Tuanze upya mchakato wa Katiba Mpya

Tuanze upya mchakato wa Katiba Mpya

Shakidinkili

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
458
Reaction score
174
Nianze kwa kukumbuka mwaka 1971 nikiwa Kijana. Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ilikusanya maoni ya wananchi nchi nzima kuhusu MAKAO MAKUU YA CHAMA NA SERIKALI KUHAMISHIWA DODOMA. Sina uhakika kama maoni hayo yalikusanywa pia Zanzibar, ila cha msingi hapa ni kuwa uliwekwa utaratibu mzuri kwa wakati ule wa kuwafikia wananchi walio wengi na walitoa maoni yao kwa maandishi. Walio wengi walikubaliana na makao makuu ya nchi kuhamia Dodoma japo mpaka leo viongozi wamepiga danadana na kuzidi kujiimarisha D'salaam.

Tulipofikia kwenye kutunga Katiba mpya sioni dalili ya kupatikana kwa katiba mpya itakayokidhi matarajio ya Watanzania walio wengi, sababu kubwa ninazoziona mimi ni

1.Kuendekezwa kwa malumbano na vijembe visivyo na tija.
2.Kubezwa kwa kundi moja kwa kudaiwa ati wana uroho wa kupata madaraka.
3.Ujinga wa kundi jingine wa kujiona wao wana hati miliki ya kukaa madarakani daima dumu milele na wana mamlaka zaidi kwa wananchi.

Mengi yamesemwa hata kufikia hatua ya kuibeza Tume ya Warioba, kuhoji weledi wao na kudai kuwa utaratibu walioutumia kupata maoni ya wananchi haukuwa sahihi na taarifa zao hazina uhalisia. Tunajua fika kuwa wajumbe wa Tume ya Warioba hawapo Bungeni na wao sio sehemu ya Bunge maalum la Katiba. Nionavyo mimi, Wajumbe wa Bunge la Katiba katu hawawatendei haki Wajumbe wa Tume ya Warioba kwa misingi kuwa hawapo Bungeni, hivyo hawawezi kufafanua lolote wala kujibu hoja, pasipo kusahau kuwa Kanuni za Bunge zinamlinda Mbunge kwa hayo atayosema akiwa Bungeni na kumzuia mtu wa nje ya Bunge kujibu mapigo.

NINI KIFANYIKE ILI KUINUSURU KATIBA MPYA?

1.Mchakato wa Katiba mpya usimamishwe ili tujipange upya kwa haya yafuatayo.
2.Tujiridhishe kuwa Tume ya Uchaguzi ni Chombo huru kitakachotenda haki, kitasimamia haki na ukweli.
3.Tume huru ya Uchaguzi iboreshe daftari la wapiga kura nchi nzima.
4.Uandaliwe utaratibu maalum utakaosimamiwa na Tume huru ya Uchaguzi ili kupata maoni ya Wananchi kuhusu yafuatayo. Sio vibaya wala sio dhambi tukijikumbusha utaratibu uliotumika kupata maoni ya Wananchi kuhusu makao makuu ya nchi kuhamia Dodoma mwaka 1971.

Maoni ya wananchi yapatikane kwa kutumia dodoso kama hili hapa chini au lililoboreshwa zaidi.

(a)Je unautaka muungano wa Tanganyika na Zanzibar? (i)NDIO. (ii) HAPANA.
(b)Kama jibu lako hapo juu ni ndio, Je unataka muungano wa namna gani? (i)Serikali moja. (ii)Serikali mbili. (iii)Serikali tatu.(iv)Mkataba.

Tuchukue SIMPLE MAJORITY kwa kila upande wa muungano kuwa ndio washindi na uwe ndio mwongozo Mkuu wa kuandikwa kwa Katiba mpya. Endapo upande mmoja wa muungano utakataa muungano, basi hakuna haja ya kulazimishana kwa kuwa unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji. Kama pande mbili za muungano zichagua aina tofauti za muungano, basi hapo itakuwepo haja ya kuundwa kamati ya maridhiano yenye watu waadilifu na wenye nia njema na nchi hii, wanaoguswa na uzalendo halisi pasipo kuingiza itikadi za kisiasa kama ilivyo sasa kwenye Bunge maalum la Katiba ili wapate muafaka wa muungano uwe wa aina gani.

Ninashawishika kuamini kwa kutumia utaratibu kama huu, tunaweza kuondokana na ombwe hili la kupatikana kwa Katiba mpya. Tuachane na mawazo au nia ya kupata Katiba mpya kabla ya uchaguzi ujao wa 2015. BETTER LATE THAN NEVER. Ndani ya hili Bunge maalum la Katiba, wapo wajumbe ambao wamejipambanua katika hoja zao kuwa wao ni wazalendo halisi na wanaitakia mema nchi hii na mawazo yao au michango yao inajenga hoja na hawana vijembe kwa kundi lolote.

Muafaka wa aina ya muungano ukipatikana ninaamini vurugu zitakwisha. Mambo ya muungano yawe yale yaliyoafikiwa na Waasisi wa muungano ambayo yamo kwenye hati ya Muungano na tujumuishe na yale yote yaliyokuwa yanaendeshwa na Jumuia ya Afrika ya Mashariki iliyovunjika mwaka 1977.
 
watakula tu pesa ya kodI zetu tu.......syo kwa viongozi waliyopo sasa
 
Katiba tuliyonayo ni mbaya, uzuri wake unategemea na utashi, weledi na ubinadamu wa Rais aliyeko madarakani.

Katiba yetu hii ni tamu sana kwa Rais na genge lake kwakuwa inamruhusu kufanya apendavyo bila kizuizi chochote kutuka kwa MTU au taasisi yoyote.

Kwa wale waliokuwepo wakati wa tawala zote tangu ile ya wakoloni, Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, na Magufuli mtagundua kuwa viongozi wote hawa walitofautiana sana katika kuiongoza nchi ingawa wengi wao walitoka CCM.

Mkoloni alikuwa na ubepari, Nyerere alijuwa mjaa aliyetaifisha mali za watu na kutapanya hela zetu katika ukombozi wa nchi nyingine ambazo sasa hivi hazitujali kabisa, Mwinyi akikuwa bepari kwa kulifuta azimio la Arusha, Mkapa akikuwa bepari aliyeuza mashirika, viwanda, nyumba za serikali, na kila kitu, Kikwete alikuwa nusu bepari na nusu mjamaa akiamini kwenye nguvu ya wahisani na magufuli alikuwa mjamaa akairudisha serikali kwenye kufanya biashara. Kila Rais alikuwa akiwateua kila mtu kwenye nafasi kubwa. Kwana marais waliozitumia nafasi zao kuteua mashemeji, ndugu zao, marafiki wao, wapwa zao, hawala zao, na jamaa zao kwenye nafasi mbalimbali.

Kuna baadhi yao waliigombanisha nchi na mataifa mengine

Huu ni ushahidi kuwa hata kama tule manyasi lazima tuandike Katiba mpya ambayo nguvu za Rais zinaweza kuwekewa checks and balance na taasisi nyingine za kikatiba.
 
Back
Top Bottom