tamuuuuu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2014
- 22,201
- 29,764
Mkuu ikigijo suala hili liko kwenye meza ya Waziri Mkuu na ameshateua watu kwenye tume ya kuboresha mishahara ambao wanaendelea na kulichakata.Uko Sahihi Mkuu...
Pigania hili Mkuu..
Lipigie Kelele Mkuu lianzishie Unzi halafu uwa tag wahusika wakuu wa Nchi!
Sent using Jamii Forums mobile app
1.) Sijasema kama wanafanya bila hiari yao.Wao wenyewe wameamua kwa hiari yao kufanyishwa kazi wewe kipi kinakuwasha.Wewe unaye fanya kazi kwanini hawakuonei wivu?,acha wivu wa kike.
Huu upbvu wa kima cha chini ni mwendelezoo wa sias zil zile za hovyo, yani unkuta dereva mwenye taauma yake kasomea hadi daraja la pili mshar wake ulingan na mfaiaji eti kwa kuwahat mfagiaji anastahili kima cha chini.BARAZA Kuu la Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (Tucta) linatarajia kukutana Aprili 2, 2019 ambapo pamoja na mambo mengine, litajadili mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara.
Akizungumza na gazeti hili Jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alisema kuwa, baraza hilo pia litajadili maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya ambapo Rais, Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Alisema kwa sasa Kamati maalumu ya kushughulikia mishahara iliweza kufanya utafiti kuhusiana na hali halisi ya maisha kwa sasa, kima cha chini cha mishahara wanaopata wafanyakazi, gharama za pango na matumizi mengine ili waweze kuleta mapendekezo yao.
“Kuna kamati maalumu ya mishahara ambayo ipo kwa mujibu wa katiba yetu, inafanya kazi ya kuangalia hali halisi ya maisha ya wafanyakazi kwa sasa, kima cha chini cha mshahara wanaopata, gharama za pango na nauli na matumizi mengine wanayokumbana nayo, wanatarajia kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika Aprili 2 mwaka huu,” alisema Nyamhokya.
Aliongeza, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo, wataweza kuangalia kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta zote binafsi na serikali ili waweze kuwasilisha mapendekezo yao kwa Rais Magufuli siku ya wafanyakazi.
Alisema, mpaka sasa, wafanyakazi wanapata kiasi kidogo cha mishahara ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya kila siku ukilinganisha na kupanda kwa gharama za maisha.
Alisema licha ya kuwasilisha mapendekezo ya kuiomba serikali kuongeza kima cha chini cha mshahara ili uweze kufikia 750,000 kwa wafanyakazi wa serikali, lakini mpaka sasa bado wanapokea Sh 375,000.
“Wafanyakazi wa serikali wanapata kima cha chini cha mshahara kuanzia Sh 375,000 na kuendelea, huku sekta binafsi wakipata kuanzia Sh 100,000 kwa mwezi kulingana na ofisi anayofanyia kazi,” alisema.
Aliongeza, kiasi hicho ni kidogo na kwamba hakiwezi kukidhi gharama za maisha, jambo ambalo limechangia kujitokeza kwa malalamiko ya kupanda kwa gharama za maisha.
Alisema, lakini pia wameiomba serikali kupunguza gharama za kodi inayokatwa kwenye mishahara yao ambayo imekua kero ya muda mrefu, jambo ambalo litasaidia kumpunguzia mzigo mfanyakazi kutokana na hali ngumu ya maisha.
http://mtanzania.co.tz/tucta-kujadili-kima-cha-chini-cha-mshahara/amp/
We jamaa unaakili sana. Me si mumunyi bali nafafanua tu. Wanachofanya TUCTA ni maigizo. Maigizo yaliyoratibiwa na wanaetaka kumsafisha (Mdaiwa) Serikali. Ipo hivi kwakuwa viongozi wa TUCTA ni mamluki wa Govt, wametumwa kufanya maigizo hayo ya kujifanya wanapendekeza mishahara na kuwasilisha mapendekezo. Kama kawaida jamaa wa Korosho atajifanya kupokea mapendekezo na kuyakubali au kuongeza kidogo na yeye kisha walioandaliwa wataripuka na maandamano ya kupongeza. Uchaguzi huo watu kama kawa iyena, iyena. Wameshasahau maumivu yote ndipo sasa unaingia awamu ya kumaliza hiyo hatuna cha kuogopa.Mie wakati naoa Mke wa pili 1994 nilizungumza nae Pembeni nikamwambia uwezo wangu wa kulipa Mahari Ni kiasi gani
Alichofanya kilipoitishwa kikao Cha Familia Yao kupendekeza Mahari aliwasilisha kiwango ambacho Mie naweza kulipa Kama ndio proposal yake
Iliporudi kwangu nami nikakubali Bila ya kusita Familia Yao ikaona imepata Mkwe Kweli Kweli maana siku burgain Mahari waliyopendekeza bali nililipia yote kwa mkupuo mmoja
Vilaza watasema nimetoka Nje ya Mada kwa Kuwa mjadala Ni nyongeza ya Mshahara Mie nazungumzia Posa
Mkuu Kuna watu/Watumishi wengine mmemaliza nao mwaka mmoja,kada moja wanakula Maisha kwenye sekta/Taasisi za Serikali na Miposho balaa....angalau tuwe pamoja Mkuu!Mkuu ikigijo suala hili liko kwenye meza ya Waziri Mkuu na ameshateua watu kwenye tume ya kuboresha mishahara ambao wanaendelea na kulichakata.
Sina hakika kama litakuwa lina mashiko au ni kwaajili ya Political gain. Tusubiri
Sina hakika kama itafanana kwa 100%, kuna taasisi nyingine za Serikali zinazalisha faida wakati Taasisi nyingine ni kutoa huduma.Mkuu Kuna watu/Watumishi wengine mmemaliza nao mwaka mmoja,kada moja wanakula Maisha kwenye sekta/Taasisi za Serikali na Miposho balaa....angalau tuwe pamoja Mkuu!
Wote tunahudumia Wananchi/Wote ni Watumishi wa Umma,LA Sivyo Wote tutahamia huko kwao.....Ofisa ugavi,Engineer,Wanasheria,HR,Civil tufanane Mkuu,labda tutofautiane kidogoooo kwenye Posho!
Lakini Mshahara tuwe pamoja,Posho ziwe Flat tufanane!
LA sivyo Kuhama hama hakuepukiki!
Sent using Jamii Forums mobile app
Napendekeza tucta ifutwe ili hiyo 2% irudi kwenye mshahara wa mfanyakaziBARAZA Kuu la Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (Tucta) linatarajia kukutana Aprili 2, 2019 ambapo pamoja na mambo mengine, litajadili mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara.
Akizungumza na gazeti hili Jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alisema kuwa, baraza hilo pia litajadili maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya ambapo Rais, Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Alisema kwa sasa Kamati maalumu ya kushughulikia mishahara iliweza kufanya utafiti kuhusiana na hali halisi ya maisha kwa sasa, kima cha chini cha mishahara wanaopata wafanyakazi, gharama za pango na matumizi mengine ili waweze kuleta mapendekezo yao.
“Kuna kamati maalumu ya mishahara ambayo ipo kwa mujibu wa katiba yetu, inafanya kazi ya kuangalia hali halisi ya maisha ya wafanyakazi kwa sasa, kima cha chini cha mshahara wanaopata, gharama za pango na nauli na matumizi mengine wanayokumbana nayo, wanatarajia kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika Aprili 2 mwaka huu,” alisema Nyamhokya.
Aliongeza, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo, wataweza kuangalia kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta zote binafsi na serikali ili waweze kuwasilisha mapendekezo yao kwa Rais Magufuli siku ya wafanyakazi.
Alisema, mpaka sasa, wafanyakazi wanapata kiasi kidogo cha mishahara ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya kila siku ukilinganisha na kupanda kwa gharama za maisha.
Alisema licha ya kuwasilisha mapendekezo ya kuiomba serikali kuongeza kima cha chini cha mshahara ili uweze kufikia 750,000 kwa wafanyakazi wa serikali, lakini mpaka sasa bado wanapokea Sh 375,000.
“Wafanyakazi wa serikali wanapata kima cha chini cha mshahara kuanzia Sh 375,000 na kuendelea, huku sekta binafsi wakipata kuanzia Sh 100,000 kwa mwezi kulingana na ofisi anayofanyia kazi,” alisema.
Aliongeza, kiasi hicho ni kidogo na kwamba hakiwezi kukidhi gharama za maisha, jambo ambalo limechangia kujitokeza kwa malalamiko ya kupanda kwa gharama za maisha.
Alisema, lakini pia wameiomba serikali kupunguza gharama za kodi inayokatwa kwenye mishahara yao ambayo imekua kero ya muda mrefu, jambo ambalo litasaidia kumpunguzia mzigo mfanyakazi kutokana na hali ngumu ya maisha.
http://mtanzania.co.tz/tucta-kujadili-kima-cha-chini-cha-mshahara/amp/
Sina hakika kama itafanana kwa 100%, kuna taasisi nyingine za Serikali zinazalisha faida wakati Taasisi nyingine ni kutoa huduma.
Kwahiyo nina wasiwasi jambo hili kama litatokea.
Usemacho kina mashiko sana Chief, ndiyo maana Waziri Mkuu ameunda timu maalum ya kulekebisha hizo dosali na kuja na scale zinazofanana.Sawa Kama watalipwa kulingana na Uzalishaji vipi Kuhusu Madaktari,Walimu?
Kuna Taasisi Kama Takukuru,mahakama,Ardhi,nk zinazotoa huduma inakuwaje?mifuko ya Hifadhi ya jamii,nk.
Hapo Inakuwaje?
Key factors iwe unachozalisha au Professional yako?
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio fadhila, ipo kisheria1.) Sijasema kama wanafanya bila hiari yao.
2.) Kinachoniwasha mimi ni wao kudai mishahara inayotokana na kodi zetu kana kwamba hiyo mishahara/ posho ni haki yao ilhali ni fadhila tu wanafanyiwa.
3.) Siwezi kuona wivu kufanyishwa kazi, no way aisee..
Uelewa wako ndo umekomea hapo,kwahiyo wewe ulitegemea washinde kutwa nzima kazini halafu wasilipwe?,Kama mfanyakazi wa nyumbani anayekula, anatibiwa. na kula kwa mwajiri wake,bado anaona anacholipwa ni kidogo,inakuwaje kwa mfanya kazi?.upende usipende kodi yako itaendelea kuliwa na wafanyakazi mpaka utakapo kufa.Wewe kazi yako ni kulipa kodi,ukishalipa serikali inapanga matumizi,ikiwa ni pamoja na kuwalipa wafanyakazi.1.) Sijasema kama wanafanya bila hiari yao.
2.) Kinachoniwasha mimi ni wao kudai mishahara inayotokana na kodi zetu kana kwamba hiyo mishahara/ posho ni haki yao ilhali ni fadhila tu wanafanyiwa.
3.) Siwezi kuona wivu kufanyishwa kazi, no way aisee..
1.) Sijasema washindwe kutwa nzima halafu wasilipwe, ninachosema ni wafanye kazi ili kujipatia riziki. (Wafanye kazi).Uelewa wako ndo umekomea hapo,kwahiyo wewe ulitegemea washinde kutwa nzima kazini halafu wasilipwe?,Kama mfanyakazi wa nyumbani anayekula, anatibiwa. na kula kwa mwajiri wake,bado anaona anacholipwa ni kidogo,inakuwaje kwa mfanya kazi?.upende usipende kodi yako itaendelea kuliwa na wafanyakazi mpaka utakapo kufa.Wewe kazi yako ni kulipa kodi,ukishalipa serikali inapanga matumizi,ikiwa ni pamoja na kuwalipa wafanyakazi.
Pili ulishawahi kuishughulisha akili yako hata kidogo kufikiri kuhusu nchi itakavyokuwa bila kuwa na watumishi wa umma?ama bado wewe ni mtoto,au ni zao la elimu ya vitin vya akina Nyambari.
umenena vyema mkuu, TUCTA ni branch ya ccmnadhani serikali ya JPM imewapa go ahead, sote tunajua TUCTA iko mfukoni mwa serikali na hayo wanayofanya ni maigizo tu, kama kima cha chini kitapanda ni kwasababu serikali imeamua na sio mapendekezo ya TUCTA.