi hapa Nchini hawajaongezewa Mishahara kwa miaka 8 kwa upande wa Sekta isiyo rasmi na miaka 6 kwa Sekta ya Umma
Amesema, "Hali hii imesababisha kupungua kwa ari ya kazi na hivyo kupunguza ufanisi ya uwajibikaji mahali pa kazi. Gharama za maisha zimezidi kupanda ilihali stahiki na ujira zimeendelea kuwa duni"
Ameeleza hayo katika Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi. Kaulimbiu ya mwaka 2021 ni "Maslahi Bora, Mishahara Juu, Kazi Iendelee"