Tuchunguze ni sehemu gani zinapata ajali mara kwa mara tuweke speed camera

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,925
31,850
Habari JF,

Leo nimekumbuka rafiki yangu wa utotoni alipata ajali akafariki, aligongwa na kuburuzwa na lori, nimefikiria nchi yetu bado inakua, hivyo vitu kama CCTV kwa kila sehemu ni vigumu na sio kipaumbele kwa sasa ila tuchunguze ni sehemu gani zinapata ajali mara kwa mara hizo sehemu ndio tuweke speed camera.

I think tutapunguza ajali tukifanya hivi.
 
Utapata wachangiaji wawili tu, lakini umeongea point nzuri sana.

Sijui kwanini watu hawaguswi na mambo ya msingi kama haya.

Wana taka kusikia sijui hamorapa na mambo kamahayo.
 
Ni kweli kabisa mtoa mada, na nchi hii ina wataalamu wengi sana wa usafirishaji na mambo ya barabara...Na hilo jambo linawezekana kabisa hata kwa nchi nzima

Ila tatizo linakuja kuwa Haohao wasomi wanakumbatia siasa na wale wanasiasa ndio wasemaji wa kila kitu.... Kazi za kitaalamu zinafanywa na wanasiasa..

Kingine cha ajabu wenye madaraka hawapendi wajuzi na wataalam kutoka hapahapa nchini...Kandarasi zinatolewa kwa wachina, wajapani, wajerumani,wacanada n.k..

Hamna kitu kinanikera hapa Tanzania kama wanasiasa kuingilia kazi za wataalam na kujifanya wao ndio kila kitu...Ajira zikikosekana wanawaambia Vijana mjiajiri...Aaah shit.... !!

Anyways Pole kwa msiba wa Rafiki yako!!
 
Uingereza kuna kipindi walizima Camera zote za barabarani Oxford gharama za kuziendesha siyo mchezo
Ndio itakuwa sisi ambao mlo mmoja tu mbinde ? Bado tuna safari ndefu sana

Pole kwako na R.I.P rafiki yako
 
siku tukiweza kutofautisha siasa na ujuzi tutafika mbali sana
Kweli Kabisa hasa Tanzania yaani..utakuta hao wajuzi wengi kwa mfano serikalini..Ni wataaalam lakini maisha yao yote ni siasa tu....Yaani kujitoa kwenye siasa atumikie taifa kwa utaalamu wake inakuwa kaaaazi kwelikweli
 
itachukua muda sana
 
Uingereza kuna kipindi walizima Camera zote za barabarani Oxford gharama za kuziendesha siyo mchezo
Ndio itakuwa sisi ambao mlo mmoja tu mbinde ? Bado tuna safari ndefu sana

Pole kwako na R.I.P rafiki yako

mkuu ni expensive lakini ita save lives,

hakuna kitu chenye gharama kubwa kama uhai,

halafu sio sehemu zote,ni sehemu zile tu zinaonyesha kupata ajali mara kwa mara,
 
mkuu ni expensive lakini ita save lives,

hakuna kitu chenye gharama kubwa kama uhai,

halafu sio sehemu zote,ni sehemu zile tu zinaonyesha kupata ajali mara kwa mara,
Mkuu hii Tanzania umepata wasaha wa kuitembelea vizuri ? Unafanya mchezo watu wanakunywa maji na mifugo sehemu moja ,kuna vifo vya wamama wajawazito na watoto kwa kukosa huduma za afya
Uhai kwa Watanzania sio gharama ni kama kuku tu kafa na maisha yanaendelea ,tuna safari ndefu sana kufikia kutambua uhai ni gharama sembuse kufunga camera

Anyway ni mtazamo tu
 
Hapa ndipo nauona umuhimu wa kuwa na watu kama wewe humu JF. Ulichosema kina maanakubwa sana lakini ni ngumu sana kufanyika kwa nchi yetu kwa sasa na hata likifanyika kuna watu watakuja kudai kuwa sio kipaumbele cha watanzania.
Chukulia mfano wa ununuzi wa ndege kila kona watu walipinga wakidai sio kipaumbele.
Kuna umuhimu mkubwa wa hilo usemalo lakini sioni uwezekano wa kufanyika.
 
Mkuu hii Tanzania umepata wasaha wa kuitembelea vizuri ? Unafanya mchezo watu wanakunywa maji na mifugo sehemu moja ,kuna vifo vya wamama wajawazito na watoto kwa kukosa huduma za afya
Uhai kwa Watanzania sio gharama ni kama kuku tu kafa na maisha yanaendelea ,tuna safari ndefu sana kufikia kutambua uhai ni gharama sembuse kufunga camera

Anyway ni mtazamo tu
Hayo unayosema ni kweli lakini je unafahamu ajali zinaondoa maisha ya watanzania wangapi kwa siku?
 
Tumewekeza sana kudhibiti mambo ya kijinga, nilishangazwa sana 2015 kila wiki ajali 2 mpaka 3 alafu serikali inaungana nasi eti kumuomba mungu ajali zipungue , are you seriouz? Hivi unamuomba mungu wakati gari mbovu ina overspeed barabara mbovu dereva kalewa.
 
mkuu ni expensive lakini ita save lives,

hakuna kitu chenye gharama kubwa kama uhai,

halafu sio sehemu zote,ni sehemu zile tu zinaonyesha kupata ajali mara kwa mara,
Mkuu acha kabisa umenitonesa machungu waanze na pale kibamb hospital jamn pameondoka na dam yangu upumzike kwa amani mdogo wangu kipenzi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom