TUCTA la pensheni sawa, geukieni bodi ya mikopo(HESLB) sasa

Maguli lii

Member
Nov 19, 2018
26
10
Hongereni sana kwa umoja wa wafanyakazi kupigania suala la pensheni kwa watumishi wote wa umma na binafsi, japo mapambano ni mabichi sana lakini kimsingi nawapongeza mliopofikia.

Nirudi ktk mada yangu sasa, Tangu kuasisiwa makato ya moja kwa moja toka mishahara ama mtu kupeleka mwenyewe mkononi kumewapo na malalamiko kadhaa.
1.KIASI KIKUBWA CHA RIBA HADI KUFIKIA KUWA MARA MBILI... mfano binafsi nimesomea 5,583,000 Lakini bodi imenizidishia hadi kufikia 11,587,000.....


Kimsingi hatukatai kulipa, lakini tulipe kwa haki si kuzidishiwa deni mara mbili zaidi hii si haki ikizingatiwa tu waajiriwa wa serikali na binafsi na hivyo kuathiri vipato vyetu, sisi ni watoa huduma kimsingi haipendezi kabisa.

Hili nalo la kulipa as you earn ni zuri sana tunaliunga mkono kwasababu linatupunguzia miezi ya makato hivyo kumaliza deni mapema zaidi.

2.Hili la detention lifuatiliwe kwa undani... deni linasoma mfano 10,000,000 limekatwa hadi kuisha, lakini ukienda bodi kuchukua certificate of clearance unakuta deni pia yaani kwa kila mwaka kadri unavyochelewa kulipa, deni linaongezeka kwa kiasi cha tsh 600,000 sasa hii si haki, bodi imejiwekea kanuni komezi kwa wakopaji hili halikubariki katu.

3.Inapotokea mtu umelipa deni lako lote ingepaswa deni liondolewe ktk salary slip yangu na muwekaji ambaye ni bodi yenyewe, sasa ni kinyume kabisa, unalipa deni lote lkn inakubidi mlipaji tena uende utumishi wilayani baada ya hapo kama halijaondolewa ina kulazimu upande basi hadi Dodoma utumishi... Hii si haki, mnatuonea watumishi wenu wa serikali.

Ndiyo maana natoa wito kwa TUCTA kulifahamu hili huenda vyombo vingine na Raisi wetu mpendwa halijui linavyofanywa na watumishi wake wa bodi hii ya mikopo... naomba sana lifuatiliwe na ikiwezekana Rais ajuzwe huu ni uonevu mkubwa sana.

NATOA WITO KWA VYAMA VYA WAFANYAKAZI KUUNGANA PIA KWENYE HILI LASIVYO BODI YA MIKOPO HAWATOKI LEO WALA KESHO KWENYE SLIP ZETU HATA DENI LIISHE WATAENDELEA KUDAI TU.

SHIME TUUNGANE KWA PAMOJA
UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI MWIKO
 
Na,zaidi ya yote kunauwezekano hiyo dentetion fee inaishia mifukoni mwao(watumishi wa bodi) .. Suala hili lifanyiwe uchunguzi wa kina.... Hawa watu wanawaumiza sana watumishi..
Naunga mkono hoja
 
Na,zaidi ya yote kunauwezekano hiyo dentetion fee inaishia mifukoni mwao(watumishi wa bodi) .. Suala hili lifanyiwe uchunguzi wa kina.... Hawa watu wanawaumiza sana watumishi..
Naunga mkono hoja
 
Suala la pensheni bado kwa namna moja au nyingine. Pamoja na Mhe. Rais kurudisha kanuni za zamani kwa kila mfuko haimaanishi wastaafu wote wa mifuko yote watafaidi 50% wapo wale wenzetu wa nssf na ppf ambao walianza kulalamika kabla ya kanuni mpya. Wao walikuwa wanapewa 25%, wamerudishwa kule mwanzo badala ya kuwasogeza kama TUCTA walivyoshauri. Hivyo bado wanatakiwa kutetewa zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FAO LA kujitoa

Kwa nini hawaongelei FAO LA kujitoa

Tucta hawana taarifa na kanuni mbaya za FAO LA kukosa ajira? Mojawapo ni kuwa ukiresign hupati haki yoyete

Pili...hakuna malipo ya mkupuo
 
Back
Top Bottom