TUCTA kujadili kima cha chini cha mshahara 2019

BARAZA Kuu la Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (Tucta) linatarajia kukutana Aprili 2, 2019 ambapo pamoja na mambo mengine, litajadili mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara.

Akizungumza na gazeti hili Jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alisema kuwa, baraza hilo pia litajadili maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya ambapo Rais, Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Alisema kwa sasa Kamati maalumu ya kushughulikia mishahara iliweza kufanya utafiti kuhusiana na hali halisi ya maisha kwa sasa, kima cha chini cha mishahara wanaopata wafanyakazi, gharama za pango na matumizi mengine ili waweze kuleta mapendekezo yao.

“Kuna kamati maalumu ya mishahara ambayo ipo kwa mujibu wa katiba yetu, inafanya kazi ya kuangalia hali halisi ya maisha ya wafanyakazi kwa sasa, kima cha chini cha mshahara wanaopata, gharama za pango na nauli na matumizi mengine wanayokumbana nayo, wanatarajia kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika Aprili 2 mwaka huu,” alisema Nyamhokya.

Aliongeza, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo, wataweza kuangalia kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta zote binafsi na serikali ili waweze kuwasilisha mapendekezo yao kwa Rais Magufuli siku ya wafanyakazi.

Alisema, mpaka sasa, wafanyakazi wanapata kiasi kidogo cha mishahara ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya kila siku ukilinganisha na kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema licha ya kuwasilisha mapendekezo ya kuiomba serikali kuongeza kima cha chini cha mshahara ili uweze kufikia 750,000 kwa wafanyakazi wa serikali, lakini mpaka sasa bado wanapokea Sh 375,000.

“Wafanyakazi wa serikali wanapata kima cha chini cha mshahara kuanzia Sh 375,000 na kuendelea, huku sekta binafsi wakipata kuanzia Sh 100,000 kwa mwezi kulingana na ofisi anayofanyia kazi,” alisema.

Aliongeza, kiasi hicho ni kidogo na kwamba hakiwezi kukidhi gharama za maisha, jambo ambalo limechangia kujitokeza kwa malalamiko ya kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema, lakini pia wameiomba serikali kupunguza gharama za kodi inayokatwa kwenye mishahara yao ambayo imekua kero ya muda mrefu, jambo ambalo litasaidia kumpunguzia mzigo mfanyakazi kutokana na hali ngumu ya maisha.

http://mtanzania.co.tz/tucta-kujadili-kima-cha-chini-cha-mshahara/amp/
Tunachotaka ni madaraja wala si kima cha China, naona TuCTa IPO kimya kama vile haihusiki. Ndiyo maana nilishakataa kukatwa hela yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi folio by a posho,mshahara mdogo ni vingi sana chamsingi tutafte fursa tupige kazi maisha yanaendelea

Sent from my SM-J810F using Tapatalk
Mbona upolisi mwingi kk
'Folio B' inatuhusu vipi sisi walimu!!
Au 'upele' haujakamilika mkuu, wamuwaza 'folio B'

5/5
 
Tutajilipa tu ,yeye aache tu kutupandishia mshahara.
 
nadhani serikali ya JPM imewapa go ahead, sote tunajua TUCTA iko mfukoni mwa serikali na hayo wanayofanya ni maigizo tu, kama kima cha chini kitapanda ni kwasababu serikali imeamua na sio mapendekezo ya TUCTA.

Uko sahihi kabisa, tena lengo hasa ni hadaa kwa ajili ya uchaguzi wa 2020. Hao TUCTA wanajifanya tu kama wanajadili lakini ukweli hawajadili lolote bali wameshaambiwa na kiwango kabisa, halafu ipigwe propaganda kuwa rais ni msikivu. Ila ukweli ni Hadaa kwa wafanyakazi kwa ajili ya uchaguzi ujao wa 2020.
 
Mie wakati naoa Mke wa pili 1994 nilizungumza nae Pembeni nikamwambia uwezo wangu wa kulipa Mahari Ni kiasi gani

Alichofanya kilipoitishwa kikao Cha Familia Yao kupendekeza Mahari aliwasilisha kiwango ambacho Mie naweza kulipa Kama ndio proposal yake

Iliporudi kwangu nami nikakubali Bila ya kusita Familia Yao ikaona imepata Mkwe Kweli Kweli maana siku burgain Mahari waliyopendekeza bali nililipia yote kwa mkupuo mmoja

Vilaza watasema nimetoka Nje ya Mada kwa Kuwa mjadala Ni nyongeza ya Mshahara Mie nazungumzia Posa

Aisee nimekuelewa sana.
Matumizi ya lugha safi bila maudhi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mie wakati naoa Mke wa pili 1994 nilizungumza nae Pembeni nikamwambia uwezo wangu wa kulipa Mahari Ni kiasi gani

Alichofanya kilipoitishwa kikao Cha Familia Yao kupendekeza Mahari aliwasilisha kiwango ambacho Mie naweza kulipa Kama ndio proposal yake

Iliporudi kwangu nami nikakubali Bila ya kusita Familia Yao ikaona imepata Mkwe Kweli Kweli maana siku burgain Mahari waliyopendekeza bali nililipia yote kwa mkupuo mmoja

Vilaza watasema nimetoka Nje ya Mada kwa Kuwa mjadala Ni nyongeza ya Mshahara Mie nazungumzia Posa
Nimekuelewa.TUCTA ni mke na Mkulu na muoaji si ndiyo

Ujumbe wako umefika, umetumia lugha ya tafsida, lakini ujumbe umeenea kabisa kwenye hii mada. Hao TUCTA ni wachekeshaji tu wa mfalme.
 
Mie wakati naoa Mke wa pili 1994 nilizungumza nae Pembeni nikamwambia uwezo wangu wa kulipa Mahari Ni kiasi gani

Alichofanya kilipoitishwa kikao Cha Familia Yao kupendekeza Mahari aliwasilisha kiwango ambacho Mie naweza kulipa Kama ndio proposal yake

Iliporudi kwangu nami nikakubali Bila ya kusita Familia Yao ikaona imepata Mkwe Kweli Kweli maana siku burgain Mahari waliyopendekeza bali nililipia yote kwa mkupuo mmoja

Vilaza watasema nimetoka Nje ya Mada kwa Kuwa mjadala Ni nyongeza ya Mshahara Mie nazungumzia Posa

Nimekuelewa sana
 
TUCTA wamezinduka kutoka ICU...!! What a joke to workers..!!! Wanacheza sana na maisha ya wafanyakazi hawa TUCTA..!!
 
BARAZA Kuu la Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (Tucta) linatarajia kukutana Aprili 2, 2019 ambapo pamoja na mambo mengine, litajadili mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara.

Akizungumza na gazeti hili Jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alisema kuwa, baraza hilo pia litajadili maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya ambapo Rais, Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Alisema kwa sasa Kamati maalumu ya kushughulikia mishahara iliweza kufanya utafiti kuhusiana na hali halisi ya maisha kwa sasa, kima cha chini cha mishahara wanaopata wafanyakazi, gharama za pango na matumizi mengine ili waweze kuleta mapendekezo yao.

“Kuna kamati maalumu ya mishahara ambayo ipo kwa mujibu wa katiba yetu, inafanya kazi ya kuangalia hali halisi ya maisha ya wafanyakazi kwa sasa, kima cha chini cha mshahara wanaopata, gharama za pango na nauli na matumizi mengine wanayokumbana nayo, wanatarajia kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika Aprili 2 mwaka huu,” alisema Nyamhokya.

Aliongeza, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo, wataweza kuangalia kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta zote binafsi na serikali ili waweze kuwasilisha mapendekezo yao kwa Rais Magufuli siku ya wafanyakazi.

Alisema, mpaka sasa, wafanyakazi wanapata kiasi kidogo cha mishahara ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya kila siku ukilinganisha na kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema licha ya kuwasilisha mapendekezo ya kuiomba serikali kuongeza kima cha chini cha mshahara ili uweze kufikia 750,000 kwa wafanyakazi wa serikali, lakini mpaka sasa bado wanapokea Sh 375,000.

“Wafanyakazi wa serikali wanapata kima cha chini cha mshahara kuanzia Sh 375,000 na kuendelea, huku sekta binafsi wakipata kuanzia Sh 100,000 kwa mwezi kulingana na ofisi anayofanyia kazi,” alisema.

Aliongeza, kiasi hicho ni kidogo na kwamba hakiwezi kukidhi gharama za maisha, jambo ambalo limechangia kujitokeza kwa malalamiko ya kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema, lakini pia wameiomba serikali kupunguza gharama za kodi inayokatwa kwenye mishahara yao ambayo imekua kero ya muda mrefu, jambo ambalo litasaidia kumpunguzia mzigo mfanyakazi kutokana na hali ngumu ya maisha.

http://mtanzania.co.tz/tucta-kujadili-kima-cha-chini-cha-mshahara/amp/
TUCTA wastaafu wenu mbona hamuwatetei? Au mnasubiri wakitetewa na wengine ndilo nyie mjichomeke kama mlivyofanya kwenye kikokotoo? Kumbukeni walipokuwa kazini mlijichana na michango yao ya lazima.
Hata hivyo inaelekea kunajambo limeandaliwa huko Mbeya kwa akili ya kupaishana kisiasa kati ya CCM na TUCTA tusubiri yajayo yanafurahisha.
 
Swala LA kupunguza kodi kwa watumishi tunaopokea kima cha chini haitusaidii chochote. Na pia kuhusu utaratibu unaofanywa na tukta kuhusu urekebishwaji wa mishahara naona. Ni komedi kwani itakua siasa tupu tumedanga nywa Mara ngapi? Kule Kilimanjaro alituahidi kua mishahara na stahiki zote za mtumishi wa umma zitakua nzuri .hatukuona chochote hadi Leo. Vilevile akasema kuhusu watumishi wa darasa LA saba hatawagusa kwani elimu yao ndio hiyo hawakudanganya watabakia kwenye ajira zao .matokeo yake wakaondolewa kwa ghafla mno mithili ya kifo hadi Leo kisa hawana cheti cha form 4. Ajabu hii .OK walipeni basi fedha walizokua wanachangia kwenye mifuko ya hifadhi wapeni kama mmewakataa lakini hawajapata chochote wanalia mno ni dhambi isiyofutika.wana kosa gani? Waliajiriwa kisheria kwa kufuata taratibu zote hadi check no walikuanazo Barua za Ajira, Barua za udhibitisho zote kwa pamoja zipo. Kwa nini unyama huu ufanyike na nchi yetu sote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko Sahihi Mkuu...
Pigania hili Mkuu..
Lipigie Kelele Mkuu lianzishie Unzi halafu uwa tag wahusika wakuu wa Nchi!
Kwani mwenyekiti wa tume ya Waziri Mkuu ya kuboresha mishahara anasemaje?

Point hapo ni kuwa na scale za mishahara inayofanana no matter what. Kama Engineer II basi atalipwa sawa na Wahandisi wenzake wote wa Daraja II awe Halmashauri/Wizarani/Tanesco/Tarura/Tanroads/ N.K

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom