Tubadili mfumo wa kuwakilisha wananchi bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tubadili mfumo wa kuwakilisha wananchi bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mapinduzi, May 16, 2010.

 1. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ni muda mrefu sasa uwakilishi wa wananchi hasa bungeni hauna mwongozo (uregulated). Raia mmoja anaweza kuwa mbunge kwa zaidi ya miongo minne. Ni ukweli usiopingika kuwa mwakilishi wa wananchi bungeni anachaguliwa na wananchi. Iwe kwa rushwa, kihalali, kwa huruma (wananchi wanamhurumia kwani analia sana wakati anaomba kura), kwa vitisho nk.

  Imefika wakati uwakilishi wa wananchi bungeni uwe na mwongozo (sheria). Kikomo cha ubunge kiwekwe. Hii itasaidia kuongeza uwajibikaji na heshima kwa wananchi.

  Pia iwekwe sheria ambayo haitalazimu mbunge kuwakilisha wananchi wake kwa kipindi cha miaka mitano. Kwa mfano, ikatokea kuwa baada ya miaka miwili au mitatu mwananchi wameona kuwa mbunge wao hawawakilishi ipasavyo kama alivyoahidi, wananchi wawe na nguvu ya kumhoji. Pale atakaposhindwa kujibu maswali ya wananchi anaowawakilisha bungeni ipasavyo au anapowadharau, basi wananchi wapewe nguvu ya kisheria kupiga kura ya kusitisha uwakilishi wa mbunge wao na kuchagua mbunge mwingine (ikishindikana kufanya uchaguzi basi ateuliwe na wananchi) kwa namna ambayo sheria itaona ni muafaka.

  Nawasilisha hoja.
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kuweka kikomo kwenye ubunge hai make sense kwangu na sija wahi kuona nchi yoyote duniani yenye kikomo katika uwakilishi wa wa Bunge. Katika mifumo mingi haswa yetu viongozi wakuu wa nchi pamoja na raisi na waziri mkuu huwa chimbuko ni bungeni. Mtu ana kuwa mbunge kwanza na kupanda ngazi. Sasa basi ukiweka kikomo cha ubunge tuseme iwe vipindi viwili(nasema vipindi viwili kwa maana hamna haja ya kusema kikomo iwe miaka ishirini au zaidi because that would be non sense) una create matatizo yafuatayo.

  1)Una discourage vijana kuongia kwenye siasa haswa wale wenye ambitions za kwenda mbali zaidi kwa sababu hawata ona sababu ya kupoteza muda na kuwa mbunge kwa muda mchache tu.

  2)Unaondoa experience factor inayo hitajika kwenye uongozi mkubwa zaidi. Kwa sababu ina maana raisi au viongozi wakuu ambao wote hutokea bungeni ina bidi wawe watu wenye limited experience.

  Hoja yako ya wananchi kumhoji na kuweza kumuondoa mbunge hiyo ni kitu ambacho tayari kipo. Wananchi wakiona hafai wana haki na uwezo wa kuto kumpigia kura kwenye uchaguzi ujayo na hiyo ni nguvu ya mpiga kura kisheria. Sasa labda ufafanue ulitaka wananchiwawe na nguvu zipi zaidi kisheria linapo kuja swala la kumwajibisha muwakilishi wao.
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Unasema kuweka kikomo kwenye kipindi cha ubunge haki-make sense kwa sababu hakuna nchi duniani imeweka kikomo cha ubunge na kukatisha tamaa vijana?

  Kuhusu kuweza kumhoji na hata kumuondoa mbunge, je una sheria yeyote au ni kwa kutumia mazoea?
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Ama nime kupa sababu mbili ya kwa nini kuweka kikomo haimakse sense. Na nika kuambia kabisa kwamba kutokana na mfumo wetu viongozi wakuu wa serikali wana tokana na bunge. Kwa hiyo ukilimit term ya ubunge pia una limit the experience one gets before becoming president. Na sheria ya kumuondoa mbunge nisha kuambia ni kura ya wananchi. Wananchi wakiona mbunge hafai hawampigii kura. Au kwako wewe kura si hehemu ya sheria mkuu?

  I see your suggestion working only if we had a completely new system which would mean an overhaul of everything not only the Parliament.
   
 5. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Imefika wakati tutafute utatuzi wa matatizo yetu kwa kutafuta sustainable solution ya matatizo yaliyopo.
  Tumeona matatizo mengi sana yanayotokana na mfumo huu. Hii inaonyesha wazi kuwa mfumo uliopo umefail.

  Kama kura ni sehemu ya sheria, sijaona wapi imewezesha kumwajibisha mbunge asiyetekeleza majukumu yake ipasavyo? Naomba kipengele cha sheria kinachoelezea baada ya kupiga kura nini kifuate, hasa kwa upande wa mpiga kura. I mean, huyu mpiga kura atafuatiliaje utendaji wa aliyempigia kura? Any checks and balances kwa mbunge?
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Labda niulize mswali moja mkuu. What checks and balances would you suggest. Una taka mpiga kura awe na uwezo gani wa kumuwajibisha mgombea wake baada ya hiyo kura. Inge kuwa wewe una tunga sheria kuhusu mpiga kura kumuajibisha mbunge wake zaidi ya kumpigia kura ya hapana unge weka vipengele gani. Because you might be on to something na mimi itakuwa sijawa objective kudismiss your ideas moja kwa moja.
   
Loading...