TUCTA: Kima cha chini cha mshahara kiwe 970,000

Watumishi wa umma wanajiona kama wapo wenyewe tu sijui hawajui ni 0.6% ya raia wote? Huu upuuzi wa kudai laki 9.7 ni Seriikali gani hii itakayolipa hyo pesa? Hv wanajua impact ya mshahara kupanda huku mitaani ?
Kwahiyo hutaki mshahara upande ? Kila mmoja alie na lake waacheni watoto wa watu waombe jasho lao
 
Dah ikifika hapo,sisi tusioajiriwa tutapata tabu sana,maana mpaka dau la kuhonga litapanda sana.
 
Uwanja CCM KIRUMBA siyo ukumbi wa CCM KIRUMBA
 
Icho kiwango kinawezekana kabisa, ila black tunanyonywa sana, na vile elimu tunayopewa ni ili tuendelee kuwa wajinga hatutakaa kulipwa icho kiwango, nishafanya kazi na wazungu wanomlipa mfanya usafi laki 4 na bima ya afya juu.
 
Huyo kwenye picha mwanzoni mwa uzi huu ndiye nani? Kwa jina cheo kwenye hiyo TUCTA?
 
Walikuwa wanataka 315,000
 
Wafanyakazi wameharibwa akili wajione maskini.

Ukienda TANESCO, NSSF, BOT, PSSSF, TIC, TANROADS mshahara wa 970,000 analipwa mfagizi/mhudumu wa ofisi.

Waaalimu na wafanyakazi wengine wa Halmashauri waliharibiwa sana akili zao na CCM ili wajione wanyonge. Ndio maana wanarogana kisa kwenda kusimamia na kusahihisha mitihani.

Msechu pale NHC alikuwa anapokea milioni 30 kwa mwezi bado posho n.k hadi JPM akaona wivu akamtimua. Wabunge milioni 13 kwa mwezi na ni watanzania kama sisi.
 


Maskini kumbe wanaroganaga kwaajili ya hayo duh!

Sasa nikuulize mpendwa ;

Huo mfano wa Mchechu naona haufanani sana na ulichokisema sababu hiyo nafasi na Mchechu ni ya mtu mmoja tu pengine nchi nzima au kama wapo wengine hata 10 hawafiki kwenye nchi ya watu 60M

Sasa nikuulize Idadi wa Walimu nchi wako wangapi?
Kila Kuanzia mtaa, kata, tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla?

Hata hivyo bado niko pamoja na wewe kuwa idadi ya wingi isiwe hoja.

Bado tumeona pesa za Umma zikitumika vibaya mfano kwenye Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba, ufisadi mbalimbali n.k

Tuvumilie huku tukiendelea kufanya kazi kwa juhudi,maarifa , weledi na uadilifu tutafika salama.
 
EVEN HERE AT EUROPE WE ARE PAID HIGH BUT ALSO LIVING COST ARE HIGH SALARY WONT EVER BE ENOUGH,
*Tuongeze mshahara pia tupandishe petrol na diesel kidogo, intelligent know how to fix it.
 
Huyu nae ni mweu tu,hizo pesa zitoke wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…